Je Uke Kujamba kwa Mwanamke husababishwa na Nini? (Uke wa Mwanamke Kujamba).

Je Uke Kujamba kwa Mwanamke husababishwa na Nini? (Uke wa Mwanamke Kujamba).

Je Uke Kujamba kwa Mwanamke husababishwa na Nini? (Uke wa Mwanamke Kujamba).

Uke Kujamba ni hali ya kutoka Gesi au Upepo wenye sauti kutoka kwenye Uke wa Mwanamke ambayo huweza kutokea wakati wa kufanya Tendo la Ndoa au Ngono, Mazoezi, Kutembea na nk. Gesi hiyo inayotoka huweza kutoka kwa sauti au bila sauti na huwa haina harufu yoyote.

Uke Kujamba (Queefing) kitaalam huitwa vaginal flatulence au Vadinal wind hali hii huwakumba wanawake 70 kati ya Wanawake 100 katika kipindi chote cha maisha yao, Uke kujamba ni hali ya kawaida huweza kuwa na sauti ila huwa haina harufu yoyote, japokuwa kwa baadhi ya akina Dada hupata aibu, kujisikia vibaya wanapopata changamoto hii haswa wakati wa tendo la Ndoa au Mbele ya Kadamnasi endapo ikitokea.

SABABU ZA UKE KUJAMBA KWA BAADHI YA WANAWAKE.

Kuna sababu baadhi ambazo huweza kupelekea Uke wa Mwanamke Kujamba, Sababu hizo ni kama hizi zifuatazo;

  1. Kufanya Tendo la Ndoa au Ngono haswa Mwanamke anapokuwa katika Mkao wa Mbwa (Dog style), Mkao huu Uke wa Mwanamke hufuunguka zaidi na kufanya hewa kuingia wakati Uume unaingia kwenye Uke wa Mwanamke.
  2. Kufanya Mazoezi Magumu au Mazoezi ya kutumia nguvu sana.
  3. Kukaa Vibaya au Mikao fulani mfano; wakati wa kufanya Mazoezi ya Yoga Mwanamke anaweza kukaa mkao ambao unaweza kuongeza Presha hasi kwenye Uke wa Mwanamke na kusababisha Hewa au Upepo kuingia kwenye Uke wa Mwanamke na badae hewa hiyo kutoka haraka na kwa sauti baada ya mwanamke kuinuka au Kubadilisha Mkao.
  4. Udhaifu wa Misuli inayouunda Sakafu ya Nyonga (Pelvic Floor Dysfunction).
  5. Ukomo wa Hedhi kwa baadhi ya Wanawake wenye umri wa Miaka zaidi ya 45 au 50, kutokana na upungufu wa homoni ya Estrojeni na kufanya kuta za Uke kuwa dhaifu.
  6. Fistula huweza kusababisha Uke wa Mwanamke Kujamba ila ni mara chache sana.

VIHATARISHI VINAVYOPELEKEA UKE KUJAMBA KWA MWANAMKE.

Mojawapo ya Mambo yanayohatarisha Uke wa Mwanamke Kujamba ni kama;

  1. Ujauzito wenye Mtoto mkubwa au Kujifungua kwa njia ya kawaida.
  2. Mwanamke mwembamba sana.
  3. Mwanamke mwenye Utapia Mlo au BMI < 24 Kg/M2
  4. Mkao Mbaya wa Kuongeza Presha hasi Ukeni na Kufanya Gesi au Upepo Kujaa Ukeni.
  5. Maambukizi ya Vijidudu kwenye Uke wa Mwanamke.
  6. Upasuaji unaohusisha Misuli inayounda Sakafu ya Nyonga au kutolewa Viungo vya kwenye Nyonga mfano; Kutolewa kwa Mji wa Uzazi.

JINSI YA KUPUNGUZA UKE KUJAMBA NA MATIBABU YAKE PIA.

Ili kuweza kupunguza Uke Kujamba na Matiba ya Uke Kujamba unatakiwa kufanya Mambo yafuatayo;

  1. Fanya Mazoezi ya Kegel, ambapo unabana Misuli inayozuia Mkojo kwa sekunde 10 na kuachia kwa sekunde 10, unarudia kufanya mazoezi haya mara 10 au zaidi na utafanya hivi kwa siku mara tatu au zaidi kila siku.
  2. Epuka kufanya Mapenzi kwa Mkao wa Mbwa haswa kwa Mwanamke badala yake tumia Mkao wa Kifo cha Mende (Missionary style).
  3. Epuka kukaa mikao inayochochea gesi nyingi kuingia Ukeni kwa mwanamke.
  4. Kufanyiwa Upasuaji wa Kuimarisha Misuli inayounda Sakafu ya Nyonga na nk.

DALILI ZA HATARI

Endapo Uke unajamba na unapata dalili tajwa hapo chini ni vema kuwahi hospitali, dalili tajwa hapo chini huashiria hatari, dalili hizo ni kama;

  1. Uke Kujamba nakutoa harufu kali.
  2. Kutokwa na Kinyesi au Mkojo Ukeni.
  3. Maambukizi ya Vijidudu Ukeni.
  4. Kuporomoka kwa Viungo vya Nyonga na nk.
Uke wa Mwanamke Kujamba

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *