Matunda Hatari kwa Mjamzito na ktk Kipindi cha Ujauzito!.
Mjamzito anaweza kula Matunda ya aina nyingi sana katika kipindi cha Ujauzito wake, Pamoja na kwamba Mjamzito anaweza kula Matunda karibia aina zote, yako baadhi ya Matunda inasemekana huweza kuwa na hatari endapo yakitumika katika kipindi cha Ujauzito haswa Miezi Mitatu ya Mwanzoni mwa Ujauzito au Mimba.
Mjamzito anapaswa kutumia Matunda mbalimbali katika kipindi chote cha Ujauzito ili kuweza kupata Vitamini mbalimbali mfano; {Vitamini A,B1,B6,B9,C na K}, Madini Mbalimbali kama; Madini chuma, Magneziamu, Kalsiamu na nk, Huongeza sukari mwilini mwa Mjamzito, Huongeza nyuzi nyuzi kwa Mjamzito ili kupunguza choo kigumu katika kipindi cha Ujauzito na Virutubisho mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha afya ya Mjamzito na ukuaji wa Mtoto aliyeko tumboni mwa Mjamzito.
MATUNDA HATARI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO
Pamoja na faida zote hizo za Matumizi ya aina mbalimbali za Matunda katika kipindi cha Ujauzito, yako baadhi ya Matunda huweza kusababisha changamoto mbalimbali katika kipindi cha Ujauzito mfano; Kuharibika kwa Mimba, kupelekea Mimba kutishia kuharibika na kuleta uchungu wa mapema na nk.
Japokuwa hakuna tafiti za kutosha kuthibitisha kuwa kweli matunda hayo ni hatari katika kipindi cha Ujauzito ni vema kuepuka Matunda haya na kutumia mbadala au Kutumia Matunda haya mara chache zaidi na kwa kiasi kisogo haswa mwanzoni mwa Ujauzito (Miezi Mitatu ya Mwanzoni).
Matunda yafutayo ni matunda hatari katika kipindi cha Ujauzito ni vema kutumia kwa tahadhari kubwa, Matunda hayo ni kama;
- Papai; Kuna aina mbili za Papai ambazo ni Papai lililoiva na Papai lisiloiva, Mjamzito ni vema kutumia Papai lililoiva na usitumie Papai ambalo halija iva,
(a). Papai lililoiva huwa la Njano na huwa limelainika vizuri, Papai lililoiva ni tunda muhimu sana kwa Mjamzito kwa sababu husaidia kupunguza changamoto ya kuwa na choo kigumu na kufanya Mjamzito kupata choo laini vile vile huwa na Vitamini Mbalimbali kama Vitamini A (carotenoids), Kiwango kikubwa cha Vitamini C na vitamini nyingine kama B na madini mbalimbali kama Kalsiamu na nk.
(b). Papai lisiloiva huwa na rangi ya Kijani ambalo pia huwa halija lainika vizuri, Papai lisiloiva huwa na kiwango kikubwa cha Maji maji yenye kemikali iitwayo latex ndani yake, latex huwa na vimeng’enyishi vya aina mbili ambayo huitwa Papain na Chymopapain ambavyo huweza kupelekea mji wa uzazi kuanza kujikamua ambapo huweza kupelekea Mimba kuweza kutishia kuharibika, kuharibika au Kupata uchungu wa Mapema endapo Mjamzito huyo alitumia Papai lisiloiva kwa kiwango kikubwa zaidi.
- Nanasi; Tunda aina la Nanasi huwa lina kemikali iitwayo Bromelain ambayo hupatikana haswa sehemu ya katikati kabisa mwa Tunda hili la Nanasi, Tunda hili huwa na kiwango kikubwa cha Vitamini C na nk
Endapo Mjamzito atatumia Nanasi nyingi na kula mara kwa mara ile sehemu ya katikati ya Nanasi na kukiwa na ongezeko kubwa la Kemikali hii ya Bromelain huweza kupelekea kulainika kwa Mlango wa Mji wa uzazi kabla ya Uchungu na kupelekea Mimba kuweza kuporomoka yaani kuharibika ikiwa chini ya Wiki 28 au Kujifungua kabla ya wakati kama Mimba iko zaidi ya Wiki 28.
Hata hivyo hii huweza kutokea endapo Mjamzito ametumia kiwango kikubwa sana cha Nanasi katika kipindi chake cha Ujauzito,japokuwa hakuna tafiti za kutosha kwa wanadamu kuhusiana na hili, tafiti zilizofanyika ni kwa wanyama kama Panya.
- Zabibu Nyeusi (Zabibu za Kiwandani); Zabibu ni Tunda ambalo huwa na kiwango kikubwa sana cha Vitamini C kuna aina Mbalimbali za Zabibu kutokana na Matumizi japokuwa kuna aina kuu mbili Zabibu ya Kiwandani na Zabibu ya Meza.
(a). Zabibu ya Kiwanda, hii ni zabibu ya rangi nyeusi huwa na ngozi ngumu sana ambayo hutumika kutengeneza bia na wine viwandani, aina hii ya zabibu huwa na kiwango kikubwa cha kemikali iitwayo Resvaratrol ambayo hupatikana kwa wingi kwenye ngozi ya zabibu nyeusi endapo Mjamzito atatumia aina hii ya zabibu kwa wingi zaidi:
- Huweza kupelekea sumu kutokana na mrundikano wa kemikali hii na huweza kupita kupitia kondo la nyuma na kwenda kwa Mtoto aliyeko tumboni na kuweza kupelekea udumavu wa ukuaji wa Kongosho ya Mtoto,
- Huweza kupelekea ongezeko kubwa la Joto kwa Mjamzito haswa zabibu nyeusi ikitumiwa kwenye miezi mitatu ya mwishoni na kuleta changamoto,
- Huweza kupelekea kuharisha kwa Mjamzito kutokana na ufinyu wa kumeng’enywa kwa ngozi ngumu ya Zabibu nyeusi kwenye mfumo wa chakula.
(b). Zabibu ya Meza, Hii ni zabibu kwa ajili ya kula huwa zinaweza kuwa na rangi tofuati tofuati mfano rangi ya Kijani, Nyekundu na nk, hii Mjamzito anaweza kutumia bila shida yeyote huwa na kiwango kidogo sana cha kemikali iitwayo Resvaratrol.
Japokuwa hakuna tafiti zinazothibitisha ukweli haswa kuhusu madhara ya Zabibu nyeusi haswa kwa Mjamzito katika kipindi cha Ujauzito, unaweza kutumia kwa kiasi kidogo tu vile vile zabibu ya mezani huweza kutumika katika kipindi cha Ujauzito.
- Bitter Melon; (Tikiti Chungu), Tunda hili ni muhimu kwa Mjamzito huwa na kiwango kikubwa sana cha Vitamini C, Vitamini B-9 (Folate) na nyuzi nyuzi kwa wingi,
japokuwa tunda hili huweza kupelekea
- Mji wa Uzazi kujikamua na kupelekea Mimba kutishia kuharibika au Mimba kuharibika mapema,
- Huweza kupelekea kujifungua Mtoto mwenye ulemavu na
- Huweza kuepelekea changamoto za mmeng’enyo kwenye mfumo wa chakula wa Mjamzito kama kuharisha,Maumivu ya Tumbo na nk.
Mjamzito anaweza kutumia Tikiti Chungu katika kipindi cha Ujauzito kwa tahadhari kubwa ili kuepuka changamoto hizo kwa sababu hakuna tafiti za kutosha kuhusu Madhara ya tunda hili kwa Mjamzito.
- Ukwaju; Ukwaju ni Mojawapo ya Matunda pendwa kwa Wajawazito kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha Vitamini C, Kupunguza kichefu chefu katika kipindi cha Ujauzito, Huongeza nyuzi nyuzi ambazo hupunguza kuwa na choo kigumu kwa Mjamzito, hudhibiti sukari kwa Wajawazito wenye kisukari, hudhibiti presha kwa wajawazito wenye shinikizo kubwa la Damu na nk.
Japokuwa kuna imani za watu wanaosema kwamba Matumizi makubwa au Utumiaji wa Ukwaju mwingi huweza kupelekea ongezeko kubwa la Vitamini C kwa Mjamzito ambayo huweza kupelekea upungufu au kupunguzwa kwa homoni ya Progesterone na Mimba kuweza kuharibika au kutishia kuharibika haswa Mwanzoni mwa Ujauzito (Miezi 3 ya Mwanzoni Mwa Ujauzito) na hatari ya kujifungua kabla ya wakati.
Hakuna ukweli kuhusu ya kwamba ongezeko la Vitamini C hupelekea upungufu wa homoni ya Progesterone badala yake Ongezeko la Vitamini C mwilini hupelekea kuongezeka kwa homoni ya Progesterone, hivyo Mjamzito anaweza kutumia Ukwaju kwa kiasi kama kawaida katika Kipindi cha Ujauzito bila shida yoyote.
Mjamzito anaweza kutumia Matunda haya tajwa hapo juu cha msingi Mjamzito anatakiwa kuzingatia kwamba ni vema kutumia Matunda haya kwa kiasi cha wastani tu na mara chache sana katika kipindi cha Ujauzito,
Endapo una wasiwasi usitumie Matunda haya katika kipindi chote cha Ujauzito badala yake tumia Matunda Mbadala kama Parachichi, Fenesi, Embe, Ndizi, Peazi, Tufaa, Tunda Damu, Pera, Matikiti Maji, Chenza, Machungwa, Pasheni na nk.
Unaweza kuuliza maswali kwenye whatsapp au kwenye comment hapo chini, Karibu sana.
Response to "Matunda Hatari kwa Mjamzito na ktk Kipindi cha Ujauzito!."
Asante sana doctor umeelweka
Haya Mama
Jaman naomba kuuliza maan nishatuma msg sijibiwi
Unaweza kujifungua kabla ya tarehe ya makadirio na kwanini
Fuatilia video za Dr.Mwanyika pale youtube
Nimekuelew vema mama me mwenyew napenda ukwaju ila natumia tumbegu 2 had 3 kwa sku Niko saw. Je vipi kuhusu kuumwa kichwa sana
Naomba soma somo la Maumivu ya Kichwa kwa Mjamzito kwenye blog hii ya mamaafya.com