NGIRI YA KITOVU KWA MTOTO MCHANGA (UMBILICAL HERNIA)

NGIRI YA KITOVU KWA MTOTO MCHANGA (UMBILICAL HERNIA)

NGIRI YA KITOVU KWA MTOTO MCHANGA (UMBILICAL HERNIA)

Ngiri ya Kitovu ni uwazi usio wa kawaida kwenye Kitovu ambao huweza kuruhusu tishu au Kiungo kutoka ndani ya tumbo (Utumbo na nk) na kuingia kwa wakati fulani fulani kwa Kichanga au Mtu yoyote mwenye shida hii.

Kati ya Vichanga 100 wanaozaliwa Vichanga 15 hadi 20 huwa na Ngiri ya Kitovu wakati wa kuzaliwa, Japokuwa Ngiri ya Kitovu kwa Watoto wachanga ni hali ya kawaida.

Ngiri ya Kitovu kwa Vichanga huwa hazina shida kwa sababu tokea Mtoto Mchanga anapozaliwa mpaka kufikia umri wa miaka 4 hadi 5 huweza kupona na kufunga yenyewe bila kuhitaji upasuaji wowote.

SABABU ZA NGIRI YA KITOVU CHA MTOTO MCHANGA(UMBILICAL HERNIA)
Sababu kubwa zinazopelekea Ngiri ya Kitovu kwa Watoto wachanga hazijulikani vizuri,Isipokuwa kuna vihatarishi ambavyo huweza kuchangia Kichanga kuwa na Ngiri ya Kitovu katika umri ndogo hususani chini ya umri wa miaka 2 hadi 3 Watoto, Vihatarishi hivyo ni kama;

  1. Mtoto Mchanga aliyezaliwa kabla ya wakati (Premature baby), tafiti zinaonesha kwamba Vichanga wanaozaliwa kabla ya Wiki 37 hadi 42 wana asilimia kubwa za kuwa na Ngiri ya Kitovu kutokana na kuto kukomaa kwa Misuli ya mbele ya tumbo na kutofunga vizuri kwa Kitovu kwa Watoto hao.
  1. Mtoto Mchanga aliyezaliwa akiwa na Uzito mdogo kuliko kawaida mfano; Tafiti zinaonesha kwamba Vichanga wanaozaliwa wakiwa na Uzito wa kilo 1 hadi 1.5, kati ya Watoto wachanga hao 100 basi Watoto wachanga 84 huweza kuwa na Ngiri ya Kitovu katika umri wa Mdogo yaani chini ya miaka 2 hadi 3, Pia Vichanga wanaozaliwa wakiwa na Uzito wa kilo 2 hadi 2.5, ukiwa chukua Vichanga hao 100, Vichanga 20 huwa na Ngiri ya Kitovu hii ni kwa sababu ya Uzito Mdogo na kutofunga kwa uwazi kwenye Kitovu chao, lakini kadiri kilo zinavyoongezeka na uwezekano wa kuwa na Ngiri ya Kitovu kwa Kichanga hupungua zaidi.
  1. Hitilafu kutokana na kuchelewa kufunga kiasilia kwenye uwazi wa kuzunguuka Kitovu cha Kichanga bila kuwa na sababu maalum.
  2. Mtoto Mchanga aliyezaliwa akiwa na changamoto za Mmeng’enyo na upungufu na Tezi ya Madini joto (Hypothyroidism).
  3. Mtoto Mchanga aliyezaliwa akiwa ulemavu kutokana na changamoto za Vinasaba Mfano; Down Syndrome na nk.
  4. Mtoto Mchanga aliyezaliwa akiwa na changamoto na ulemavu wa Tishu mbalimbali zinazo unda mfumo wa mjongeo Mfano; Tishu zinazounda Misuli(Collagens) na nk.

NB: Ngiri ya Kitovu huweza kuwapata baadhi ya watu wazima endapo kuna vihatarishi kama; Ujauzito,Magonjwa ya muda mrefu ya Mfumo wa hewa (COPD),Fetma Au Kiriba tumbo, Maji mengi kujaa Tumboni na nk.

DALILI ZA NGIRI YA KITOVU KWA MTOTO MCHANGA (UMBILICAL HERNIA)
Ngiri ya Kitovu kwa Kichanga huweza kuwa na dalili tofauti tofauti inawezekana ikawa dalili za kawaida hadi kuwa na dalili hatarishi ambazo huhitaji matibabu ya dharula,
Dalili za Ngiri ya Kitovu kwa Kichanga ni kama;

  1. Uvimbe uliopo kwenye Kitovu cha Mtoto Mchanga ambao huweza kuonekana zaidi pale ambapo Mtoto Mchanga analia,Kujikamua au Kukohoa na hupotea au kurudi pale ambapo Kichanga yuko katika hali ya utulivu.
  2. Ngiri ya Kitovu ya Kichanga ya kawaida huwa inakuwa na tabia ya kuvimba wakati Mtoto Mchanga akiwa ana jikamua au kulia na nk, vile vile hurudi ndani au uvimbe hupotea pale ambapo Mtoto Mchanga yupo kwenye hali ya utulivu.
  3. Ngiri ya Kitovu kwa Kichanga iliyozuiliwa huwa ina vimba bila kurudi ndani hata kama Mtoto Mchanga yupo katika hali ya utulivu hii ni kwa sababu ya kuingia kwa tishu au Kiungo kutoka ndani ya tumbo kwenye uwazi wa eneo la Ngiri ya Kitovu uonapo dalili hii kwenye Ngiri ya Kitovu kwa Kichanga wako ni vema kumuwahisha hospitali kwa ajili ya matibabu ya dharula.
  4. Ngiri ya Kitovu kwa Kichanga iliyobanwa, wakati mwingine tishu zilizomo ndani ya tumbo huweza kuingia kwenye uwazi kwenye Ngiri na kuzuiliwa na badae kubanwa hii huweza kupelekea kubanwa kwa mishipa ya Damu na kupungua kwa usafirishwa wa Damu kwenye Tishu/Kiungo kilicho banwa na kupelekea maumivu makali kwa Kichanga na huwa ni hatari zaidi.
  5. Endapo ukiona Kichanga wako mwenye Ngiri ya Kitovu, Ngiri yake imevimba bila kurudi ndani, eneo la Kitovu limekuwa na rangi nyekundu au nyeusi, Kichanga analia saaana, kutapika au kutopata choo hizo ni dalili za hatari ni vema kuwahi hospitali kwa matibabu ya dharula.

MATIBABU YA NGIRI YA KITOVU KWA MTOTO MCHANGA (UMBILICAL HERNIA)

Matibabu ya Ngiri kwa Vichanga na Watoto chini ya miaka 2 hadi 3 hutofautiana kulingana na umri au dalili ya Ngiri kwa Kichanga mmoja au Mtoto mmoja na mwingine, Ziko namna tofauti tofauti za matibabu ya Ngiri ya Kitovu kwa Vichanga ambazo mara nyingi hutofautiana na Matibabu ya Ngiri ya Kitovu kwa Watu wazima ambazo ni kama;

  1. Ngiri ya Kitovu ya Kichanga isiyokuwa na dalili mbaya kwa Kichanga huweza kusubiriwa na kutazamiwa kwa sababu huweza kupona au kufunga yenyewe bila kuhitaji upasuaji wowote endapo Mtoto ana umri chini ya miaka 2 hadi 3.
  2. Ngiri ya Kitovu cha Mtoto Mchanga ambayo imevimba bila kurudi ndani pale ambapo Mtoto Mchanga akiwa na utulivu ambapo huweza kuambatana na dalili Mfano; Kulia sana, Kutapika,kugeuka rangi ya Ngozi kuzunguuka Kitovu kuwa nyekundu au nyeusi, kukosa choo ni vema kuwahi hospitali kwa ajili ya upasuaji wa dharula kwa sababu huwa ni hatari sana endapo kama tishu au Kiungo mfano; Utumbo umeingia kwenye uwazi ambapo kuna Ngiri.
  3. Ngiri ya Kitovu ya Kichanga ina vimba na kurudi au hata kama hakuna dalili yoyote hatari ila mpaka kufikia umri wa miaka 3 au 4 na haijafunga basi Mtoto huyo hutakiwa kufanyiwa upasuaji wa kufunga Ngiri hiyo kwa sababu uwezekano wa kufunga yenyewe ni Mdogo sana.
  4. Ngiri ya Kitovu kwa Kichanga yenye Kipenyo cha ukubwa usiozidi sentimita 0.5 huweza kupona yenyewe bila matibabu mpaka Mtoto anapofikisha Miaka 2 na endapo Kipenyo cha Ngiri ya Kitovu ni zaidi ya sentimenta 1.5 huhitaji kufanyiwa upasuaji wa kufunga kwa sababu haiwezi kufunga yenyewe kiasilia ndani ya umri wa miaka 2 ya Mtoto.

NB: Uwazi Mdogo au Tundu la Ngiri ya Kitovu ya Kichanga lenye kipenyo kidogo huwa ni mbaya hivyo huhitaji ungalizi wa Madaktari wa karibu zaidi, endapo una wasiwasi kuhusu Ngiri ya Kitovu kwa Kichanga wako ni vyema uende hospitali haraka ili Daktari amchunguze mwanao.

Video kuhusu Ngiri ya Kitovu kwa Mtoto Mchanga (Umbilical hernia)

Response to "NGIRI YA KITOVU KWA MTOTO MCHANGA (UMBILICAL HERNIA)"

  • Mimi mtowangu an umri wamiezi miwili lakini bado kitomvu chake bado hakija funga bado kinatoa majimaji naomba msaada wakitabibu

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *