FAIDA ZA KULA TENDE KWA MJAMZITO NI ZIPI?{JE KUNA FAIDA GANI ZA TENDE KWA MJAMZITO}?

FAIDA ZA KULA TENDE KWA MJAMZITO NI ZIPI?{JE KUNA FAIDA GANI ZA TENDE KWA MJAMZITO}?

FAIDA ZA KULA TENDE KWA MJAMZITO NI ZIPI?{JE KUNA FAIDA GANI ZA TENDE KWA MJAMZITO}?

Mjamzito anapotumia Tende ktk Ujauzito wake huweza kumletea faida nyingi Sana, Tende huweza kutumika kipindi chochote cha Ujauzito wako. Zifuatazo ni faida za kutumia Tende kwa Mjamzito;

  1. KUPUNGUZA MUDA WA UCHUNGU.

Mjamzito anayetumia Tende hususani mwezi mmoja kabla ya tarehe ya matarajio yaani Mimba yenye umri kati ya wiki 36 hadi 40 huweza kupunguza muda wa Uchungu na kufanya Mjamzito ajifungue mapema zaidi, hupunguza uwezekano wa kuanzishiwa uchungu (IOL) au kuongezewa uchungu (AOL) Hii ni kwa sababu tende huwa na baadhi ya mafuta (Oleic acid, Linoleic acid na Linolenic acid) ambayo huweza kubadilishwa kuwa prostaglandini ambazo huipa nguvu misuri ya mji wa uzazi na kufanya mlango wa Uzazi kufunguka mapema. Mjamzito anayetumia matunda 6 ya Tende kwa siku hususani ktk Ujauzito wenye wiki 36 hadi 40 huweza kujifungua ndani ya masaa 20 tokea uchungu uanze hii ni mapema zaidi ukilinganisha na mjamzito asiyetumia Tende ambaye huweza kujifungua masaa 29 au zaidi tokea Uchungu uanze.

  1. KUZUIA UPOTEVU WA DAMU BAADA YA KUJIFUNGUA AU MIMBA KUHARIBIKA.

Mjamzito anayetumia Tende hususani miezi mitatu ya mwishoni mwa ujauzito huweza kumsaidia mama kutopoteza Damu nyingi baada ya kujifungua au endapo Mimba iliharibika kwa bahati mbaya, Hii ni kwa sababu tende huwa na baadhi ya mafuta (Oleic acid, Linoleic acid na Linolenic acid) ambayo huweza kubadilishwa kuwa Thromboxane ambazo husaidia chembe sahani za damu ili kusababisha damu igande haraka na kuzuia upotevu wa damu baada ya kujifungua.

  1. HUONGEZA DAMU KWA MJAMZITO NA KUZUIA MGONGO WAZI KWA MJAMZITO.

Tende huwa na kiwango kidogo cha Madini chuma na Vitamini B-9 (Folic acid) ambayo husaidia Mjamzito asiwe na upungufu wa damu katika kipindi cha Ujauzito na kupunguza uwezekano wa kupata mtoto mwenye mgongo au kichwa wazi.

  1. HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA PRESHA YA UJAUZITO.

Matumizi ya Tende hupunguza Mjamzito kupata presha ya ujauzito katika kipindi cha ujauzito.

  1. HUPUNGUZA CHOO KIGUMU (FUNGA CHOO).

Matumizi ya Tende kwa mjamzito hupunguza uwezekano wa kupata choo kigumu katika ujauzito hii ni kwa sababu tende huwa na nyuzi nyuzi nyingi ambazo hupunguza uwezekano wa kupata choo kigumu katika kipindi cha Ujauzito.

  1. HUMPA NGUVU KWA MJAMZITO.

Tende huwa na kiwango kingi cha Sukari ambayo huweza kumwongezea Mjamzito nguvu katika wakati fulani katika kipindi cha Ujauzito.

HASARA ZA MATUMIZI MAKUBWA YA TENDE KATIKA UJAUZITO.

Unashauriwa kutumia Tende 60mg hadi 80mg kwa siku, si vema kiafya kutumia kiwango kingi zaidi katika kipindi cha Ujauzito kwa sababu huweza kuleta madhara kama;

  • KUONGEZEKA UZITO KUPINDUKIA KATIKA UJAUZITO WAKO.
  • KUONGEZEKA KWA HATARI YA KUPATA UGONJWA WA KISUKARI KTK KIPINDI CHA UJAUZITO.
  • KUOZA KWA MENO KAMA UNATUMIA TENDE BILA KUWA NA USAFI MZURI WA KINYWA KWA SABABU TENDE HUWA NA SUKARI NYINGI.

KUMBUKA: TUMIA TENDE KWA KIWANGO STAHIKI AMBAYO NI SAWA NA MATUNDA 6 KWA SIKU AU 60MG HADI 80MG KILA SIKU HUSUSANI MIMBA INAPOFIKISHA WIKI 36 MPAKA 40 AU MWEZI MMOJA WA MWISHONI MWA UJAUZITO WAKO.

Sikiliza video ya Faida ya Tende kwa Mjamzito na ktk kipindi cha Ujauzito.

Response to "FAIDA ZA KULA TENDE KWA MJAMZITO NI ZIPI?{JE KUNA FAIDA GANI ZA TENDE KWA MJAMZITO}?"

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *