DALILI ZA HATARI KWA MJAMZITO KTK KIPINDI CHA UJAUZITO, WAKATI WA KUJIFUNGUA NA BAADA YA KUJIFUNGUA

DALILI ZA HATARI KWA MJAMZITO KTK KIPINDI CHA UJAUZITO, WAKATI WA KUJIFUNGUA NA BAADA YA KUJIFUNGUA

DALILI ZA HATARI KWA MJAMZITO KTK KIPINDI CHA UJAUZITO, WAKATI WA KUJIFUNGUA NA BAADA YA KUJIFUNGUA

Kipindi cha Ujauzito ni kipindi ambacho unatakiwa kuwa makini zaidi kwa sababu umebeba kiumbe hai Tumboni mwako, kuna baadhi ya dalili unapozipata unatakiwa kuwa makini ili kuhakikisha wewe mwenyewe Mjamzito na Kijacho wako anakuwa salama, Dalili tajwa hapo chini ukiziona unahitaji msaada wa dharula ili kuepuka kumpoteza Kijacho wako au wewe mwenyewe kupoteza maisha yako.

Dalili hizo ni kama ifuatavyo;

  1. Kutokwa Damu Ukeni kwa Mjamzito Mimba ya Wiki 28 au zaidi inawekeza ni ;

(a). Abruptio Placenta ambapo Kondo la Nyuma libananduka au kuachia kutoka kwenye Ukuta wa Mji wa Uzazi kabla ya Kujifungua au kabla Mimba kufikia wakati wa Kujifungua huweza kupelekea Damu kutoka Ukeni kwa Mjamzito.

au

(b). Placenta Previa ambapo Kondo la Nyuma linakuwa limejishikiza sehemu ya chini karibia na Mlango wa mji wa Uzazi hupelekea kutojishikiza vizuri au sahihi hivyo hupelekea Damu kuanza kutoka Ukeni kwa Mjamzito kabla ya Mimba haijakomaa vizuri.

  1. Mimba kuharibika au kutishia kuharibika hii hutokea Mimba inapokuwa chini ya wiki 28 hapa Tanzania.
    Ambapo kuna aina mbalimbali za Mimba kuharibika (Abortion) ambazo ni kama;

(a). Threatened Abortion hii ni aina ya Abortion ambayo maana yake ni Mimba inatishia kuharibika au kutoka endapo huduma stahiki za kuzuia Mimba hiyo kuendelea mpaka kuharibika zikifanyika Mimba haiwezi kuharibika na utajifungua Mtoto wako salama.

(b). Inevitable Abortion hii ni aina ya Abortion ambayo maana yake ni Mimba hata kama bado ipo haiepukiki kuweza kuharibika kabisa, hata kama utapewa huduma stahiki za kuzuia Mimba hiyo isiharibike au kutoka.

(c). Incomplete Abortion hii ni aina ya Abortion ambayo maana yake ni Mimba imeharibika ila kuna Uchafu umebaki kwenye Mji wa Uzazi hivyo Mwanamke huhitaji kusafishwa kwa Upasuaji au Dawa inategemeana na kiwango cha uchafu uliobaki kwenye Mji wa Uzazi.

(d). Complete Abortion hii ni aina ya Abortion ambayo maana yake ni Mimba imeharibika na hakuna Uchafu uliobaki kwenye Mji wa Uzazi kwa kawaida Mwanamke hahihitaji kusafishwa mji wa Uzazi.

(e). Missed Abortion ni hii ni aina ya Abortion ambayo ni maana yake Mtoto anakuwa amefia ndani ya Mji wa Uzazi na hakuna damu inayotoka Ukeni kwa Mwanamke Mimba ikiwa chini ya wiki 28 hapa Tanzania.

(f). Septic Abortion hii ni aina ya Abortion ambayo Maana ni yake Mimba imeharibika na kuna Maambukizi kwenye mji wa Uzazi inawezekana imetokana na Uchafu uliobaki kwenye Mji wa Uzazi ambao ulivamiwa na Vijidudu ambapo Mwanamke huhitaji Matibabu ya dharula.

  1. Mimba kutunga nje ya Mji wa Uzazi (Ectopic pregnancy).
    Mimba inapokuwa imetunga nje ya Mji wa Uzazi mfano Mimba kutunga kwenye mirija ya Uzazi, Mlango wa Uzazi au Tumboni huweza kupelekea hatari ya dharula kwa Mjamzito na huhitaji msaada wa haraka sana.
  2. Presha ktk Ujauzito au Mimba (PIH au Pre eclampsia).
    Hii huweza kutokea Mimba inapofikisha wiki 20 kwenda juu ambapo Mjamzito anakuwa na Presha ya 140/90 mmHg kwenda juu na kwa baadhi huweza Pre eclampsia ambapo presha inakuwa 140/90 mmHg au zaidi ambapo huambata na Protini kwenye Mkojo ya kuanzia au zaidi ya 300mg ndani ya Masaa 24 au (+3) au dalili nyingine mfano kuumwa kichwa au kuona mawenge.
  3. Chupa kupasuka na kutokwa maji ukeni kabla ya Mimba komaa kati wiki 28 hadi wiki 36 na siku 6. (PROM au Pre PROM).
  1. Udhaifu wa Mlango wa Uzazi (Cervical incompetence).
    Baadhi ya akina Mama Wajawazito huwa na Udhaifu wa Mji wa Uzazi kutokana na sababu mbalimbali au Mlango wa Uzazi mfupi (chini ya 2.5 Sentiminta).
  1. Mtoto kupunguza kucheza kuanzia Mimba ya wiki 28 kwenda juu ( reduced fetal kicks).Mimba inapofikisha wiki 28 kwenda juu, Mtoto anatakiwa kucheza kuanzia mara 10 kwenda juu ndani ya Masaa 12 endapo Mtoto anacheza chini ya mara 10 ndani ya Masaa 12 siku mbili mfululizo huashiria changamoto na vile vile endapo Mtoto anapunguza kucheza au mtoto asipocheza kabisa ndani ya Masaa 12 baada ya Masaa 24 anaweza kufariki unatakiwa kuwa makini sana endapo Mtoto amepunguza kucheza Tumboni mwako siku mbili mfululizo wahi hospitali.
  1. Kupasuka kwa Mji wa Uzazi kabla au wakati wa Kujifungua (Ruptured Uterus).
  2. Uchungu Pingamizi wakati wa Kujifungua (OL) hii hutokea endapo Mjamzito ana Nyonga ndogo au Nyonga ya Kiume, Mtoto mkubwa kilo 4 au zaidi na Nyonga ya mama ikashindwa kupitiisha Mtoto huweza kupelekea Uchungu Pingamizi na Mjamzito hatoweza kujifungua kwa njia ya kawaida huhitaji Upasuaji wa dharula.
  3. Uchungu wa muda mrefu wakati wa Kujifungua (PL), Uchungu mkali zaidi ya Masaa 24 huweza kupelekea Mtoto kuchoka Tumboni hivyo Madaktari huweza kufanya maumivu ya Upasuaji wa dharula.
  4. Mrija kujitokeza au kutangulia wakati wa Kujifungua kabla Mtoto kuzaliwa (Cord Prolapse).
  5. Kutokwa Damu Ukeni baada ya kujifungua (PPH).
  6. Kutokwa na Uchafu wenye harufu kali Ukeni baada ya kujifungua au ndani ya siku 42 tokea kujifungua.
  7. Homa au kuchemka sana mwili ndani ya siku 42 tokea kujifungua.

KUMBUKA:
Mama Mjamzito au Mama unayenyonyesha unapoona dalili hizo wahi hospitali bila kujiuliza maswali, nenda hospitali hata kama ni usiku wa manane ili kupewa msaada na huduma za DHARULA.

Wakati wa Kujifungua Madaktari huweza kufanya huduma ya dharula mfano; Kufanyiwa upasuaji wa dharula endapo Mrija umetangulia kabla ya mtoto na umebanwa kwa sababu ni hatari kwa afya ya Mtoto wako aliyeko Tumboni mwa Mjamzito.

Sikiliza video ya Dalili Mbaya au Dalili hatarishi kwa Mjamzito.

© Dr.Mwanyika.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *