Je Mjamzito mwenyewe Mimba ya Mapacha hutakiwa kujifungua Mimba ikifikisha wiki ngapi?
Kuna aina nyingi sana za Mapacha lakini kuna aina kuu 3 za Mapacha ambazo ni kama zifuatazo;-
1. Mapacha wasio wa kufanana / Fraternal Twins
Hujumuisha 80% ya Mapacha wote katika Jamii,Hutokea Mara baada ya Mayai mawili ya kike kurutubishwa na Mbegu mbili za kiume tofauti tofauti katika Mzunguko mmoja wa Mfuko wa mayai ya mwanamke.
2. Mapacha wa kufanana/Identical Twins
Hujumuisha 20% ya Mapacha wote katika Jamii,Hutokea Mara baada ya Yai Moja la kike kurutubishwa na Mbegu moja ya kiume na badae kugawanyika kwa wakati tofauti tofauti.
Mapacha wa kufanana wamegawanyika katika makundi makuu 3.
A. Diamniotic- Diachorionic Twins
Hujumuisha 30% ya Mapacha wanaofanana ambao hufanyika siku 0 hadi siku ya 3 Mara baada ya Mimba kutungwa na hutokea Mara baada ya Kiini kugawanyika.
B. Diamniotic – Monochorionic Twins
Hujumuisha 70% – 75% ya Mapacha wanaofanana ambao hufanyika siku 4 hadi siku ya 8 Mara baada ya Mimba kutungwa na hutokea Mara baada ya Kiini cha ndani kugawanyika zaidi.
A. Monoamniotic – Monochorionic Twins
Hujumuisha 1% – 2% ya Mapacha wanaofanana ambao hufanyika siku 9 hadi siku ya 13 Mara baada ya Mimba kutungwa na hutokea Mara baada ya Kiini kugawanyika.
3. Mapacha walioungana viungo vyao/Conjoined Twins
Hujumuisha chini ya 1% ya Mapacha wote katika Jamii,Hutokea Mara baada ya hitilafu ya mgawanyiko wa mapacha wa kufanana au kuchelewa kugawanyika kwa kiini kuanzia wiki 2 kwenda juu mara baada ya Mimba kutungwa.Kiujumla Mama Mjamzito mwenye Mapacha anatakiwa kujifungua wiki 37 hadi 39 hatakiwi kupitiisha wiki 40, inaweza kupelekea watoto kufia ndani ya Tumbo lake.
Lakini ikumbukwe kwamba Siku au wiki za kujifungua hutofautiana kati ya Mapacha aina Moja na nyingine mfano;
1. Mama Mjamzito mwenye Mapacha aina ya Monoamniotic – Monochorionic anaweza kujifungua kuanzia wiki ya 32 hadi wiki ya 34.
2. Mama Mjamzito mwenye Mapacha aina ya Diamniotic – Monochorionic anaweza kujifungua kuanzia wiki ya 34 hadi wiki ya 37 au 37 na siku 6 hatakiwi kuzidisha wiki 38.
3. Mama Mjamzito mwenye Mapacha aina ya Diamniotic – Dichorionic anaweza kujifungua kuanzia wiki ya 37 hadi wiki ya 38 au 38 na siku 6 hatakiwi kuzidisha wiki 39.
Hii ni kwa sababu Mapacha wanawahi kukomaaa mapafu yao na endapo wako karibu zaidi basi hupata stress zaidi na kupelekea wao mapafu yao kuwahi kukomaa kuanzia wiki ya 31 hii hutofautiana na Mama Mjamzito mwenye Mimba ya mtoto mmoja ambapo mapafu huanza kukomaa kuanzia wiki ya 34.
Response to "Je Mjamzito mwenyewe Mimba ya Mapacha hutakiwa kujifungua Mimba ikifikisha wiki ngapi?"
Je mwanamke aliyekutana na mwanaume Tar 2 Mwezi wa 9 mwaka Jana anaweza kujifungua mapacha Tarehe 20 Mwezi wa 4 mwaka huu?
Nadhani tulizungumza whatsApp
Je umekutana na mwanaume tarehe 26/03 makadilio ya kujifungua mapacha Ni wiki ngapi
Download pregnancy calculate pale playstore itakusaidia kujua hilo
Soma hapo kwenye somo tafadhari