SABABU ZA KUJIFUNGUA KABLA WAKATI NA MAMBO AMBAYO HUPELEKEA KUJIFUNGUA KABLA YA WIKI 37 NA MTOTO KUWEZA KUFARARIKI.
Dalili za uchungu za mwanzoni,Kujifungua kabla ya wakati,Kujifungua kabla ya wiki 37,Kujifungua mapema,Maumivu ya Tumbo kwa Mjamzito,Uchungu kabla ya wiki 37,Uchungu Mjamzito,Uchungu wa haraka,Uchungu wa kabla ya siku,Uchungu wa mapema,Uchungu wa mwanzoni,Uchungu wa uongo
2 Comments
SABABU KUBWA YA MJAMZITO KUJIFUNGUA KABLA YA MTOTO KUKOMAA AU CHINI YA WIKI 37 HAZIJULIKANI.
YAFUATAYO NI MAMBO HATARISHI YANAYOWEZA KUFANYA UJIFUNGUE KABLA YA WAKATI.
- Historia ya kujifungua mapema, Kama Mimba yako iliyopita ulijifungua kabla ya wiki 37 basi kunauwezekano mkubwa wa inayofuata kujifungua pia.
- UTI Mara kwa Mara, Mjamzito U anayeumwa UTI mara kwa mara inaweza kupelekea chupa kupasuka kabla ya Mimba kukomaa na kufanya ujifungue kabla ya wakati.
- Presha ya Mimba, Mjamzito anayepata presha ya ujauzito huweza kupelekea kutakiwa kujifungua mapema endapo presha yake haitadhibitiwi na dawa za presha ili kuepuka kifafa cha Mimba na kuweza kusababisha kifo kwa mama au Mtoto pia.
- Kutokwa na Damu ktk Ujauzito, Endapo Mjamzito unatokwa na Damu, hii inawezekana Mimba inatishia kutoka au kuharibika endapo Mimba yako ina umri wa chini ya wiki 28 na kama Mimba ina wiki 28 kwenda juu kabla ya wiki 37 na Damu zinatoka labda kwa sababu ya kujishikiza kwa Kondo la Nyuma karibia na Mlango wa Uzazi (Pracentae Previa) au ulipatwa Ajari (Abraptio Placenta) basi utatakiwa kujifungua kabla ya wakati kuepuka upotevu wa damu.
- Msongo wa mawazo/Stress huweza kupelekea Mjamzito kupata Uchungu wa mapema.
- Uvutaji sigara, umasikini au Mjamzito mwenye uzito chini ya BMI ya 18kg/M² huweza kujifungua kabla ya wakati.
- Maji mengi kwenye Tumbo la Mjamzito ambayo humzunguuka mtoto huweza kuchochea kupata Uchungu wa mapema kabla ya wiki 37.
- Uzaifu wa Mlango wa Uzazi au Ulemavu wa Mji wa Uzazi, Mjamzito mwenye shida ya kuharibikiwa mara kwa mara na Mimba miezi mitatu ya katikati yaani miezi 4, 5 na 6 ya Mimba na akajifungua ghafla Mtoto hai baada ya muda akafariki kwa sababu ya kushindwa kupumua au Mjamzito kujifungua wiki ya 28 Mimba mbili au tatu hii huonesha kuwa Mjamzito huyo ana shida ya Udhaifu wa Mlango wa Uzazi.
- Kuchemka sana kwa Mjamzito au Homa kali hii huweza kupelekea udhaifu wa kuta zinazounda chupa ya Mtoto Tumboni mwa Mjamzito na kupelekea kupasuka kwa chupa mapema na kunzishwa kwa Uchungu kabla ya wakati.
- Kuharisha sana ktk Ujauzito.
- Kisukari cha Ujauzito/Mimba.
Ugonjwa wa Kisukari au Mjamzito mwenye Kisukari huweza kuwa na maji mengi yanayomzunguka Mtoto Tumboni mwake kwa sababu Mtoto hukojoa sana na hali hiyo hupelekea kuweza kuanza kwa uchungu mapema kabla ya wakati. - Ugonjwa wa Pumu ktk Ujauzito, endapo Mjamzito mwenye Pumu atapata changamoto itakayo mfanya Mjamzito kushindwa au kuathiri afya yake kwa sababu Ugonjwa wa Pumu na pia ni Mjamzito hutakiwa kujifungua mapema.
- Magonjwa ya Moyo ktk Ujauzito,endapo Mjamzito atabanwa au kushindwa kupumua kutokana na Ugonjwa wa Moyo usio dhibitiwa na Dawa na kuathiri afya ya Mjamzito basi atatakiwa kujifungua mapema.
- Upungufu mkubwa wa Damu, Mjamzito mwenye Damu chini ya 5 g/dL wakati mwingine hutakiwa kujifungua mapema zaidi.
- Magonjwa ktk Njia za Uzazi, Maambukizi ya Vijidudu katika via vya Uzazi huweza kupelekea chupa kupasuka kabla ya wakati na uchungu kuanza mapema.
- Mimba ya Mapacha Mjamzito mwenye Mapacha huweza kujifungua kabla ya Wiki 37 na watoto wakapona vizuri kabisa na ni kawaida.
- Hitilafu ya Kondo la Nyuma, kutokwa Damu Mimba ya kati ya wiki 28 na 37 kutokana na hitilafu ya kujishikiza karibua na Mlango wa Uzazi au Kondo kujiachia kabla ya muda kwa Mjamzito wakati mwingine hutakiwa kujifungua kabla ya wakati.
- Historia ya kuharibu au kuharibika kwa Mimba, Mjamzito mwenye historia ya kuharibu au kuharibikiwa Mimba na kusafishwa mara kwa mara huweza kupelekea udhaifu wa mlango wa Uzazi na kujifungua kabla ya wakati.
- Mshono kuuma, Mjamzito mwenye mimba na Mimba ya nyuma alijifungua kwa upasuaji na anapata maumivu ya Tumbo makali hutakiwa kujifungua mapema ili kuepuka Mji wa Uzazi kupasuka kutokana na uchungu.
KUMBUKA: Uonapo vihatarishi hivyo unatakiwa kuwahi hospitali mapema kwa ajili ya uangalizi au ushauri wa Daktari wako
©Dr.Mwanyika
Response to "SABABU ZA KUJIFUNGUA KABLA WAKATI NA MAMBO AMBAYO HUPELEKEA KUJIFUNGUA KABLA YA WIKI 37 NA MTOTO KUWEZA KUFARARIKI."
Elimu muhimu sana hii,
Ni kweli kabisa