JE MJAMZITO ANAWEZA KUNYWA MAZIWA AU MTINDI?

JE MJAMZITO ANAWEZA KUNYWA MAZIWA AU MTINDI?

Jibu:

Ndio, Mjamzito anaweza kutumia Maziwa au Zao lolote litokanalo na Maziwa bila shida yoyote kwa Mjamzito.

Isipokuwa tuu Mjamzito haruhusiwi kunywa Maziwa au Zao lolote lililotokana na Maziwa ambayo hayaja chemshwa ipasavyo hii ni kwa sababu endapo Maziwa hayakuchemshwa vema huweza kuwa na Bakteria hatari ambao huweza kusababisha Mimba kuharibika, Maambukizi kwa Mtoto na Kujifungua kabla ya wakati kama Mjamzito atatumia maziwa hayo na akapata Maambukizi ya Bakteria hao.

MUDA SAHIHI WA KUNYWA MAZIWA NI UPI?.
Ni vema kunywa Maziwa kipindi cha ahsubuhi kabla ya kula chakula chochote au masaa fulani baada ya kula chakula chako.

Muadhi madogo madogo kwa Baadhi ya Wajawazito ni kama:

  1. Kupata maumivu ya Tumbo kutokana na kujaa gesi Tumboni.
  2. Kujamba au kupumua kwa njia ya haja kubwa

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *