Je kutokwa Damu kipindi cha Ujauzito ni hatari? | Je unatokwa Damu wakati wa Ujauzito?? Fanya hivi!.

Je kutokwa Damu kipindi cha Ujauzito ni hatari? | Je unatokwa Damu wakati wa Ujauzito?? Fanya hivi!.

Je kutokwa Damu kipindi cha Ujauzito ni hatari? | Je unatokwa Damu wakati wa Ujauzito?? Fanya hivi!.

Je kutokwa na Damu kipindi cha Ujauzito ni dalili ya hatari?
Ndio,
Endapo Mimba yako ina umri wa chini ya wiki 28 sawa na miezi 7 na unatokwa na Damu hata kama hupati maumivu ya Tumbo hii huweza kuonesha kuwa Mimba yako inatishia kutoka au inawezekana tayari imekwisha kuharibika.

Kutokwa na Damu zaidi ya wiki 28 au Miezi 7 bila kupata maumivu yoyote ya Tumbo hii huonesha wazi kuwa inawezekana Kondo la Nyuma limejishikiza karibu na Mlango wa Uzazi.

Kumbuka:
Kutokwa na Damu katika mwezi wa kwanza wa Ujauzito, endapo ikiwa inafanana na siku ya Hedhi kabla ya kupata Ujauzito ijapokuwa Damu zinatoka kidogo na kwa siku chache huwa inatokana na Mimba baada ya kutungwa inapojishikiza kwenye Mji wa Uzazi.
Endapo hutokana na Hali hii Mimba inaposhikiza kwenye Mji wa Uzazi huwa ni hali ya kawaida unahitaji kwenda hospitali kwani si rahisi Mjamzito kugundua kuwa ana hiyo Hali bila usaidizi wa Daktari.

Unapo tokwa na Damu kipindi cha Ujauzito hata kama huna maumivu unatakiwa kwenda hospitali upewe Matibabu na vile vile hutakiwi kushiriki Tendo la Ndoa badala yake muda mwingi utatumia kulala na utatembea tuu unapokwenda haja na kuoga basi hii ni kwa Wajawazito wote wanaopata Dalili za kutokwa Damu wakati wa Ujauzito haijalishi umri gani wa Mimba.

Je Mara baada ya Mimba kuharibika natakiwa kufanya nini ili nipate Mtoto na nijifungue salama?.

Mambo ya kufanya ni kama:
1. Tambua kitu gani kimefanya Mimba kuharibika na ukiondoshe hicho kitu endapo kimegundulika. Kumbuka si lazima kuwe na sababu zinazojulikana wakati mwingine unaweza usipate sababu ya Mimba yako kuharibika maana inaweza kutokea tu.

2. Pata Matibabu stahiki kulingana na umri wa Mimba ilipoharibika lakini pia kulingana na Hali yako kiafya na Kimwili.

3. Unahitaji kutumia njia ya Uzazi wa Mpango kwa muda wa Miezi sita kama huna haraka ya kupata Ujauzito endapo unaharaka na Ujauzito unaweza kusubiri mpaka Miezi Mitatu ndipo upate Ujauzito mwingine.

4. Kipindi cha kusubiri kabla ya kupata Ujauzito utahitaji kutumia mlo kamili, Vitamini mfano folic acid na Madini Chuma na kuujenga Mwili wako kwa ajili ya kujiandaa na kubeba Mimba nyingine.

5. Unahitaji kujilinda na kuepukana na Magonjwa ya zinaa mfano Gono, kaswende na UKIMWI.

Je nikiwa na Ujauzito nahitaji kufanya mazoezi gani?.

Endapo wewe ni Mjamzito huhitaji mazoezi makubwa mfano kukimbia au kuruka ruka sana zaidi ya kutembea tembea na kufanya shughuli ndogo ndogo za nyumbani kama kupalilia maua,kulima Mboga Mboga, kufagia, kuosha vyombo na kufanya mazoezi ya kunyoosha viungo katika kipindi cha Ujauzito wako.

Unaweza kujifunza kwa kupitia video hapa YouTube.


Response to "Je kutokwa Damu kipindi cha Ujauzito ni hatari? | Je unatokwa Damu wakati wa Ujauzito?? Fanya hivi!."

  • Je mjamzito kutokana na damu nyingi katika siku zilezile za hedhi na kwa zaid y cku saba na kwa mfululizo wa miez 3. Nabado kipimo cha utlasound kinaonyesha mtoto bado yumo na anamapigo ya moyo je hii inamadhara kwa mtoto atakae zaliwa baadae?

  • Samahani nimepima nikakuta nina mimba ya wiki mbili ila baadae nimeingia period kabla ya siku zangu. Je hiyo inaweza ikawa tatizo?

  • Sor niko nje ya mada kidogo ila nahitaji msaada kusema kweli nilimeza dawa za kutoa mimba misoprosto lakini niliona matone machache ya damu then inatulia nikifanya kazi naona matone ya damu afu yanakata yanatoka tena sehemu nyingine actual siyo damu nyingi ni matone machache mimba ilikuwa ya wiki 3 naomba ushauri naogopa kwenda hospital

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *