Uchungu usio halisi kwa Mjamzito(False labor).

Uchungu usio halisi kwa Mjamzito(False labor).

Uchungu usio halisi kwa Mjamzito(False labor).

Uchungu usiohalisi ni maumivu ya tumbo chini ya kitovu ambayo hubana na kuachia ambayo Mjamzito anaweza kupata katika kipindi cha Ujauzito.

Maumivu ya kubana na kuachia huweza kuanza miezi mitatu ya mwanazoni mwa Ujauzito,Miezi mitatu ya katikati au Miezi mitatu ya mwishoni mwa Ujauzito kitalaamu huitwa Braxton Hicks Contractions.

Maumivu haya huweza kutokea haswa miezi mitatu ya katikati na Miezi mitatu ya Mwishoni ambayo kwa jina lingine huitwa Uchungu usio halisi (False labor),Uchungu usio halisi huanza wiki 1 hadi 3 kabla ya Uchungu halisi kwa Mjamzito wa mimba ya kwanza na huanza siku chache kabla ya Uchungu halisi kwa Mjamzito wa mimba ya pili na kuendelea.

KUMBUKA: Uchungu usiohalisi endapo ukikazana au maumivu ya kubana na kuachia yakijirudia kila baada ya dakika 5 zaidi ya saa 1 huweza kuwa Uchungu halisi (True labor) na mama anaweza kujifungua kama kawaida.

SABABU ZA UCHUNGU USIOHALISI KWA MJAMZITO.

Mjamzito unaweza kupata maumivu haya ya tumbo kwa sababu kuu mbili na kuanzia sababu ya 3 na kuendelea ni vichochezi vya Uchungu usio halisi kwa Mjamzito, sababu hizo ni kama;

  1. Kushuka kwa Mtoto aliyeko tumboni kwenye Nyonga yako halisi, Mtoto wako tumboni anaposhuka kwenye nyonga yako huweza kupelekea kutanuka kwa mji wa uzazi sehemu ya chini na mlango wa uzazi hupelekea maumivu ya kubana na kuachia katika Ujauzito wako (Uchungu usiohalisi).
  2. Mji wa Uzazi na Mtoto hubana sehemu za mishipa ya fahamu katika mazingira ya Nyonga na kupelekea uchungu usiohalisi.
  3. Kutokunywa maji ya kutosha; Mjamzito usipokunywa maji ya kutosha unaweza kupata maumivu ya tumbo ya kubana na kuachia.
  4. Kulala kwa kutumia upande moja katika Ujauzito wako.
  5. Kutofanya mazoezi madogo madogo walau dakika 30 kila siku katika wiki.
  6. Kufanya tendo la ndoa huweza kuchangia pia.

SIFA ZA UCHUNGU USIO HALISI KWA MJAMZITO.

Endapo Mjamzito unapata dalili zifuatazo basi ujue una Uchungu usio halisi;

  1. Maumivu ya Tumbo ya kubana na kuachia chini ya Kitovu, Endapo Mjamzito una Uchungu usio halisi unaweza kupata maumivu ya tumbo chini ya kitovu haswa sehemu ya mbele ambayo huwa hayazunguki kwenda kiunoni na hata kama yakizunguka kiunoni huwa ni mara chache sana.
  2. Maumivu ya tumbo huwa yasiyo na mpangilio maalum hutokea na kupotea kwa muda fulani na badae huweza kuacha kabisa na kupoa.
  3. Kuto tokwa na ute wa pinki au wenye rangi nyekundu, Mjamzito utapata maumivu bila kutokwa ute ukeni kwako ambao kitalaam huitwa Show.
  4. Kuto tokwa maji ukeni, maumivu ya tumbo huwa haya ambatani na kutokwa maji ukeni au chupa kupasuka.
  5. Kutokuwepo kwa mabadiliko ya mlango wa uzazi mfano; Kufunguka kwa mlango wa mji wa uzazi.
  6. Maumivu hupungua kwa kutumia Dawa au kubalisha upande ulio lalia au kufanya mazoezi kidogo kidogo.

KUMBUKA: Uchungu usiohalisi endapo ukikazana au maumivu ya kubana na kuachia yakijirudia kila baada ya dakika 5 zaidi ya saa 1 huweza kuwa Uchungu halisi (True labor) na mama anaweza kujifungua kama kawaida.

JINSI YA KUPUNGUZA UCHUNGU USIO HALISI KTK KIPINDI CHAKO CHA UJAUZITO.

Mjamzito unapopata dalili tajwa hapo juu usiwe na wasiwasi bali ongeza umakini haswa kama kweli ni uchungu usio halisi au uchungu halisi,Uchungu usiohalisi au maumivu yake huwa haya hitaji dawa au matibabu isipokuwa tu kama maumivu hayo yataendelea kujirudia kila dakika 5 zaidi ya saa 1 utatakiwa kwenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi, jinsi ya kupunguza uchungu usiohalisi;

  1. Kunywa maji ya kutosha, ukavu wa mwili huchangia uchungu usio halisi hivyo unapokunywa maji lita 2 na nusu kila siku unapunguza uchungu usiohalisi.
  2. Muda wa kupumzika, endapo ulikuwa unafanya mazoezi madogo madogo ukaanza kuhisi maumivu hayo ni vema kupata muda wa kupumzika.
  3. Lala kwa kutumia upande mwingine,endapo maumivu yanatokea jaribu kubadilisha upande au mkao ulio kaa huweza kusaidia kupunguza maumivu.
  4. Endapo tendo la Ndoa linachangia basi ni vema kuhakikisha kuwa unapunguza ufanyaji tendo hilo katika Ujauzito wako.
  5. Maumivu haya yanaweza kupoa yenyewe japokuwa yakizidi au kujirudia rudia kila baada ya dakika 5 zaidi ya saa 1 na vema kuwahi hospitali kwa ajili ya matibabu.

MJAMZITO UKIONA DALILI HIZI NI VEMA KUWAHI HOSPITALI HARAKA.

Mjamzito pamoja na kwamba unapata dalili za Uchungu usiohalisi haijalishi umri wa mimba ni vema kwenda hospitali haraka kama utaona dalili hizi katika kipindi chako cha Ujauzito.

  1. Endapo unapata maumivu ya tumbo chini ya kitovu ya kubana na kuachia kila baada ya dakika 5 zaidi ya saa 1 na kuendelea.
  2. Kutokwa Damu ukeni hata kama ni matone.
  3. Kutokwa maji ukeni au dalili ya chupa kupasuka.
  4. Mtoto kupunguza kucheza kuliko kawaida au kutocheza kabisa.
  5. Kizunguzungu,Kuvimba miguu ghafla na maumivu ya Kichwa au kushindwa kuona vizuri(kuona mawenge)
  6. Dalili nyingine hatarishi kama homa, kuharisha sana na nk.

MAMA AFYA BOTTOM LINE: Uchungu usiohalisi endapo ukikazana au maumivu ya kubana na kuachia yakijirudia kila baada ya dakika 5 zaidi ya saa 1 huweza kuwa Uchungu halisi (True labor) na mama anaweza kujifungua kama kawaida.

Dalili za Uchungu usiohalisi

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *