JE MTOTO ANAWEZA KUCHEZA TUMBONI MWA MJAMZITO MIMBA IKIWA CHINI YA WIKI 16 AU MIEZI MINNE?
Jambo la kustaajabisha sana kuna baadhi ya Wajawazito wanaweza kuhisi Mtoto kucheza Tumboni mwao mapema zaidi hii ni kwa sababu wahisia kali zaidi na kuhisi mtikisiko Mimba ikiwa na wiki 12 tu au chini ya wiki 16 za Ujauzito wao, ambao hii inapingana na baadhi ya maandiko ya kisayansi ambayo huthibitisha kuwa Mjamzito huhisi Mtoto kucheza kwa mtoto Tumboni mpaka mimba itakapofikisha wiki 16 na kuendelea.
Tafiti za kisayansi zinathibisha kwamba kwa kawaida mtoto anaweza kuanza kucheza Tumboni mwa Mjamzito Mimba inapofikisha wiki 16 kwenda juu.
Mjamzito ambaye mimba yake ni ya kwanza au Mjamzito ambaye hajawahi kubeba Mimba katika maisha yake huweza kuanza kuhisi Mtoto kucheza Mimba inapofikisha wiki 18 kwenda juu wengine huweza kuchelewa kidogo mpaka wiki 24 za Ujauzito.
Mjamzito ambaye amewahi kubeba Mimba labda mfano Mimba ya 2, 3, 4 au zaidi huweza kuhisi Mtoto kucheza Tumboni mwake Mimba inapofikisha wiki 16 au zaidi katika kipindi cha Ujauzito wake.
Hii ni kwa sababu ya uzoefu lakini na mabadiliko ya Mji wa Uzazi ambayo huwa tofauti na Mjamzito ambaye anabeba mimba kwa mara ya kwanza.
Ni kweli kwamba kwa baadhi ya akina Mama Wajawazito huweza kusikia mtoto kucheza Tumboni mapema zaidi kabla ya wiki 16 endapo;
- Mjamzito atakuwa na Mimba ya Mapacha au Mimba zaidi ya Mtoto mmoja hii huweza kupelekea Mjamzito kuhisi watoto au mtikisiko mapema zaidi kabla ya umri wa Mimba kufikia wiki 16 na hii ni hali ya kawaida kabisa.
- Mjamzito kusahau tarehe ya kwanza hedhi yake ya mwisho hii huweza kupelekea Mjamzito kushindwa kujua umri sahihi wa Ujauzito wake na kupelekea kupunguza umri wa Mimba na kuona kuwa mtoto ameanza kucheza mapema zaidi kabla ya wiki 16 inawezekana ni wiki 12 au wiki 13 na nk.
Habari za kustaajabisha ni kwamba kuna baadhi ya Wajawazito wanaweza kuhisi Mtoto kucheza sana Tumboni mwao Mimba inapokuwa chini ya wiki 16 yaani kuna baadhi ya Wajawazito wao husikia mtoto kucheza Mimba inapofikisha wiki 12 tu,Na Mimba zao huwa na mtoto mmoja tu yani siyo Mapacha na hawajasahau tarehe za hedhi zao za mwisho.
😄😄😄😄😄😄.
Baadhi ya akina mama wajawazito wanaosema kuwa wasikia mtoto akicheza tumboni kabla ya wiki 16 ni hawa hapa chini nimeambatanisha screenshot za sms zao.
Lakini kumbuka kwamba kuna baadhi ya Wajawazito huwa wanafanya ultrasound Mimba ikiwa na wiki 12 au wiki 13 na huweza kuona kwenye ultrasound Mtoto anacheza vizuri tuu.
Mwisho wa siku huwa wanafuatisha uchezaji wa mtoto katika kipindi cha Ujauzito kabla ya wiki 16 baada ya kuona kwenye ultrasound, kumbe si kweli wanakuja kuhisi mtoto anacheza badae kuanzia wiki 16 na kuendelea.
NB: Nakubaliana na wajawazito wachache sana ambao huweza kusikia mtoto kucheza Mimba inapofikisha wiki 14 au 15, lakini chini ya wiki 12 si kweli kuwa ni Mtoto huwa anacheza inawezekana ni:
- Mjongeo wa Utumbo katika Tumbo la Mjamzito.
- Hisia tu za Mjamzito ambazo hupelekea kufikiri kuwa ni mtoto kumbe si mtoto.
Response to "JE MTOTO ANAWEZA KUCHEZA TUMBONI MWA MJAMZITO MIMBA IKIWA CHINI YA WIKI 16 AU MIEZI MINNE?"
Dr mke wangu ana mimba ya miezi Tisa lakini ameenda kufanya kuchukua utrasound kaambiwa mimba Ina wiki 23 Ila miezi ya mwanzoni alipatwa na tatizo la kutokwa na damu wakati alipopata mimba
Mke wako anakumbuka hedhi yake ya mwisho ilianza lini kabla ya mimba kutunga?
Habari doctor mke wangu ni mimba yake ya kwanza kuanzaia wiki ya 17 mtoto alianza kucheza lakini kufika 20 ni kama ameacha je hii ni hatari kwa mama na mtoto wake
Uende hospitali kufanya vipimo
Dr ata mie hali imenipata hii mtoto kaanza kucheza mimba ya wiki 9 sjasahau tareh yang ya mwisho wa hedhi sjasahau wiki tisa alikuw anacheza upande wa kulia ilivo vika woki 12 anacheza kushoto kunasiku nilimskia kulia. Na kushoto anacheza amekaa wiki mbili ajacheza nimeanza kumskia leo wiki ya 15 anacheza ten,,,,nilifanya oltsound mimb ikiwa na wiki 13 nikaambiwa ni mmoja tu mim mimb zang zilizopita watot wanacheza miez5 hii wiki 9 ilinishangaza na kujibadil na ubavu kulia kwend kushoto
Okay sawa
Doc. Mimi nimekaa mda mrefu miaka 15 ndo nimebeba mimba ya pili. Je mtoto wangu atacheza kwa mda wa miezi minne au atachelewa kama mtoto wa kwanza???
Itategemeana ndugu una uwezekana mkubwa wa kuchelewa kumsikia
Dr Mimi mimba yangu ni kwanza lakini Kuna mda naisi maumivu yanahama hama Mara kulia kushota maumivu hayo nayapata asubui nikiwa nimelala. nikiamka kutembea nahisi maumivu kwenye kisingino, naomba msaada mimba yangu ni ya miezi mi tatu sasa
Tunaomba ufuatilie Video zetu pale youtube
Dr mke wangu ana uja uzito wa wiki 10, alishafanya ultra sound akiwa week 8 kulingana na maelezo ya Gynaecology wake…mtoto alikuwa vzr na kila kitu normal. Shida ni kwamba mke wangu anatapika mno kuna dawa wamempatia ameze but anashindwa coz anazitapika folic acid, Carofit sasa sijui tufanyeje???
Pole sana Mkuu naomba nitumie meseji kwenye whatsapp namba +255629019936