SABABU ZA KUCHOKA SANA KWA MJAMZITO KTK KIPINDI CHA UJAUZITO (KUISHIWA NGUVU KTK UJAUZITO)
KUCHOKA SANA KTK KIPINDI CHA UJAUZITO NI HALI YA KAWAIDA KABISA JAPOKUWA KUNA WAKATI UNATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI KWA KUFANYA VIPIMO AU KUMWONA DAKTARI.
Kuchoka ktk kipindi cha Ujauzito hutokea zaidi miezi mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito wako na pia hujirudia zaidi miezi mitatu ya mwishoni mwa Ujauzito wako, japokuwa kuna baadhi ya akina Mama wajawazito huweza kuchoka sana ktk kipindi cha Ujauzito miezi mitatu ya katikati mwa Ujauzito.
SABABU ZINAZOPELEKEA KUCHOKA SANA KWA MJAMZITO KTK KIPINDI CHA UJAUZITO NI KAMA;
- Ongezeko la homoni ktk Ujauzito.
Miezi mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito, Mjamzito huchoka zaidi kwa sababu ya ongezeko la homoni ya Progesteroni miezi mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito ambayo hupelekea kulegezwa kwa tishu mbalimbali za mwili kwa Mjamzito na kupelekea Mjamzito kuchoka sana. - Choo kigumu na Tumbo kujaa gesi,
Mjamzito mwenye shida ya choo kigumu hupelekea kujaa gesi kwenye utumbo wake hivyo hupelekea kupata maumivu, hali hizi zikijitokeza wakati usiku huweza kufanya Mjamzito akose Usingizi na kuwa mchovu muda wote katika kipindi cha Ujauzito. - Kukosa usingizi wa kutosha labda kwa sababu ya Tumbo kujaa gesi au kutokana na Choo kigumu ambavyo vimesababishwa na ongezeko la homoni ya Progesteroni hufanya Mjamzito kuwa mchovu katika kipindi cha Ujauzito.
- Kukojoa mara kwa mara, Ukuaji wa mji wa Uzazi miezi mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito huweza kugandamiza kibofu cha mkojo kati ya mji wa uzazi na mfupa wa kinena na kupelekea Mjamzito kukojoa mara kwa mara nyakati za usiku hii hupelekea Mjamzito kukosa usingizi wa kutosha na kuwa mchovu ktk kipindi cha Ujauzito.
- Maumivu ya Kiungulia kwa Mjamzito, kutokana na kulegezwa kwa Mlango kati ya Koo la chakula na tumbo la chakula hii hupelekea chakula kilicho changanywa na asidi kurudi kwenye Koo la chakula na kuchoma sehemu ya chini ya Koo la chakula na kupata maumivu ya kuwaka moto au kukwangua sehemu ya chini ya kifua ktk Ujauzito.
- Kutapika na kichefuchefu kutokana na ongezeko la homoni ya HCG inayopelekea kutapika na kichefuchefu, huweza kumdhoofisha Mjamzito hususani Miezi mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito.
- Mood changes/Mabadiliko ya mhemko katika kipindi cha Ujauzito huweza kupelekea Mjamzito kuwa na hasira mara kwa mara na kuwa na Msongo wa mawazo katika kipindi cha Ujauzito wake.
- Kichwa kuuma kwa Mjamzito ambapo huweza kutoka na kukosa usingizi wa kutosha au njaa kali ktk kipindi cha Ujauzito.
- Upungufu wa Presha mwilini, Ni vema kupima presha yako mara kwa mara isiwe chini ya 90mmHg/60mmHg au zaidi ya 139mmHg/89mmHg.
- Upungufu wa Sukari mwilini, Ni vema kupima Sukari mwilini mwako isiwe chini ya 4mmol/L au 70mg/dL
KUMBUKA:
Hakikisha unapata usingizi wa kutosha ktk kipindi cha Ujauzito, hata mchana ukisikia kulala au kupumzika unatakiwa kupumzika vile vile ukiona unachoka kupita kiasi ni vema kwenda hospitali na kufanyiwa vipimo, pia hakikisha unaanza kliniki mapema ili kufanyiwa vipimo mbalimbali na mgonjwa yasiyo na dalili maalumu mfano Upungufu au Ongezeko kubwa la Shinikizo la Damu (Presha) au Kisukari na upungufu wa Sukari mwilini kwa wagonjwa wanaotapika sana na hawapati chakula cha kutosha.
No comments.