Jinsi ya kupunguza Mate Mdomoni kwa Mjamzito (Mate Mdomoni kwa Mjamzito).

Jinsi ya kupunguza Mate Mdomoni kwa Mjamzito (Mate Mdomoni kwa Mjamzito).

Jinsi ya kupunguza Mate Mdomoni kwa Mjamzito (Mate Mdomoni kwa Mjamzito).

Ptyalism Gravidarum ni hali ya kuwa na Mate mengi Mdomoni kwa Mama Kijacho ambapo jina lingine kitaalamu huitwa majina mengine ni kama Hypersalivation au Sialorrhea.

Mjamzito mwenye changamoto hii huweza kutengeneza Mate lita 2 au zaidi kila siku katika kipindi cha Ujauzito, Changamoto hii hutokana na mabadiliko ya kawaida ya kifiziolojia ambayo husababishwa na ongezeko la homoni mbalimbali katika kipindi cha Ujauzito mfano; Human Chorionic Gonadotropin (HCG), Estrojeni na Projesteroni katika kipindi cha Ujauzito haswa Miezi Mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito.

Mate mengi mdomoni kwa Mjamzito hutokea zaidi Miezi Mitatu ya Mwanzoni mwa Ujauzito na hali hii huondoko kabisa kwa Wajawazito wengi Mimba inapofikisha Miezi Mitatu ya katikati mwa Ujauzito lakini baadhi ya Wajawazito huendelea kuwa na Mate mengi Mdomoni katika kipindi chote cha Ujauzito wao, hata hivyo hali hii hupona kabisa ndani ya Mwezi Mmoja baada ya kujifungua.

Hali ya kuwa na Mate mengi Mdomoni kwa Mjamzito huleta kero kwa Mjamzito mwenyewe na Watu wa karibu yake, hususani anapokuwa maeneo yenye watu wengi mfano; Ofisini, kwenye Gari na nk.

VIHATARISHI VYA MJAMZITO KUWA NA MATE MENGI MDOMONI KWA MJAMZITO

Hali ya kuwa na Mate mengi Mdomoni katika kipindi cha Ujauzito huwapata baadhi ya Wajawazito lakini si Wajawazito wote hupata hali hii, Vihatarishi au Vichochezi vya hali hii ni kama ifuatavyo;

  1. Ongezeko la Homoni katika Mwili wa Mjamzito katika kipindi cha Ujauzito haswa Miezi 3 ya Mwanzoni ya Ujauzito, Ongezeko la baadhi ya homoni mfano; HCG, Ostrojeni na Projestroni ndio sababu kubwa ya kutengenezwa Mate mengi mdomoni kwa Mjamzito.
  2. Mimba ya Mapacha, baadhi ya Wajawazito wenye Mimba za Mapacha hupata hali ya kuwa na Mate mengi Mdomoni katika kipindi cha Ujauzito wao.
  3. Hali ya kutapika au Kichefuchefu mara kwa mara katika kipindi cha Ujauzito hususani Miezi 3 ya mwanzoni mwa Ujauzito huleteleza hali ya kuwa na Mate mengi Mdomoni kwa baadhi ya Wajawazito.
  4. Kuongezeka kwa kuhisi harufu kwa baadhi ya Wajawazito huambatana na hali ya kujaa Mate mengi Mdomoni kwa Mjamzito katika kipindi cha Ujauzito.
  5. Baadhi ya Wajawazito hupendelea kula vyakula visivyomeng’enywa mfano; kula Udongo au Vijiti hali hiyo huwa sambamba na hali ya kuwa na Mate mengi Mdomoni kwa Mjamzito.
  6. Matumizi ya baadhi ya Dawa mfano; Madini chuma, kwa baadhi ya Wajawazito huchochea Kichefuchefu na hali ya kuwa na Mate mengi mdomoni kwa Mjamzito.
  7. Jinsia ya Mtoto wa Kiume aliyeko Tumboni mwa Mjamzito, Baadhi ya Watu kwenye jamii husema kwamba Mjamzito yeyote anaye tema Mate mara kwa mara huwa na jinsia ya Mtoto wa Kiume tumboni mwake ingawa baadhi ya Tafiti zimethibitisha kuwa si kweli na hakuna uhalisia wa jinsia ya Mtoto aliyeko tumboni kwa kuangalia dalili za Mjamzito.

MAMBO YA KUFANYA ILI KUPUNGUZA MATE MENGI MDOMONI KWA MJAMZITO

Yafuatayo ni Mambo ambayo Mjamzito anaweza kufanya ili kupunguza Mate kujaa Mdomoni katika kipindi cha Ujauzito wake;

  1. Mjamzito Kunywa Maji mara kwa mara katika kipindi cha Ujauzito.
  2. Mjamzito tafuna au fyonza kipande cha Limao, Limao husaidia kupunguza Mate mengi mdomoni na hali ya kichefuchefu kwa baadhi ya Wajawazito.
  3. Mjamzito tafuna Bigijii au Chewing gums ambazo hazina Sukari katika kipindi cha Ujauzito huweza kusaidia kupunguza Mate Mdomoni kwa Mjamzito lakini baadhi ya Wajawazito wanapotafuna Bigijii hupelekea Mate mengi kuongezeka zaidi kuliko wasipotumia Bigijii,Endapo inatokea hivyo kwako unaweza tumia njia nyingine.
  4. Mjamzito fyonza Barafu huwezi kupunguza hali ya kuwa na Mate mengi mdomoni kwa Mjamzito katika kipindi cha Ujauzito.
  5. Mjamzito tafuna Karanga, Popcons au Clips huweza kupunguza Mate mengi Mdomoni kwa baadhi ya Wajawazito.
  6. Mjamzito epuka Harufu au Vyakula fulani mfano; Vyakula vyenye Mafuta mengi ambavyo huweza kupelekea Kichafuchefu na Kujaa Mate mengi Mdomoni katika kipindi cha Ujauzito.
  7. Mjamzito epuka Dawa ambazo hukupelekea kuwa na kichefuchefu na tumia mbadala wa baadhi ya Dawa Mfano; Madini Chuma ambayo hupelekea kuongezeka kwa Kichefuchefu na Mate mengi Mdomoni katika kipindi cha Ujauzito badala yake tumia Folic asidi ambazo hazijachanganywa na Madini chuma.
  8. Mjamzito Swaki na Safisha Meno yako mara kwa mara katika kipindi cha Ujauzito wako hususani endapo unatapika mara kwa mara hii itakusaidia pia kupunguza kuoza kwa Meno yako katika kipindi cha Ujauzito wako.
  9. Mjamzito hakikisha unapata Usingizi wa kutosha katika kipindi cha Ujauzito wako, Hata kama ni Mchana unapohisi uchovu ni vema kupumzika au kulala, kwa sababu unapolala unapunguza hali ya kuwa na Mate mengi katika kipindi cha Ujauzito wako.
  10. Mjamzito temea Mate kwenye Kopo safi lenye Mfuniko, endapo umefanya njia zote tajwa hapo juu na imeshindikana ni vema kutafuta Kopo safi lenye mfuniko na ukawa unatemea Mate humo.

KUMBUKA;

Endapo umeshindwa njia Tajwa hapo juu za kupunguza Mate mengi Mdomoni ni vema kufuata njia tajwa namba 10 au ya mwishoni hapo juu ya kutema Mate kwenye Kopo lenye Mfuniko ambalo utakuwa unatembea nalo kwenye Pochi au begi lako itakusaidia sana.

Endapo unapata hali ya Kichefuchefu mara kwa mara au kutapika ni vema kuwahi hospitali ili Daktari au Mhudumu wa Afya akufanyie vipimo na kukuandikia Dawa au kukubadilishia baadhi ya Dawa endapo unatumia na zinakusababishia Kichefuchefu katika kipindi cha Ujauzito wako.

Video ya Mjamzito kuwa na Mate mengi mdomoni katika kipindi cha Ujauzito

Response to "Jinsi ya kupunguza Mate Mdomoni kwa Mjamzito (Mate Mdomoni kwa Mjamzito)."

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *