Mfungo/Kufunga kwa Mjamzito.
Mjamzito anaruhusiwa kufunga katika kipindi cha Ujauzito kama akina Mama wengine wasio Wajawazito?
Jibu ni HAPANA!!!,
MJAMZITO HURUSIWI KABISA KUFUNGA AU KUFANYA MFUNGO KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO WAKO, KUTOKANA NA SABABU ZIFUATAZO!
Unapokuwa Mjamzito huwa kuna mabadiliko mengi yanayotokea mwilini mwako, Mabadiliko hayo kama;
- Ongezeko la uhitaji wa nishati kwa Mjamzito, Mjamzito unahitaji nishati zaidi ya 340kcal kila siku ukilinganisha na ulipokuwa si Mjamzito, ili kukidhi mahitaji ya Mtoto aliyeko tumboni haswa miezi Mitatu ya katikati mwa Ujauzito na kuendelea.
- Ongezeko la uhitaji wa Maji kwa Mjamzito, Mjamzito unahitaji kiwango cha Maji zaidi ya Mililita 300 kila siku ukilinganisha na kiwango cha Maji ulipokuwa si Mjamzito.
- Mjamzito unahitaji Mlo kamili kila siku ili kuwa na afya bora wewe mwenyewe na Mtoto aliyeko tumboni katika kipindi chote cha Ujauzito wako.
- Mjamzito unatakiwa kutumia Dawa lishe (Folic acid/Vitamin B-9 na Madini Chuma/Iron) kila siku katika kipindi chote cha Ujauzito wako, inategemeana na matumizi ulivyoandikiwa na Dawa zako, wako wengine huhitaji kutumia dawa hizo mara mbili au mara tatu kwa siku badala ya mara moja kila siku.
- Mjamzito unahitajika kuongezeka Uzito kwa wastani kutokana na BMI yako katika kipindi chote cha Ujauzito na nk.
- Mjamzito mwenye Magonjwa mbalimbali kutokana na mabadiliko ya Ujauzito mfano; Kisukari cha Ujauzito na nk.
Kutokana na sababu hizo Mjamzito huruhusiwi kufunga katika kipindi cha Ujauzito wako, endapo utafunga katika kipindi cha Ujauzito wako unaweza kupata changamoto zifuatazo;
- Mjamzito unapofunga katika kipindi cha Ujauzito wako, Uzito wako unaweza kupungua badala ya kuongezeka, kitu ambacho si salama katika afya ya Ujauzito wako.
- Kujifungua Mtoto chini ya Uzito, Baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba Wajawazito wanaofunga vipindi virefu katika Ujauzito mfano; Kufunga zaidi ya masaa 18 wanaweza kujifungua Mtoto chini ya Uzito (chini ya kilo 2.5) ukilinganisha na wale wasio funga.
- Kujifungua kabla ya wakati, Wajawazito wanaofunga katika Ujauzito wao, wako kwenye hatari ya Kujifungua kabla ya Wiki 37 au kabla Mimba haijakomaa.
- Kupata ukavu wa mwili, Mjamzito unapofunga na kutokunywa Maji ya kutosha muda mrefu unaweza kuwa na ukavu wa mwili, ambao huweza kukusababishia kupata maumivu ya Kichwa mara kwa mara au UTI ya kujirudia rudia katika kipindi cha Ujauzito.
- Hali ya Kutapika na kichefuchefu kuongezeka zaidi, Endapo umefunga na hunywi Maji ya kutosha muda mrefu huweza kupata ukavu wa mwili pia ambao huweza kupelekea hali ya kichefuchefu na kutapika kuongezeka zaidi.
- Mjamzito kama una Magonjwa mbalimbali mfano; Ugonjwa wa Kisukari kutokana na Ujauzito huruhusiwi kufunga na endapo unatumia dawa za Ugonjwa huo.
Baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba Mama Mjamzito unaweza kufunga katika Ujauzito wako haswa Miezi Mitatu(3) ya Mwanzoni mwa Ujauzito kwa sababu kunakuwa na mabadaliko kiasi kidogo ulikinganisha na vipindi vingine vya Ujauzito wako!.
MAMA AFYA BORA; Tunasema Mjamzito usifunge wale kufanya mfungo katika kipindi chote cha Ujauzito wako ili kuepuka madhara kutokana na Kufunga katika Ujauzito wako.
Bonyeza link hii kusikiliza video
No comments.