Upungufu wa Damu kwa Mjamzito.

Upungufu wa Damu kwa Mjamzito.

Upungufu wa Damu kwa Mjamzito.

UPUNGUFU WA DAMU KWA MJAMZITO.

Kwa kawaida mwanamke ambayo siyo Mjamzito ila mwenye uwezo wa kushika Ujauzito inatakiwa akipimwa Protini iliyomo ndani ya Chembechembe nyekundu za Damu iitwayo Himoglobini iwe katika kiwango cha kuanzia 12g/DL mpaka 16g/dL.

Mwanamke Mjamzito anatakiwa kuwa na kiwango cha kuanzia 11g/dL kwenda juu.

Upungufu wa Damu kwa Mjamzito ni pale ambapo endapo protini iliyomo ndani ya ChembeChembe nyekundu za Damu iitwayo Himoglobini ikipimwa kuwa chini ya 11.0g/dL hii ni kulindana na Maana ya Upungufu wa Damu kutoka na  Shirika la Afya Duniani (WHO).

Upungufu wa Damu umegawanyika katika makundi makuu matatu kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambayo ni kama ifuatavyo;-

1. Kupungukiwa na kiasi kidogo ambapo Protini iitwayo Himoglobini ikipimwa  itaonesha kiwango kuanzia 9g/dL – 10.9g/dL.

2. Kupungukiwa Damu katika kiwango cha Kati ambapo Protini iitwayo Himoglobini ikipimwa  itaonesha kiwango kuanzia 7g/dL – 8.9g/dL.

3. Kupungukiwa Damu katika kiwango hatari ambapo Protini iitwayo Himoglobini ikipimwa  itaonesha kiwango chini ya 7g/dL.

MAMBO YANAYOPELEKEA UPUNGUFU WA DAMU KIPINDI CHA UJAUZITO.

1. Ujauzito au Mimba yenyewe.

2. Kuto kula Mlo wenye Madini Chuma ya kutosha.

3. Kula vyakula kwa kuambatanisha na Chai au     Kahawa kipindi cha Ujauzito.

4. Kuwa na upungufu wa Madini Chuma /Damu kabla ya kuwa Mimba.

5. Kutokwa na Damu nyingi wakati wa Hedhi kabla ya kupata Ujauzito.

6. Kutokwa na Damu kipindi cha Ujauzito.

7. Kutoweka nafasi zaidi ya Miaka miwili kutoka Mimba Moja hadi nyingine.

8. Kutapika sana katika Miezi mitatu ya Mwanzoni mwa Ujauzito.

9. Mimba ya Mapacha au zaidi ya Mtoto Mmoja.

10. Kubeba Mimba au Mimba ya kwanza kutokana na kukosa uzoefu na kutohudhuria clinic mapema.

11. Mama aliyezaa zaidi ya Mara 5.

KUMBUKA: Hapa nimezungumzia zaidi, Upungufu wa Damu katika Ujauzito kutokana na Upungufu wa Madini Chuma!
Usikose maana ijayo kuhusu dalili na Mambo yapi iliufanye kuondoka na Athari zake!

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *