JE KIPORO CHA CHAKULA MJAMZITO ANARUHUSIWA KULA KTK KIPINDI CHA UJAUZITO?
KIPORO (LEFTOVERS) ni chakula ambacho kimebaki au masalia ya chakula baada ya mtu kula chakula alicho kiandaa katika kipindi fulani inawezekana Jioni, Mchana na ahsubuhi!
Vile vile hutegemeana na aina ya chakula inawezekana kikawa Kiporo cha Wali, Ugali, Nyama, Maharage, Ndizi, Njegere na nk.
Kwa utamaduni uliozoeleka kwenye Jamii wa kula kiporo cha chakula kwa muda fulani fulani, lipokuja suala la ulaji wa viporo kwa Mjamzito hutakiwa kutumika kwa uangalifu na tahadhari kubwa ili kuepuka athari kubwa za kiafya kwa Mjamzito na Mtoto aliyeko Tumboni mwake,
Endapo kama Mjamzito atatumia kiporo bila kuchemsha kwa ufasaha au kuhifadhi ipasavyo ili kiporo kisiaambukizwe na Vijidudu au Bakteria hatarishi.
Kumekuwa na usemi mwingi mtaani na ktk jamii ya kwamba:
- Mjamzito anayekula kiporo mara kwa mara ktk kipindi cha Ujauzito, Mjamzito hujisaidia Choo kingi wakati wa Kujifungua.
- Mjamzito anayekula kiporo anapokaribia kujifungua au miezi mitatu ya mwishoni mwa Ujauzito huweza hujisaidia Choo kingi kipindi cha kujifungua Mtoto wake.
Ukweli ni kwamba Mjamzito unaweza kula au kutumia kiporo kama watu wengine ktk kipindi cha Ujauzito, endapo tu utazingatia Mambo nitakayo zungumzia hapa.
MJAMZITO UNAWEZA KULA KIPORO CHENYE SIFA ZIFUATAZO:
Mjamzito anaweza kula kiporo ktk Ujauzito wake endapo tuu Kiporo kitakuwa na vigeo vifuatavyo;
- Kiporo ambacho kimehifadhiwa kwenye friji nyuzi Joto 4 kwenda chini kwa muda usiozidi siku 2 hadi 4 tu.
- Kiporo kilichochemshwa vizuri kwa joto zaidi ya centigrade 74.
- Kiporo ambacho kitachemshwa mara moja tu na siyo mara mbili au zaidi.
- Hata kama kiporo hakija hifadhiwa kwenye friji basi kiwe kimefunikwa au kuwekwa kwenye chombo kisafi na kufunikwa vizuri.
- Kiporo kihifadhiwe kwenye friji lisilo na vitu vingi sana ili ubaridi uweze kuzunguuka kwenye kiporo chote kuepusha maambukizi ya Vijidudu hatari ambao wanaweza kuleta athari kwa Mjamzito na Mtoto aliyeko Tumboni.
- Usitumie kiporo kilichochemshwa zaidi ya Mara moja na zaidi.
MJAMZITO USILE KIPORO (LEFTOVERS) KTK KIPINDI CHA UJAUZITO CHENYE SIFA HIZI:
- Kiporo kisicho hifadhiwa katika mazingira safi na salama.
- Kiporo kisichofunikwa au kuto chemshwa zaidi ya jotoridi la nyuzi 74 centigredi zaidi ili kuua Vijidudu hatari kwa afya mtoto aliyeko tumboni mwa Mjamzito
- Kiporo kilichokuwa zaidi ya siku 4 hata kama kilikuwa kwenye friji chini ya jotoridi la chini nyuzi centigredi 74, kwa sababu huweza kuwa na Maambukizi ya Vijidudu hatari kwa Mtoto aliyeko Tumboni mwa Mjamzito.
- Kiporo kinachochemshwa zaidi ya Mara mbili au kurudia rudia kuchemsha.
- Kama huwa unapata athari mfano; kuharisha, Tumbo kuuma endapo ukila kiporo haina haja ya kula ni vema kuepuka kabisa.
Mjamzito usile kiporo ambacho kimehifadhiwa mazingira yasiyo salama ili kuepuka kula chakula chenye Maambukizi ya vijidudu, mfano; Listeria monocytogenes ambaye huweza kumathiri Mtoto aliyeko tumboni mwa Mjamzito.
KUMBUKA: Mjamzito anaweza kula kiporo endapo kimehifadhiwa katika mazingira safi na salama bila athari zozote kiafya.
Mjamzito unashauriwa kula chakula laini unapokaribia kujifungua mfano; Uji, Mtori, Chai na nk, ili kuepuka kupata haja kubwa nyingi sana wakati wa Kujifungua na kuleta kero kwa wanaokusaidia kujifungua.
No comments.