Ulaji wa Bamia kwa Mjamzito

Ulaji wa Bamia kwa Mjamzito

Ulaji wa Bamia kwa Mjamzito

Wajawazito walio wengi hutamani sana kula Bamia katika kipindi cha Ujauzito, ni kweli kwamba Bamia huwa ni muhimu sana katika kipindi cha Ujauzito.

Wajawazito wengi huamini kuwa Mjamzito anapotumia Bamia huweza kusaidia kuongeza ute kwenye Mlango wa Uzazi na Ukeni na kufanya Mjamzito kuweza kujifungua haraka kwa ajili ya ule ulaini na maji maji yanayotolewayo na Bamia yenyewe.

Vile vile inasemekeana kuwa Ulaji wa Bamia husaidia kupunguza Mjamzito kuwa na choo kigumu katika kipindi cha Ujauzito na kufanya Mjamzito kupata choo laini katika kipindi cha Ujauzito.

Kuna faida kubwa sana ya matumizi ya Bamia katika kipindi cha Ujauzito haswa katika afya ya Mjamzito mwenyewe, zifuatazo ni faida za matumizi ya Bamia katika kipindi cha Ujauzito;

  1. Kupata nyuzinyuzi ambazo humsaidia Mjamzito kupata choo laini,kinachofanya Mjamzito kupata choo laini siyo maji maji au ute utokanao na Bamia bali ni nyuzi nyuzi zitokanazo na Bamia.
  2. Huongeza Madini mbalimbali kwa Mjamzito na katika kipindi chote cha Ujauzito haswa Madini chuma ambayo husaidia kuongeza Damu na kudhibiti upungufu wa Damu kwa Mjamzito.
  3. Huongeza Vitamini mfano; Vitamin B- 9 au Folic acid ambayo husaidia kupunguza uwezekano wa kujifungua Mtoto mwenye mgongo wazi au ubongo wazi na kuongeza Damu kwa Mjamzito katika kipindi chote cha Ujauzito.
  4. Huongeza Vitamini A ambayo huongeza kuona kwa Mjamzito, afya ya macho na kuongeza kinga ya Mjamzito.
  5. Huongeza Vitamini B1 na Vitamini B6 au Pyridoxine ambayo huweza kupunguza changamoto za kichefuchefu na kutapika kwa Wajawazito haswa miezi mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito.
  6. Huongeza Vitamini C,ambayo husaidia kuongeza kinga ya Mjamzito pia husaidia katika kuhamasisha ufyonzwaji wa madini chuma yatokanayo na mimea kama vile beetroot, Rozela, Mchicha au Matembele kutoka kwenye utumbo kwenda kwenye mfumo wa damu.
  7. Huongeza kinga ya Mjamzito kwa kufanya kazi kama Anti inflammatory au Antioxidant katika kipindi chote za Ujauzito.
  8. Hudhibiti sukari kwa Wajawazito wenye kisukari cha Ujauzito au Kisukari cha muda mrefu, hivyo husaidiana na Dawa za kisukari ili kudhibiti ongezeko kubwa la sukari mwilini kwa Mjamzito.
  9. Huongeza mafuta mazuri mfano; Linoleic fatty acids ambayo ni muhimu katika kuimarisha afya ya Mtoto kabla na baada ya kuzaliwa na nk

NB; Bamia hairahisishi kujifungua au kuongeza maji maji au Ute kwenye Mlango wa mji wa uzazi ili Mjamzito aweze kujifungua haraka hiyo ni imani tu wala hakuna ukweli wowote kabisa .

Bonyeza link hii sikiliza video kuhusu matumizi ya Bamia katika kipindi cha Ujauzito.

Video kuhusu ulaji wa bamia kwa Mjamzito

Response to "Ulaji wa Bamia kwa Mjamzito"

  • Asante kwa mafunzo but Nina dalili zote za mimba ila Kila nikipima napata majibu kua negative na Nina mabadiliko yote ya mwili kama mtyu mwenye mimba

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *