MIMBA ISIYOKUWA NA KIINI (BRIGHTEN OVUM).

MIMBA ISIYOKUWA NA KIINI (BRIGHTEN OVUM).

MIMBA ISIYOKUWA NA KIINI (BRIGHTEN OVUM).

Mimba isiyo na Kiini ni aina ya Mimba ambayo hutokea baada ya Yai la kike lilorutubishwa ambalo hugawanyika na kushindwa kufanyika kwa Kiini ipasavyo ambapo huweza kujishikiza kwenye ukuta wa Mji wa Uzazi na kushindwa kukua kwa Mimba na mwisho wa siku Mimba huharibika au kutoka yenyewe.

Aina hii Mimba huweza kuwapata baadhi ya akina Mama katika kipindi cha maisha yao na hupelekea Mimba kuharibika ndani ya Miezi Mitatu au ndani ya wiki 12  za mwanzoni mwa Ujauzito na hujumuisha 50% kati ya Mimba zote zinazo haribika katika kipindi cha Ujauzito.

Mimba ya aina hii huweza kugundulika baada ya kufanya Ultrasound,ina maana bila Ultrasound huweza kugundulika kuwa una Mimba isiyo na kiini.
Hatima ya Mimba hii huwa ni kuharibika au kutoka  yenyewe, japokuwa Baadhi ya wanawake huhitaji Matibabu ya Dawa au kusafishwa kwa ajili ya kutoa Uchafu unaobaki kwenye Mji au Mfuko wa Uzazi.

Je Mimba isiyo na Kiini husababishwa na Nini?
Vitu vinavyopelekea aina hii ya Mimba ni Kama:-

1.Hitilafu kwenye Vinasaba.
Aina hii ya Mimba huweza kusababishwa na hitilafu ya Vinasaba hususani wakati wa ugawanyikaji na ukuwaji wa Kiini kinacho unda Kijusi katika hatua za mwanzo za ufanyikaji wa Mtoto Tumboni mwa Mjamzito.

2. Visababishi visivyo julikana.
Ukweli ni kwamba sababu inayopelekea kufanyika Mimba isiyo na Kiini bado hajajulikana vizuri.

Je Mimba isiyo na Kiini hugundulikaje.?
Kama ilivyoandikwa hapo juu aina hii ya Mimba hujulikana tuu endapo Mjamzito alifanyiwa Ultrasound, aina hii ya Mimba huwa na dalili za Mimba kama kawaida mfano:
1. Kupata kichefu chefu au kutapika asubuhi pindi Mjamzito anapoamka.
2. Kupata maumivu ya Matiti au kuhisi Matiti kujaa.
3.Kuhisi harufu Mbaya.
4. Kutoona hedhi yako.
5. Kuchoka Mara kwa Mara na kujisikia vibaya.
6. Kukojoa Mara kwa Mara.
7. Chuchu kuwa na rangi nyeusi.
8. Kutokwa na Damu Kama matone matone.
9. Kupata maumivu ya kubana na kuachia kwa muda fulani au Maumivu ya kiuno.
10. Kipimo Cha Mimba Cha Mkojo kuonesha kuwa ni Mjamzito.

Endapo Mjamzito atapa Dalili hizi za Ujauzito za kawaida na akaamua kwenda kufanya Ultrasound ndipo aina hii ya Mimba huweza kugundulika au endapo Mjamzito amepata Dalili za Mimba kutishia kutoka au kutokwa na Damu ukeni anapoamu kwenda kufanya Ultrasound ndipo huweza kugundulika kwa aina hii ya Mimba.

KUMBUKA: Aina hii ya Mimba huweza kugundulika kwa bahati mbaya endapo Mjamzito aliamua kufanya Ultrasound kama Mimba hiyo haikuwa na dalili za kutishia kutoka, Mimba hii huweza kutoka au kuharibika yenyewe bila Mjamzito kujigundua kuwa ni Mjamzito.

Je Matibabu yake yakoje?
Endapo umegundulika una Mimba isiyo na Kiini kwa kawaida Matibabu hutegemea na mhudumu wa Afya(Daktari) unayekutana nae na maamuzi yako wewe Kama Mgonjwa.
Matibabu yamegawanyika katika aina kuu tatu.
1. Kusubiri Mimba hiyo itoke yenyewe,
Kama ilivyoelezewa hapo juu kuwa hatima ya Mimba ya aina hii ni kutoka yenyewe bila kuhitaji Matibabu yaani utahisi maumivu ya Tumbo ya kubana na kuachia na Mwisho wa siku Uchafu hutoka wenyewe cha msingi tu utahitaji kufatiliwa kwa ukaribu na Daktari wako kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya Mimba yako.

2. Kupewa Dawa za kufungua Mlango wa Uzazi na kuchochea utolewaji wa Uchafu kutoka kwenye Mji wa Uzazi kupitia Mlango wa Uzazi.

3. Kusafishwa kwa kutumia Vifaa vitakavyoingizwa kwenye Mji wa Uzazi kwa ajili ya kutoa Uchafu kabla ya kusafishwa utahitaji kutanuliwa kwa Mlango wa Uzazi au  kupewa Dawa kwa ajili ya kufungua Mlango wa Uzazi.

KUMBUKA:
Hivyo matibabu hutegemea maamuzi ya Daktari wako na wewe kama mgonjwa bila kusahau na Hali uliyo nayo katika kipindi hicho, hivyo Matibabu hutofautiana kati ya Mtu mmoja na mwingine.

Je baada ya Mimba isiyo na Kiini kuharibika au kutoka naweza kubeba Mimba tena?
Ndio, Unaweza kubeba Mimba nyingine Mara baada ya Mimba kutoka na kuweza kujifungua Mtoto salama kabisa.

Utahitaji tuu kupumzika kwa muda wa angalau Miezi 6 bila kubeba Mimba ili kupumzisha mwili na Mji wa Uzazi.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *