Matumzi ya Chumvi Kwa Mjamzito Na Madhara Yake!

Matumzi ya Chumvi Kwa Mjamzito Na Madhara Yake!

Matumzi ya Chumvi Kwa Mjamzito Na Madhara Yake!

Chumvi ya Mezani hutengenezwa kwa madini mbalimbali japokuwa kwa kiwango kikubwa Chumvi ya meza huundwa na madini ya aina mbili Sodium(Na) na Chlorine (Cl) ambayo huwa katika mfumo wa chaji chanya {Sodium ion (Na+)} na hasi {Chloride ion(Cl-)} hivyo Chumvi ya mezani kwa 100% huitwa Sodium chloride (NaCl), japokuwa baadhi ya Chumvi za Mezani huongezwa baadhi ya Madini muhimu kwa afya ya Ujauzito mfano; Madini Joto (Iodine), Madini Chuma (iron) na nk.

Chumvi ya Meza ina umuhimu mkubwa kwa sababu huongezea Madini ya Sodiamu (Na) mwilini ambayo huhusika katika kujenga afya ya Mwanadamu na Ujauzito haswa katika kuleta msawazo wa Maji mwilini,usafirishwaji wa umeme na taarifa kwenye Mfumo wa fahamu, utengenezwaji wa Nishati ya Seli hai mbalimbali za Mwili haswa katika Seli za Misuli na nk.

Pamoja na umuhimu wa Chumvi ya mezani katika mwili wa Mwanadamu na Ujauzito, Matumizi makubwa ya Chumvi ya Meza au Matumizi ya vyakula vilivyo chakatwa zaidi na kuongezwa Chumvi vinavyo patikana kwenye Madukani,Super maket na nk, mfano; Crips na nk huweza kuleta madhara kwa Mjamzito, Chumvi huongeza Sodiamu mwili endapo sodiamu ikiwa nyingi zaidi mwili huweza kuleta athari kubwa katika kipindi cha Ujauzito.

Baadhi ya Wajawazito hupata hamu ya kula chumvi nyingi katika kipindi cha Ujauzito wao,kwa sababu ya mabadiliko makubwa ya homoni na mwili haswa mwanzoni mwa Ujauzito na kupelekea wao kupendelea kuongeza Chumvi kwenye baadhi ya vyakula mfano; Maembe yasiyo komaa, Mahindi ya kuchoma, Chips au Chips Mayai na nk.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri ya kuwa Mjamzito hutakiwa kutumia chumvi chini ya gramu 5 kwa siku, ambayo ni sawa na kiwango cha chini ya gramu 2 ya Sodiamu kwa siku, vile vile hutakiwi kutumia Chumvi chini ya kiwango cha nusu gramu (gramu 0.5) kwa siku kwa sababu huweza kuleta athari kwenye afya ya Mtoto aliyeko tumboni mwa Mjamzito na Mjamzito.

MADHARA YA MATUMIZI YA CHUMVI NYINGI AU CHACHE KWA MJAMZITO NA KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO.

Mjamzito anapotumia Chumvi zaidi ya gramu 6 au Kutumia Chumvi ya Chini ya gramu 0.5 kwa siku huweza kuleta madhara mbalimbali kwa Mjamzito,Mtoto aliyeko tumboni katika kipindi cha Ujauzito na baada ya Kujifungua,Yafuatayo ni madhara ya kutumia Chumvi zaidi ya kiwango stahiki na Chini ya kiwango stahiki katika kipindi cha Ujauzito.

MADHARA YA KUTUMIA CHUMVI NYINGI ZAIDI KWA MJAMZITO.

Endapo Mjamzito atatumia chumvi zaidi ya gramu 6 kwa siku anaweza kupata madhara mbalimbali katika kipindi cha Ujauazito wake,madhara hayo ni kama;

  1. Presha katika kipindi cha Ujauzito au Presha ya Muda mrefu katika Maisha ya mwanamke baada ya kujifungua.
  2. Kupata Kifafa cha Mimba kutokana na Presha au Shinikizo kubwa kubwa la Damu kwa Mjamzito.
  3. Kupata kiharusi au Stroke kwenye maisha baada ya badae.
  4. Magonjwa ya Moyo kwa Mjamzito kwenye maisha ya badae.
  5. Kuvimba Miguu ya Mjazmito au Mwili mzima.
  6. Figo kushindwa kufanya kazi vizuri katika kipindi cha Ujauzito au Maisha ya badae.
  7. Kupungua kwa Ukuaji wa Mtoto Tumboni mwa Mjamzito.
  8. Kujifungua Mtoto chini ya Uzito (Chini ya kilo 2.5).
  9. Kichanga kupata shida za Upumuaji endapo amezaliwa kabla ya wakati.
  10. Kujifungua Mtoto kabla ya wakati (Chini ya wiki 37).
  11. Kutumia gharama nyingi hospitali endapo Kichanga atalazwa kutokana na shida za kuto kukomaa vizuri na nk.

MADHARA YA KUTUMIA CHUMVI CHACHE KUPITA KIASI KWA MJAMZITO.

Endapo Mjamzito atatumia chumvi chini ya gramu 0.5 kwa siku anaweza kupata madhara mbalimbali katika kipindi cha Ujauzito wake, Endapo wewe ni Mjamzito una Presha kubwa au Shinikizo kubwa katika Ujauzito wako ni vema kuzungumza na Daktari wako, Kwa sababu haturuhusu Mjamzito kupunguza Chumvi katika Ujauzito wake kutokana na Presha yake ya Ujauzito ukilinganisha na Mtu Mwingine mwenye Presha ya Muda mrefu isiyo husiana na Ujauzito ambapo huweza kuleta madhara kwa sababu upungufu wa Sodiamu kutokana na kupunguza au kuto kula chumvi katika kipindi cha Ujauzito na kupata madhara kama;

  1. Mjamzito kuvimba Miguu katika kipindi cha Ujauzito.
  2. Mjamzito kuchoka kupitiliza.
  3. Huweza kupelekea Mjamzito kupata kizunguzungu au Kuanguka katika kipindi cha Ujauzito.
  4. Kupungua kwa ukuaji wa Mtoto tumboni mwa Mjamzito.
  5. Mtoto kufia Tumboni mwa Mjamzito.
  6. Mimba kuharibika Mapema kabla ya wiki 28.

KUMBUKA: Mjamzito ni Vema kula Chumvi kiasi cha wastani kisichozini gramu 6 kwa siku au usipinguze kiwango cha Chumvi ya Mezani chini ya gramu 0.5 kwa siku katika kipindi cha Ujauzito wako.

Mjamzito mwenye Magonjwa mfano; Presha ya Ujauzito ni Vema kuzungumza na Daktari wako kabla ya kupunguza kiwango cha chumvi ya Mezani katika Mlo wako wa Kila siku, si vema kuongeza Chumvi kiholela kwenye chakula pasipo kuwa na ulazima, ili kuwa na afya bora ya Ujauzito.

Tazama video hii

Video kuhusu Madhara ya Matumizi Ya chumvi nyingi au chache kwa Mjamzito.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *