MWISHO LINI KUFANYA MAPENZI/TENDO LA NDOA KWA MJAMZITO.

MWISHO LINI KUFANYA MAPENZI/TENDO LA NDOA KWA MJAMZITO.

MWISHO LINI KUFANYA MAPENZI/TENDO LA NDOA KWA MJAMZITO.

Tendo la Ndoa ni mojawapo ya starehe muhimu sana kwa afya ya mwanadamu vile vile huongeza uimara wa mahusiano baina ya mke na Mume, japokuwa Tendo la Ndoa katika kipindi cha Ujauzito huweza kubadilika kulingana na Mjamzito mmoja na mwingine.

Je Mjamzito Mwisho lini kushiriki Tendo la Ndoa ktk Ujauzito wake?

Mjamzito anaweza kufanya Tendo la Ndoa kama kawaida mwanzoni mwa Ujauzito yaani kuanzia Miezi Mitatu ya Mwanzoni, Katikati na Mwishoni mwa Ujauzito hadi anapokaribia kuweza kujifungua.

Baadhi ya Wajawazito hupunguza hamu au shauku ya kufanya Tendo hilo katika kipindi cha Ujauzito kitu ambacho huwapa wakati mgumu wenzao wao, hali ya kupungua kwa hamu ya Tendo la Ndoa hutokea Mjamzito tangu anapokuwa na Mimba ya Miezi Mitatu ya Mwanzoni mwa Ujauzito na wakati mwingine Miezi Mitatu ya mwishoni mwa Ujauzito.

Miezi Mitatu ya Mwanzoni mwa Ujauzito, Baadhi ya Wajawazito hupunguza hamu ya Tendo hilo kutokana na mabadiliko mbalimbali Mwilini mwao mfano Ongezeko la baadhi ya Homoni na mabadiliko mengine kama: Mabadiliko ya mudi, kichefuchefu au kutapika, Maumivu ya Chuchu, Kuchoka sana na kujisikia vibaya na nk

Miezi Mitatu ya katikati mwa Ujauzito,Akina Mama wajawazito wengi waliopoteza hamu ya Tendo la Ndoa Miezi 3 ya Mwanzoni mwa Ujauzito wao hamu ya Tendo la Ndoa huweza kurudi kama kawaida na kuendelea kufurahia starehe ya Tendo la Ndoa na wenza wao, hii ni kwa sababu baadhi ya mabadiliko ya Homoni huweza kupungua kidogo ukilinganisha na Mwanzoni mwa Miezi 3 ya Ujauzito wao, japokuwa kuna baadhi ya Wajawazito huweza kuendelea kukosa hamu ya Tendo la Ndoa ktk Miezi 3 ya katikati mwa ujauzito pia ni hali ya kawaida kabisa wala haihitaji kuwa na hofu.

Miezi Mitatu ya mwishoni mwa Ujauzito, Baadhi ya Wajawazito hupata Maumivu ya Kiuno, Kichefuchefu na Maumivu ya Tumbo, Maumivu Ukeni na nk, ambayo huweza kupelekea baadhi ya Wajawazito kutokuwa na hamasa ya kufanya Tendo la Ndoa kitu ambacho ni kawaida pia, japokuwa kuna baadhi wanaweza kuwa vyema na wakaendelea kushiriki Tendo la Ndoa kama kawaida katika kipindi hiki cha Mwishoni mwa Ujauzito.

Pamoja na hayo yote wako Wajawazito wachache ambao hupata hamu kubwa ya kushiriki tendo la Ndoa na waume zao kuliko kipindi ambacho hawakuwa wajawazito kitu ambacho ni kawaida na haina shida yoyote.

Habari Njema!

Mjamzito anaweza kufanya Tendo la Ndoa kipindi chote cha Ujauzito wake kuanzia Mimba inapokuwa na wiki 1 hadi Mimba inapokuwa imekomaa na kipindi ambacho anaelekea kujifungua(Wiki 37 hadi 42), japokuwa kuna Mambo ambayo yanaweza fanya Mjamzito asishiriki tendo la Ndoa hata kama ana hamu au shauku ya kufanya Mapenzi au kushiriki Tendo ndo la Ndoa na mwenza wake.

MJAMZITO USISHIRIKI TENDO LA NDOA KAMA UNA SIFA HIZI.

Mama Mjamzito hatoruhusiwa kushiriki Tendo la Ndoa hata kama anapata hamu au shauku ya kufanya Tendo hilo katika kipindi cha Ujauzito ikiwa ana sifa au Mambo yafuatayo;

  1. Kutokwa Damu Ukeni katika kipindi chochote cha Ujauzito.
  2. Mimba Kutishia Kuharibika ktk kipindi cha Ujauzito
  3. Historia ya Mimba kuharibika mara kwa mara kabla ya Wiki 28.
  4. Historia ya kujifungua au kuzaa mapema kabla Mimba kukomaa (Chini ya Wiki 37 hadi 42).
  5. Kondo la Nyuma/Zalio kujishikiza karibia na Mlango wa Uzazi au Kujishikiza kwenye Mlango wa Uzazi.
  6. Udhaifu wa Mlango wa Uzazi au Mlango wa Uzazi mfupi kuliko kawaida (Chini ya Sentimenta 2.5).
  7. Chupa kupasuka mapema kabla ya Uchungu.
  8. Mume au Mwenza wa Mjamzito mwenye Maambukizi ya Magonjwa ya Zinaa.

KUMBUKA: Mjamzito kama una Wenza zaidi ya Mmoja au Mpenzi mmoja ambaye si mwaminifu ni vema kutumia Kondomu ili kujikinga na Magonjwa ya Zinaa katika kipindi chote cha Ujauzito wako.

Response to "MWISHO LINI KUFANYA MAPENZI/TENDO LA NDOA KWA MJAMZITO."

  • Mkewangu kwenye dalili 30 yeye ana dalili28 lakin alienda kupima akakutwa Hana mimba na Kuna siku amejikuta anatoka dam Yani kama anaingia kwenye cku shida apo ni nini

  • Habari tatizo langu nikuwa mke wangu ananiambia kuwa ujauzito wake uko inje ya mfuko wa uzazi so hataki kufanya mapenzi , je nikweli huturuhusiwi kufanya mapenzi??

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *