KUTOKWA MAZIWA KTK KIPINDI CHA UJAUZITO!
Kutokwa na Maziwa au Maji maji kwenye matiti ktk kipindi cha Ujauzito.
Wajawazito wengi huwa wanapata hali ya kutokwa Maziwa au Maji maji ktk kipindi cha Ujauzito na kabla ya kujifungua hali hiyo ni kawaida kabisa hutakiwi kuwa na wasiwasi.
Hali ya kutokwa Maziwa au Maji maji ktk Ujauzito hutokana na ongezeko la homoni ya prolactin ktk kipindi cha Ujauzito na hali hii huweza kuanza mwishoni mwa miezi mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito au Miezi mitatu ya katikati mwa Ujauzito na kuendelea.
Ni kweli kwamba tishu za kwenye Matiti huwa hazisisimki hata kama homoni ya prolactin ipo katika kiasi kikubwa kwa Mjamzito ndio maana wajawazito wengi huwa hawatokwi na maziwa kabla ya mwishoni mwa Miezi Mitatu ya Mwishoni mwa Ujauzito hii ni kwa sababu ya uwingi wa homoni za Progesteroni na Estrogeni katika kipindi cha Ujauzito lakini baada ya Mjamzito kujifungua homoni hizo hushuka haraka na kupelekea tishu za matiti kuanza kusisimka kutokana na homoni ya prolactin na Oxytocin hivyo hupelekea Mama aliyejifungua kuanza kutoa maziwa ndani ya muda mfupi baada ya kujifungua.
Endapo unatokwa Maziwa au Maji maji ktk Ujauzito wako basi unatakiwa kufanya Mambo yafuatayo:
- Usijikamue au kushika shika Maziwa au Matiti au Chuchu za Matiti yako.
- Usivae Brazia au Nguo zinazobana mwili sana katika kipindi cha Ujauzito wako.
- Endapo unatokwa Maziwa mwambie mpenzi wako asiweze kukusisimua kwenye Maziwa au Matiti yako katika kipindi cha kushiriki tendo la Ndoa.
- Tafuta Brazia za wajawazito na pia vaa nguo zisizogusa gusa chuchu za Matiti yako.
Endapo Maziwa yanatoka mengi zaidi unatakiwa kuvaa Brazia za akina Mama wanaonyonyesha.
Endapo Maziwa yanatoka mengi au Unatokwa na Maziwa yaliyo jichanganya na Damu basi ni vema kumwona Daktari.
Response to "KUTOKWA MAZIWA KTK KIPINDI CHA UJAUZITO!"
Asante
Docta nmefany mapenz wiki sasa imepita lakn ckua ktk cku hatarsh lakn nashangaa nkibinya matiti maziwa yanatoka
Usibinye ndugu yangu
Matiti nikibonyeza yanatoa maji na vijimaziwa. Inaweza kuwa ni dalili ya mimba Dr.?
Siyo mara zote cha msingi pima mimba kama una wasiwasi?
Dactari habari ya Leo?
Karibu
Dr natokwa na majimaji mwenye matiti ila Yana rangi Shida nn Dr?
Huwa unakamua kwenye Matiti
Habari dokta, natokwa na maji maji yasiyo na ladha wala harufu kwenye titi langu la kushoto na nimepima sina mimba, shida ni nini?
Unafanya kujikamua si ndio?
Ndio. Kuna mda yanakua kama yana kichomi ndio nkibinya maji yanatoka, na nimegundua ni yote mawili
Ndio. Kuna mda yanakua kama yana kichomi, nimegundua ni yote mawili yanaleak