MTOTO HUANZA KUCHEZA LINI KATIKA TUMBO LA MJAMZITO.
Kwa kawaida akina Mama wajawazito huwezi kuhisi kucheza kwa mtoto tumboni katika umri tofauti tofauti kulingana Mama Mjamzito husika.
1. Mama Mjamzito ambaye hakuwahi kujifungua kwa maana kwamba Mimba yake ni Mimba ya kwanza,huwezi kuanza kuhisi mtoto kucheza tumboni kuanzia miezi 4½ hadi miezi 5.
2. Mama Mjamzito ambaye amewahi kujifungua au kubeba mimba Mara mbili au Mara tatu huweza kuhisi mapema zaidi kucheza kwa mtoto tumboni ambapo huhisi mtoto kucheza kuanzia miezi 4 au miezi 4½ ukilinganisha na wale ambao ni Mara ya kwanza kuwa na Mimba.
👉Ni vema kujua kwamba unapofikia umri huo wa mimba kuanzia miezi 4 kwenda juu uweze kuhisi mtoto akicheza tumboni na kama hata cheza baada ya umri huu utatakiwa kuwahi hospitali kupata vipimo zaidi.
❤️Kuanzia wiki ya 28 au miezi 7 ni muhimu mama kuhesabu kucheza kwa mtoto kila siku, endapo Mama Mjamzito huyu anaumwa magonjwa kama Kisukari,Magonjwa ya Moyo au shida nyingine ambazo zinaweza kupelekea hatari kwa Mama Mjamzito au Mtoto wake aliyeko tumboni.
Vile usikose kufuatilia video hii hapa chini
Response to "MTOTO HUANZA KUCHEZA LINI KATIKA TUMBO LA MJAMZITO."
Wale ambao hedhi zao haziko katika mpangilio wanaweza kushika mimba?
ndio
Nina swali naomba kuuliza nimepima mara 3 mara ya kwanza kipimo kinaonyesha ninayo Cha pili Sina Cha tatu ninayo na hedhi sijaona apo shida ni nini na Ninahisi kitu kikicheza tumboni
NAOMBA UTUME MESSAGE WHATSAPP NAMBA 0629019936
Ndioo wanaweza kushika mimba especially Mimi pia sikua na mpangilio wa siku zangu za hedhi tarehe zilikua zanabadikika Kila mwezi but now ni mjamzito
Okay hongera sana
Unaweza ukapima Kwa kipimo Cha UPT kikakwambiw kua huna mimba na ukawa nayo??
Hapana labda kama umepima mapema sana ni vema kurudia kupima baada ya wiki 1 tena
Doctor nina wiki20 lakini mtoto sisikii kucheza ?😔
Muda bado ingawa kama una wasiwasi uende hospitali ukafanyiwe vipimo
Jee kama mtoto kaanza kucheza nda ya siku mbili harafu mama anapata maumivu makali Sana ya tumbo hii imekaaje
Hali ya kawaida
Je inawezekana ultrasound ikatoa majibu tofauti kuhusu umri wa mtoto kinyume na matarajio ya mama ? Kama kweli ni kwanini?
Kweli ni kawaida inategemea na anayefanya na umri wa mimba bonyeza link hii sikiliza video https://youtu.be/ay-PE4r4Q74
Naomba unisaidie Mimi ni mjamzito wa miezi3 lakini nawashwa sana ukeni tatizo laweza kuwa Nini?
Pole sana naomba nitafute whatsApp namba +255629019936
Mimi ni mjamzito nina mimba ya wiki 14 na siku 3 nilikua natumia style ya kulala chali kwenye tendo la ndoa je naweza nikawa nimemdhuru mtoto?
Hapana Mimba inapozidi kuwa kubwa ni vema kutumia style nyingine
Mimi nina mimba ya miezi minne, na nimeanza kuhisi mtoto akicheza na ni mimba ya kwanza kwangu. Hapo juu umesema kwa mimba ya kwanza si rahisi kuhisi mtoto akicheza katika umri huo, maelezo zaidi
Ndio, japokuwa si kwa akina mama wote wako ambao wanahisi hata kabla ya Miezi 4
Sikuwa najua kama mjamzito nikapata maralia nikanywa mseto ujauzito ukiwa na wiki 2 naweza pata madhara? Ingawa mwili uko sawa na nna mwezi wa 2 sasa
Haina shida ndugu yangu
Mtoto kucheza upande mmoja katika mimba ya umri wa miezi minne kasoro sio tatizo !?
Ndio, Hakuna shida ndugu yangu
hbr nahic kua nina mimba na nina his kitu kinacheza tumbon kabisa lakin nikipima UPT inasoma Negative
Hauna Mimba
Mtoto wake wiki 9 na siku 5 snacheza tumboni NI sawa?
Hapana
Nina ujauzito wa wiki 15 n siku kadhaa,nimekuwa na changamoto ya miscarriage ,mwenz wa 5 nlipata hiyo shida,nikabeba mimba tena mwez wa 9 .natoka nimebeba mimba nimekuwa nikitumia duphstone 2×2 kwa siku mpk.sasa n vidonge vy maumivu ya tumbo hyscine 2×3.kwa kila siku.kwa kuelekezwa n doct.je na maumivu y tumbo hayakomii n niko bedrest.swali langu nikutaka kujua hivi vidonge havitaleta madhara kwa mtoto?
Asante.
Message whatsApp namba +255629019936
Nina ujauzito was miezi minne na ni wa kwanza lakin Bado sijaaanza kwenda klinik, je Kuna madhara naweza kupata?
Ndio