HOMA YA MANJANO KWA MTOTO MCHANGA.

HOMA YA MANJANO KWA MTOTO MCHANGA.

Watoto wachanga walio wengi wanapokuwa wamezaliwa hususani wiki ya 1 tu ya maisha yao huwa na Unjano kwenye macho yao au kwenye ngozi zao.

Hali hii ya Unjano wa Macho ya Kichanga au Ngozi yake huitwa kitaalamu Jaundice ni dalili ya ongezeko kubwa la pigimenti iitwayo Bilirubin kwenye Damu kwa Mtoto Mchanga.

Huweza kupelekea Unjano kwa Watu wa zima endapo ongezeko la hii pigimenti kiwango cha kimekuwa kikubwa zaidi ya 2mg/dL .

Watoto wachanga huwa na Unjano kwenye macho na kwenye ngozi endapo kiwango cha pigimenti hii kimeongezeka kufikia 7mg/dL au zaidi.

  1. Kati ya Watoto wachanga wanaozaliwa Mimba zikiwa zimekomaa yaani wiki 37-41 basi 25%-50% ya Watoto wachanga hao huwa na Unjano wiki 1 ya mwanzoni mwa maisha yao.
  2. Kati ya Watoto Wachanga wanaozaliwa Mimba ikiwa haija komaa yaani chini ya wiki 37 basi 80% ya Watoto wachanga hao huwa na Unjano wiki 2 za mwanzoni mwa maisha yao.

Pigimenti hii iitwayo Bilirubin ni zao litokanalo na kuharibiwa au kuvunjwa vunjwa kwa protini zenye heme katika mwili wa mwanadamu mfano: Seli hai Nyekundu za Damu, Tishu za Misuli (Myoglobin), Cytochrome, Catalase na nk.

Seli hai Nyekundu za Damu zilizozeeka zinapovunjwa vunjwa kwenye mfumo wa Reticulo-endothelial System huzalisha kiwango kikubwa cha pigimenti ya Bilirubin ambayo hufikia 75%.

Bilirubin ambayo huzalishwa baada ya kuvunjwa vunjwa kwa Seli hai nyekundu za Damu kwenye mfumo wa RES huwa ni ile ambayo haijachakatwa na huitwa Unconjugated/Indirect Bilirubin hii huchukuliwa kwenda kwenye Seli za INI kupitia mishipa ya Damu ili kuweza kuchakatwa na kuzalisha Bilirubin ambayo imechakatwa iitwayo Conjugated/Direct Bilirubin ambayo hutolewa kwenye INI katika mchanganyiko wa kimiminika kiitwacho Bile ambayo huhifadhiwa kwenye kifuko cha Nyongo (Gall bladder) ambapo hutolewa kidogo kidogo kwenye mfumo wa chakula na hutoka kwenye Mwili wa Binadamu kupitia Choo/Kinyesi.

Bilirubin iliyochakatwa (Conjugated/Direct Bilirubin) inapoingia kwenye mfumo wa chakula kiwango fulani hubadilishwa na baaadhi ya Vijidudu waliopo kwenye Utumbo na kuwa Urobilinogen ambayo huweza kufyonzwa kwenye Utumbo kiwango fulani ambacho hurudi kwenye INI na kingine huenda kwenye Figo na kuchujwa na kuupa Mkojo rangi yake vile vile Baadhi ya urobilinogen hugeuzwa kuwa Stercobilin ambayo hukipa Choo/Kinyesi rangi yake hivyo Bilirubin hutoka kwa Mwili wa mwanadamu kupitia Choo/Kinyesi.

Kiwango fulani cha Bilirubin ambayo imechakatwa (Conjugated/Direct Bilirubin) kwenye Utumbo hugeuzwa na baadhi ya vimeng’enyishi vilivyomo kwenye utumbo na kuwa Bilirubin ambayo haijachakatwa (Unconjugated/ Indirect Bilirubin) ambayo hufyonzwa kwenye ukuta wa Utumbo kuingia kwenye Damu na kwenda kuchakatwa kwenye INI kwa mara ya pili kitendo hicho huitwa Enterohepatic Circulation yaani mzunguko unaohusu mzunguko wa bilirubin kutoka kwenye INI kwenda kwenye Utumbo na kurudi kwenye INI tena vivyo hivyo mara kwa mara hii ni muhimu kwa Mtoto Mchanga.

SABABU ZA KUWA NA UNJANO WA NGOZI AU MACHO KWA MTOTO MCHANGA.

Zifuatazo ni sababu kubwa Nne (4) zinazopelekea Unjano kwa Mtoto Mchanga ambazo ni:

  1. Unjano wa Macho au Ngozi kutoka na Mabadiliko ya kawaida ya Kichanga baada ya kuzaliwa (Physiological Hyperbilirubinemia) hii hutokana na Mtoto Mchanga kuwa viungo vyake haswa INI na nk kuto kukomaa na kushindwa kuchakatwa kwa Bilirubin na kufanya kuongezeka kwa bilirubin ambayo haijachakatwa (Unconjugated/Indirect Bilirubin).
  2. Maziwa ya Mama na vilivyomo ndani yake huweza kusababisha Unjano kwa Mtoto Mchanga.
  3. Ukose wa Maziwa ya Mama baada ya Kichanga kuzaliwa huweza kupelekea Unjano kwa Mtoto Mchanga.
  4. Unjano kutokana na ongezeko la Bilirubin ambayo imechakatwa (Conjugated/Direct Bilirubin) ambayo inawezekana kwa sababu ya Magonjwa mbalimbali, hitalafu ya Damu kwa Kichanga na nk.
Sikiliza Video ya sababu za Manjano kwa Mtoto Kichanga

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *