Upele wa Joto kwa Mtoto Mchanga | Vipele vya Joto Kwa Mtoto Mchanga (Miliaria).

Upele wa Joto kwa Mtoto Mchanga | Vipele vya Joto Kwa Mtoto Mchanga (Miliaria).

Upele wa Joto kwa Mtoto Mchanga | Vipele vya Joto Kwa Mtoto Mchanga (Miliaria).

Vipele vya Joto ni Ugonjwa wa kawaida wa ngozi unaosababishwa na kuzibwa na/au kuvimba kwa mifereji inayopitisha jasho kutoka kwenye tezi za Jasho, wakati mwingine huitwa Upele wa jasho.

Upele wa Joto huwapata watoto wachanga kaunzia umri wa wiki 1 au zaidi haswa wanaoishi katika mazingira yenye joto kali, unyevu na nk.

VISABABISHA NA VIHATARISHI VYA UPELE WA JOTO KWA MTOTO MCHANGA

Viko vihatarishi vingi na sababu nyingi zinazopelekea Upele wa Joto kwa Watoto wachanga mfano kama;

  1. Mazingira au hali ya hewa ya Joto kali.
  2. Kutokuwa na ukomavu wa mifereji ya Jasho kwa Watoto wachanga.
  3. Mazingira yenye unyevu mwingi unaochangiwa na Joto.
  4. Kumvisha Mtoto mchanga nguo nyingi.
  5. Kumvisha Mtoto mchanga nguo za kubana sana.
  6. Kumvisha Mtoto Mchanga nguo nzito zenye kuongeza Joto zaidi.
  7. Matumizi ya Mafuta ya Vaseline au Mafuta yoyote ya Mgando kwenye mazingira yenye joto kali.
  8. Mtoto Mchanga anayevishwa nguo zisizo za pamba (Nylon).
  9. Homa kwa Mtoto Mchanga na nk.

SEHEMU ZA MWILI WA MTOTO MCHANGA AMBAPO UPELE WA JOTO HUTOKEA.

Ziko sehemu mbalimbali ambapo upele huu wa Joto hutokea katika Mwili wa Mtoto Mchanga, sehemu hizo ni kama;

  1. Usoni (Kwenye paji la uso) mwa Mtoto Mchanga.
  2. Mabegani kwa Mtoto Mchanga.
  3. Kifuani au sehemu ya mbele ya kifua cha Mtoto Mchanga.
  4. Mgongoni au sehemu ya juu ya mgongoni kwa Mtoto Mchanga.
  5. Makwapani kwa Mtoto Mchanga.
  6. Sehemu mbalimbali za Kichwani.
  7. Kiunoni maeneo ambako pampasi au nepi hufungwa.
  8. Maungio ya Mapajani na nk.

JINSIA YA KUZUIA NA KUPUNGUZA UPELE WA JOTO KWA MTOTO MCHANGA.

Sababu kubwa za Upele wa joto kwa Watoto wachanga ni uwepo wa joto kali na unyevu katika mazingira yanayo mzunguuka Mtoto mchanga.

Mambo yakufanya ili kuweza kupunguza upele wa joto kwa Mtoto mchanga ni kutengezea uvuguvugu au ubaridi haswa katika mwili na mazingira yanayozunguuka Mtoto mchanga, ambayo ni kama;

  1. Epuka kumweka Mtoto Mchanga katika mazingira ya Joto kali.
  2. Epuka kumvisha Nguo nyingi Mtoto Mchanga haswa katika mazingira ya Joto kali.
  3. Epuka Kumvisha Nguo nzito kwa Mtoto Mchanga haswa katika mazingira ya Joto kali na unyevu mwingi.
  4. Mvishe nguo nyepesi za pamba Mtoto mchanga katika Mazingira ya Joto kali.
  5. Epuka kumvisha Nguo za kubana Mtoto Mchanga katika mazingira yenye joto kali.
  6. Ogesha Mtoto mchanga wako mara mbili au tatu kila siku kwa maji ya uvuguvugu zaidi ili kupunguza Joto la mwili kwa Mtoto Mchanga.
  7. Unaweza tumia kitambaa cha pamba na kuloweka kwenye maji ya ubaridi au vuguvugu na kumgusisha mwanao kwenye paji la uso wake endepo anatokwa na Jasho jingi sana.
  8. Fungua madirisha kuruhusu hewa kuingia na unaweza kuwasha feni kwa mwendokasi mdogo au Kiyoyozi ili kupunguza Joto kwenye chumba aliko Mtoto mchanga.
  9. Usitumie Mafuta ya Mgando kumpaka Mtoto Mchanga katika mazingira ya Joto kali.
  10. Unaweza kutumia Calamine lotion endapo kama Mtoto wako anaonesha ishara za kuwashwa ngozi yake.

MATIBABU YA UGONJWA HUU WA UPELE WA JOTO KWA WATOTO WACHANGA

Mtoto mchanga mwenye Upele wa Joto huweza kupona mwenyewe bila kuhitaji matibabu yoyote endapo utapunguza Joto kali kwenye mwili wake na Mazingira yanayo mzunguuka Mtoto Mchanga.

Endapo Mtoto Mchanga amekuwa na Homa kali yaani Joto la Mwili zaidi ya centigredi 38, Ngozi kuchubuka, Upele kutoa Usaha au Upele kuendelea kuongezeka ni vema kwenda hospitali kuonana na Daktari ili kuweza kuandikiwa Dawa za kutibu Ugonjwa wa Upele wa Joto kwa Mtoto Mchanga.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *