JE CHOO CHEUSI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO HUSABABISHWA NA NINI?
Kwa kawaida rangi ya Choo cha Mwanadamu huwa na rangi ya kahaiwa (Brown), lakini baadhi ya sababu huweza kupelekea Mjamzito kupata Choo cheusi katika kipindi cha Ujauzito, Choo cheusi kwa Mjamzito huweza kuashiria magonjwa mbalimbali ya mfumo wa chakula au hali ya mabadiliko ya kifiziolojia ya kawaida.
MAMBO YANAYOPELEKEA CHOO CHEUSI KWA MJAMZITO
1. Matumizi ya Dawa za kuongeza Damu (Madini Chuma) katika cha Ujauzito.
Mjamzito anapotumia Madini Chuma yanaweza yasifyonzwe vizuri kwenye mfumo wa chakula yanapotoka kwenye choo huweza kupelekea Mjamzito kupata Choo cheusi.
2. Matumizi ya Dawa za kupunguza maumivu ya kiungulia.
Matumizi ya Dawa za kupunguza kiungulia mfano; Aluminium hydroxide au Magnesium hydroxide huweza kupelekea Mjamzito kupata Choo cheusi katika kipindi cha Ujauzito.
3. Matumizi ya baadhi ya vyakula mfano blueberries, Chocolate na Vyakula vingine ambazo vimeongezwa rangi huweza kupelekea Mjamzito kupata Choo cheusi katika kipindi cha Ujauzito.
4. Magonjwa ya mfumo wa chakula, Mjamzito mwenye ugonjwa wa vidonda vya tumbo kwa muda mrefu bila kutibiwa, vidonda huweza kutoka Damu ambayo huweza kupelekea Mjamzito kupata Choo cheusi katika kipindi chochote cha Ujauzito.
5. Kutokwa Damu sehemu ya juu ya mfumo wa chakula (Upper GI bleeding), Mjamzito ambaye amepasuka sehemu ya chini ya Koo la chakula kutoka na kutapika Sana huweza kupata Choo cheusi katika kipindi cha Ujauzito.
No comments.