Hedhi ya Kichanga wa Kike/Kutokwa Damu Ukeni Kwa Kichanga wa Kike.

Hedhi ya Kichanga wa Kike/Kutokwa Damu Ukeni Kwa Kichanga wa Kike.

Hedhi ya Kichanga wa Kike/Kutokwa Damu Ukeni Kwa Kichanga wa Kike.

Hedhi ya Mtoto Mchanga wa Kike (Neonatal Uterine Bleeding), Hali hii huitwa hedhi ya Uongo Kwa Watoto Wachanga wa Kike ambayo hutokea ndani ya Wiki 1 toke kuzaliwa kwao,

Hii hutokea pale ambapo Mtoto Mchanga wa Kike hutokwa Damu Ukeni, hali hii hutokea kati ya siku ya 3 hadi siku ya 10 tokea Mtoto Mchanga wa Kike azaliwe.

Kikawaida Damu hiyo huonekana Ukeni mara nyingi Mtoto Mchanga wa Kike Mtoto akiwa na Umri wa Siku 3 hadi 4 na badae huweza kupotea siku ya 5, 6,7 au 8 na huwa hazidi siku 10, Damu hiyo hutoka kwa kiasi kidogo sana ambayo Mama anaweza kuona kwenye Mashavu ya Uke ya Kichanga wake!

Hali hii huweza kuwa kuwapa Vichanga wa Kike 3 hadi 5 kati ya Vichanga wa Kike 100 ambapo akina Mama wa Vichanga hao huweza kuona kabisa Damu, Ingawa wakati mwingine Vichanga wa Kike 40 hadi 50 kati ya 100 huweza kupata hali ya kutokwa Damu bila Damu kuonekana Ukeni Vichanga hawa kwa akina Mama zao, labda kwa sababu Damu hiyo imerudi nyuma (Retrograde reflux) na kutokea Tumboni (Peritoneal cavity).

SABABU ZA HEDHI YA UONGO KWA VICHANGA WA KIKE.

Hali hii ni hali ya kawaida kabisa kwa baadhi Vichanga wakike hutokea kutokana na sababu kubwa Moja tu ambayo ni;

Kupungua kwa homoni (Estrogen na Progesterone) za Mama kwenye Mwili wa Mtoto Mchanga ambazo ziliongezeka kipindi ambacho Mtoto alikuwa Tumboni mwa Mama yake katika kipindi cha Ujauzito, Mtoto anapokuwa Tumboni mwa Mama yake, Homoni hizo huweza kuongezeka kwenye mwili wa Mtoto kutoka kwa Mama yake angali Mjamzito kwa kupitia Kondo la Nyuma na kwenda kwa Mwanae Tumboni.

Mtoto Mchanga wa Kike anapozaliwa homoni hizo hupungua na kupelekea Kichanga wa Kike kupata hali ya kutokwa Damu Ukeni kama hedhi ambayo Kitalaam huitwa Hedhi ya Uongo kwa Kichanga wa Kike.

Hali hii ni hali ya kawaida kabisa kutoka kwa baadhi ya Vichanga wa Kike hivyo Mama au Mlezi uonapo hali hii hupaswi kuwa na wasiwasi mkubwa japokuwa ni vema kwenda hospitali ila Daktari akuthibitishie kama hali hiyo ni hedhi ya Uongo au lah.

Ziko sababu nyingine ambazo zinazoweza kusababisha Kichanga wa Kike kutokwa Damu Ukeni mfano; Upungufu wa Vitamini K, Kichanga wa Kike kuumia Ukeni mara chache sana, Shida za Kushindwa kuganda kwa Damu kwa Mtoto Mchanga na nk.

Hedhi ya Uongo ni hali ya kawaida kabisa,Ijapokuwa Wazazi wa Kichanga wa Kike aliyepata hedhi ya Uongo ndani ya wiki 1 tokea kuzaliwa kwake mnapaswa kuhakikisha kwamba mnaweka kumbukumbu ya kwamba Mtoto wenu alipata hiyo hali akiwa Kichanga ili ikitokea shida ya Uzazi katika maisha ya Mtoto huyo hapo badae katika maisha yake itakuwa rahisi kugundulika,

Hivi karibu kuna tafiti zimeonesha kwamba kuna baadhi ya Vichanga wakike wanaopata hedhi ya Uongo damu huweza kutoka na kurudi nyuma na kuingia tumnboni mwao hivyo huweza kupelekea baadhi ya seli kuzaliana tumboni na Mtoto huyo kupatwa na shida ya Uzazi iitwayo (Endometriosis) na huweza kupelekea shida za uzazi ukubwani mwa Mtoto huyo mfano; kukosa Mtoto, Shida za Ujauzito, kupata maumivu makali ya tumboni bila shida yoyote kugundulika na nk.

VIHATARISHI VINAVYOWEZA KUPELEKEA HEDHI YA UONGO KWA VICHANGA WA KIKE. Pamoja na kwamba hali hii ni ya kawaida yako baadhi ya Mambo yanaweza kuhatarisha Kichanga wako kuweza kupata hali hii ya hedhi ya Uongo ndani ya Wiki Moja tokea kuzaliwa kwake,

Vihatarishi hivyo vimehusishwa ya kwamba hupekelea hali ya Msongo au changamoto ya muda mrefu kwa mtoto anapokuwa tumboni mwa Mjamzito kabla ya kuzaliwa, Vihatarishi ni kama;

  1. Kichanga aliyezaliwa na Mjamzito aliyekuwa na dalili za kuelekea kuwa na Kifafa cha Mimba au Presha kubwa sana (Pre-eclampsia).
  2. Kichanga aliyezaliwa na alikuwa na Udumavu Tumboni mwa Mjamzito (Intra-Uterine Growth Restriction).
  3. Kichanga aliyezaliwa ila alikuwa na Uzito Mdogo tumboni Mwa Mjamzito kulinganisha na Umri wa Mimba ya Mjamzito (SGA).
  4. Kichanga aliyezaliwa baada ya Tarehe ya Matarajio au Mtazamio yaani zaidi ya Wiki 40 na kuendelea (Post-term).
  5. Kichanga aliyezaliwa na Mjamzito mwenye shida za kutokana na Utofuati wa Makundi ya Damu na Mumewe (RH & ABO incompatibility) na nk.

Kumbuka; Hedhi ya Uongo kwa Kichanga wa Kike ni hali ya kawaida kabisa Mzazi usiwe na wasiwasi endapo Kichanga wako amepata hali hiyo, ila ni vema kuweka kumbukumbu ya kwamba Mwanao alipata hali hiyo kipindi alipokuwa Kichanga ili ikitokea shida ya Uzazi Maishani mwa Mwanao inakuwa rahisi kujua shida ni ipi hata hivyo bado tafiti zinafanyika ili kubaini kama hali hii inaweza kuwa shida zaidi……..

Hedhi ya Uongo kwa Kichanga wa Kike

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *