KUINAMA KWA MJAMZITO (JE MJAMZITO ANAWEZA KUINAMA KTK KIPINDI CHA UJAUZITO)?

KUINAMA KWA MJAMZITO (JE MJAMZITO ANAWEZA KUINAMA KTK KIPINDI CHA UJAUZITO)?

KUINAMA KWA MJAMZITO (JE MJAMZITO ANAWEZA KUINAMA KTK KIPINDI CHA UJAUZITO)?

Ukweli ni kwamba Mjamzito anaweza kuina katika kipindi chote cha Ujauzito bila shida yoyote ile katika Ujauzito wake, isipokuwa tuu kuna namna nzuri ya kuinama katika kipindi cha Ujauzito.

Mjamzito anapokuwa katika Miezi Mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito,anaweza kuinama bila shida yoyote hususani anapoinama kama kawaida ambapo hukunja kiuno na shingo au kama alivyokuwa si Mjamzito.

Mjamzito anapofikia Mimba ya Miezi 4 kwenda juu mpaka Miezi 6 yaani Miezi Mitatu ya katikati mwa Ujauzito hapa hutegemeana Mjamzito mmoja na mwingine lakini pia Mimba moja na nyingine, Wako Wajawazito ambao Mimba zao hazina shida na pia huwa wepesi kwa sababu Tumbo lao ni dogo huweza kuinama vizuri bila shida yoyote hususani wanapofuata namna nzuri ya kuinama hapa maana yake Mjamzito huwa kama ana chuchumaa bila kukunja kiuno na kuweza kuinama bila shida yoyote katika kipindi cha Ujauzito hususani Miezi Mitatu ya katikati ya Ujauzito.
Kuna Baadhi ya Wajawazito miezi mitatu ya katikati mwa Ujauzito hushindwa au hupata changamoto mfano maumivu makali sana wakati wa kuinama, wajawazito hawa ni kwa Mfano:

  1. Mjamzito mwenye Mtoto mkubwa Tumboni mwake.
  2. Mjamzito mwenye Maumivu makali ya kiuno na Nyonga.
  3. Mjamzito mwenye Maji mengi Tumboni yanayo mzunguka Mtoto Tumboni mwake.
  4. Mjamzito mwenye Mimba ya Mtoto zaidi ya mmoja inawezekana ni Mapacha au Watoto 3 na nk.
  5. Mjamzito mwenye Tumbo kubwa labda kutokana na Uzito mkubwa au kitambi katika kipindi cha Ujauzito wake.

Miezi Mitatu ya mwishoni mwa Ujauzito wajawazito wengi hupata changamoto ya kuinama na wengi wao hushindwa kufanya shughuli ndogo ndogo mfano; Kuosha vyombo, kupiga Deki, Kufua nguo, kutembea tembea, Kujisaidia chooni au kipindi cha kuoga hususani katika kipindi hiki Cha Mwishoni mwa Ujauzito hii ni kwa sababu Tumbo huwa kubwa sana na pia msawazo wima wa Mwili wake hubadilika na hivyo kani uvutano ya kwenda chini ya Duniani huelemea mbele ambako Tumbo limeelekea hivyo huweza kupelekea Mjamzito kuangukia au kudondokea mbele wakati wa kuinama kufanya shughuli ndogo ndogo za maisha yake katika kipindi cha Ujauzito wake. Hivyo Mjamzito anapaswa kujua Mbinu au Namna nzuri za kuinama katika kipindi cha Ujauzito ambapo huwa tofauti na wanawake wasiyokuwa Wajawazito ili kuepuka madhara na changamoto zitokanazo na kuinama vibaya au ndivyo sivyo katika kipindi cha Ujauzito wake.

MBINU AU NAMNA MBILI KUU ZA KUINAMA KTK KIPINDI CHA UJAUZITO.
Mjamzito ni vema kuepuka kuinama vibaya katika kipindi cha Ujauzito wako yaani kuinama kama ulivyokuwa si Mjamzito ambapo una inama kwa kukunja kiuno kwenda mbele na chini au Maungio kati ya mifupa ya Nyonga na Mifupa ya mapaja ambapo vinakuwa katika nyuzi 90 au 45 vile vile kukunja shindo kwenda mbele, badala yake fanya mbinu hizi kuu mbili ambazo ni.

  1. KUWA KAMA UNA CHUCHUMAA BILA KUKUNJA KIUNO KWENYE MAUNGIO KATI YA MFUPA WA PAJA NA MFUPA WA NYONGA.
    Mbinu hii Mjamzito hapaswi kukunja Kiuno kwa kwenda mbele na chini hapa anahitaji tuu kunyoosha kiuno chake, kupanua mapaja ili kuweka nafasi ya Tumbo lake la Ujauzito na kukunja jointi za goti yote miguu yote miwili na kushuka chini kufanya jambo lake vile vile Mjamzito hapaswi kukunja shingo yake kipindi ana inama katika kipindi chote cha Ujauzito.
  2. KUTANGULIZA MGUU MMOJA MBELE KIDOGO YA MGUU MWINGINE NA KUSHUKA WIMA BILA KUKUNJA KIUNO.
    Mbinu hii haina tofauti na mbili Ile ya kwanza hapa Mjamzito anahitaji Mguu ambao huwa anatumia sana utangulie mbele kidogo ya Mguu mwingine kwa sababu watu wengi hutumia sana Mguu wa kulia kuliko wa kushoto basi Mguu wa kulia utangulie mbele kama unataka kupiga hatua hivi hapo pia unahitaji kutanua msamba ili kuweka nafasi ya tumbo halafu unashuka ukiwa wima bila kukunja Kiuno mpaka chini na kufanya shughuli ulivyokuwa unataka kufanya muda huo.

KUMBUKA: Ukiangalia katika mbinu hizi mbili Mjamzito ili kushuka chini na kuinuka anatumia zaidi misuli ya Mapaja (Hamstring Muscles) ambayo ni salama zaidi humpa stamina vile vile humkinga kuweza kudondokea mbele na kutopata maumivu ya Kiuno katika kipindi cha Ujauzito wake
ukilinganisha na mbinu ya kawaida ambayo itamlazimu Mjamzito kutumia misuli ya mbele ya Tumbo ambayo imeshavutika na kuelemewa kwa sababu ya Tumbo kubwa la Mjamzito na pia kuvutika kwa Kiuno kitu ambacho huweza kupelekea Mjamzito kuangukia mbele na kupata maumivu makali zaidi ya Kiuno.

ATHARI ZA KUINAMA NDIVYO SIVYO KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO.

  1. KUPATA KIZUNGUZUNGU KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO
    Endapo Mjamzito atatumia mbinu ya kuinama kama alivyokuwa si Mjamzito kwa kuinama kwenda mbele na kukunja shingo hii huweza kupelekea ongezeko la usafirishwaji wa Damu kwenye ubongo na pindi anapoinuka haraka huweza kupelekea kupata kizunguzungu katika kipindi cha Ujauzito wake.
  2. KUDONDOKA AU KUANGUKIA KWA MJAMZITO.
    Mjamzito hususani kipindi ambacho Tumbo limekuwa kubwa huwa kuna mabadiliko ya Kani ya uvutano wa Dunia kwa sababu ya mabadiliko ya maumbile yake hususani Tumbo lipokuwa kubwa zaidi kwa hivyo anapoinama kwa kwenda mbele huweza kuelemewa na uzito wa Tumbo hivyo huweza kupelekea Mjamzito kuangukia au kudondokea mbele katika kipindi cha Ujauzito wake, vile vile endapo Mjamzito atatumia mbinu ya kuinama kama alivyokuwa si Mjamzito kwa kuinama kwenda mbele na kukunja shingo hii huweza kupelekea ongezeko la usafirishwaji wa Damu kwenye ubongo na pindi anapoinuka haraka huweza kupelekea kupata kizunguzungu katika kipindi cha Ujauzito wake.
  3. KIUNGULIA AU TINDIKALI KURUDI KWENYE KOO LA CHAKULA KUTOKA TUMBONI.
    Mjamzito na kipindi cha Ujauzito kunakuwa na ongezeko kubwa la homoni ya Progesteroni ambayo hulegeza Mlango kati ya Koo la chakula na tumbo la chakula hivyo endapo Mjamzito atatumia mbinu ya kuinama kama alivyokuwa si Mjamzito kwa kuinama kwenda mbele na kukunja shingo hii huweza kupelekea chakula kilicho changanywa na tindikali tumboni kurudi kwenye Koo la chakula na kuchoma sehemu ya chini ya Koo la chakula na Mjamzito huanza kupata maumivu ya kuwaka Moto au kiungulia au maumivu ya kukwangua maeneo ya chembe ya Moyo au sehemu ya juu ya Tumboni.
  4. MAUMIVU MAKALI YA KIUNO KTK KIPINDI CHA UJAUZITO.
    Endapo Mjamzito atatumia mbinu ya kuinama kama alivyokuwa si Mjamzito kwa kuinama kwenda mbele na kukunja shingo hii huweza kupelekea maumivu ya kiuno katika kipindi cha Ujauzito au kuzidi kwa maumivu katika kipindi cha Ujauzito wake.
  5. MIMBA KUHARIBIKA AU KONDOO LA NYUMA KUACHIA KABLA YA WAKATI WA KUJIFUNGUA.
    Endapo Mjamzito utaanguka katika kipindi cha Ujauzito wako na kujigongesha tumbo lako vibaya huweza kupelekea kondo la nyuma kubanduka au kujiachia kutoka kwenye ukuta wa Mji wa Uzazi kabla ya kujifungua au Mimba kukomaa na kupelekea Mimba kuharibika kabla ya wakati au kukomaa.

Ni vema kuinama kwa ufasaha katika kipindi cha Ujauzito bila kukunja kiuno kwa kuelekea mbele au chini katika kipindi cha Ujauzito wako hii itakusaidia kuepuka changamoto za kuanguka au kudondoka katika kipindi cha Ujauzito wako na nk.

Sikiliza video ya Kuinama kwa Mjamzito

Response to "KUINAMA KWA MJAMZITO (JE MJAMZITO ANAWEZA KUINAMA KTK KIPINDI CHA UJAUZITO)?"

  • Habar doct ivi Ipoje.
    Uck nikiwa naenda haja ndogo pindi nanyanyuk nasikia km mifupa ivi inagongan maeneo ya kweny kibof mpk chini… Mimba ina week 35 na siku 4 je inawez kuwa nn.?

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *