Je! Mjamzito anaweza kutumia Kahawa(Coffee) ktk kipindi cha Ujauzito? {Matumizi ya Kahawa kwa Mjamzito}.

Je! Mjamzito anaweza kutumia Kahawa(Coffee) ktk kipindi cha Ujauzito? {Matumizi ya Kahawa kwa Mjamzito}.

Je! Mjamzito anaweza kutumia Kahawa(Coffee) ktk kipindi cha Ujauzito? {Matumizi ya Kahawa kwa Mjamzito}.

Jibu: Ndio!

Mjamzito ili uweze kutumia Kahawa ni lazima uwe mwangalifu na utumie kwa tahadhari kubwa kwa sababu Mjamzito hatakiwi kutumia zaidi 200mg za caffeine ambayo zipo ndani ya Kahawa (coffee).

Ni vema Mjamzito usitumie zaidi ya Vikombe viwili (2) vya Kahawa katika kipindi cha Ujauzito hususani Miezi Mitatu ya Mwanzoni mwa Ujauzito, hata kama Mimba yako ina Umri zaidi ya Miezi mitatu ya mwanzoni hutakiwi kuzidisha vikombe viwili vya Kahawa yaani kipindi chote cha Ujauzito.

Soma hapa
👉Kahawa (Coffee) kwa kawaida huwa ina kemikali inayoitwa caffeine, Kemikali hii huwa na Madhara kwa Mjamzito lakini pia na Mtoto aliyeko tumboni mwa Mjamzito endapo inapita kwenye Kondo la nyuma au Zalio (Placenta) na kwenda Moja kwa Moja kwa Mtoto kwenye Mji wa Uzazi.

MADHARA YA KAHAWA HUSUSANI CAFFEINE ILIYOMO KWENYE KAHAWA KWA MJAMZITO NI KAMA:

  1. Matumizi ya Kahawa zaidi ya miligramu 200 kwa siku katika kipindi cha Ujauzito au kwa Mama Mjamzito tafiti zinaonesha kwamba Caffeine inaweza kudumaza ukuaji wa Mtoto aliyeko tumboni na Mjamzito kujifungua Mtoto mwenye chini ya kilo 2.5.
  2. Matumizi ya Kahawa Mwanzoni mwa Ujauzito kushababisha kuharibika Mimba endapo Mama Mjamzito atatumia zaidi ya (Uniti 6) miligramu 200 au Vikombe 6 kwa siku hususani katika kipindi cha Miezi 3 ya mwanzoni mwa Ujauzito.
  3. Mjamzito anaweza kupoteza Maji mengi katika kipindi chake cha Ujauzito hii ni kwa sababu Caffeine iliyomo kwenye kahawa husababisha Mjamzito kukojoa sana.

👉Kwa hiyo endapo Mjamzito atatumia kuanzia uniti 6 ambayo ni sawa na vikombe sita kwa siku inaweza kuathiri ukuaji wa mtoto aliyeko tumboni mwa Mjamzito na kuharibu Mimba ingawa ni asilimia ndogo.

👉6 units ni sawa na vikombe 6 vya Kahawa ambapo kikombe kimoja kinakadiriwa kuwa kitachukua kijiko cha chai 1.6 cha kahawa ambayo ni sawa na gramu 8.3 ya kahawa na huu mchanganyiko ukijumuishwa na maji utakuwa ≈ 150mls, unakadiriwa kuwa kutakuwa na miligramu 77- 90 za caffeine.

👉Madhara hutokea endapo mama atatumia ≈ miligramu 400- 540 kwa siku moja.

Note: Hii hapa chini inaonesha makadirio ya coffee na caffeine kwenye kikombe kimoja na ujazo wake,
Kikombe kimoja cha 150mls kitachukua ≈ vijiko 1.6 vya kahawa ≈ gramu 8.3 za kahawa ≈ 77-90mg za caffeine. Lakini inategemeana na aina ya kahawa na kiwango cha caffeine katika hiyo kahawa

NB; Hakuna uhakika wa madhara au kutokuwa na madhara ya kahawa kwa mama mwenye Mimba kuanzia miezi minne kwenda juu ingawa miezi mitatu ya mwanzo huwa kuna madhara endapo mama akitumia zaidi vikombe 6 vya kahawa kwa siku!

Kumbuka hili pia
📌Pamoja na kwamba caffeine ipo kwenye kahawa lakini pia hupatikana kwenye chai,chocolate na soda(Cocacola na Pepsi)

Mama Afya Bora ushauri:

Kama hakuna ulazima kwa kutumia Kahawa katika Ujauzito wako ni bora usitumie katika kipindi chote cha Ujauzito.

Je Mjamzito anaweza kutumia Kahawa (Coffee) katika kipindi cha Ujauzito?? (Matumizi ya Kahawa kwa Mama Mjamzito na Dr.Mwanyika).

Mjamzito usitumie Kawaha zaidi ya Vikombe Viwili (2) katika kipindi cha Ujauzito, Kama hakuna Ulazima ni vema kutotumia kahawa katika kipindi cha Ujauzito wako.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *