UBUYU KWA MJAMZITO (BAOBAB FRUIT IN PREGNANCY)

UBUYU KWA MJAMZITO (BAOBAB FRUIT IN PREGNANCY)

UBUYU KWA MJAMZITO (BAOBAB FRUIT IN PREGNANCY)

FAIDA ZA UBUYU KWA MJAMZITO NI ZIPI?
UBUYU(BAOBAB FRUIT) ni Tunda litakanalo na mti uitwao Mbuyu kisayansi unaitwa Adansonia digitata. Jamii ya Miti hii hupatikana ukanda wa Savanna!

Africa Mti huu baadhi ya Makabila huita Mti wa Uzima hii ni kwa sababu Mti huu hutoa Malazi kwa baadhi ya Watu, Matunda yake ni Chakula, Mavazi yaani Magome ya Mti huu, Maji na vile vile hutumika kama Dawa kwa baadhi ya Mgonjwa na baadhi ya sehemu walikuwa wanatumia kutambikia na nk.

Mti huu umewafanya Baadhi ya watu kuwa na Matajiri kwa sababu Matunda yake huweza kutengeneza Unga wa Ubuyu na Mazao mbalimbali ambayo hutumika kutengeneza Vyakula mbalimbali ambavyo hutumika na Binadamu na huuzwa kwa bei ghari.

JE MJAMZITO ANAWEZA KUTUMIA UBUYU?
JIBU NI NDIO!
Ukweli ni kwamba Ubuyu huwa na Vitamini na Madini mbalimbali ambayo ni muhimu katika Afya ya Mwanadamu hususani kwa Wajawazito.
Vitu gani hufanya Ubuyu kuwa na umuhimu kwa Mjamzito?

  1. VITAMINI C ( ASCORBIC ACID).
    Ubuyu huwa na kiwango kingi cha Vitamini C,yaani mara 6 zaidi Vitamini C inayopatikana kwenye Matunda mfano; Machungwa.
    Vitamini C ni muhimu sana kwa Mjamzito ili kuhakikisha kuwa Mtoto anakuwa katika afya, vilevile huimarisha nyuzi nyuzi ziitwazo Collagen ambazo hutumika kutengeneza tishu mbalimbali Mwilini ikiwemo kuta zinazozunguka Mtoto Tumboni mwa Mjamzito.

Vitamini C ni muhimu kwa Mjamzito kwa sababu hutumika kuhamasisha ufyonzwaji wa Madini chuma kutoka kwenye Utumbo kwenda kwenye Damu, huwa ni muhimu katika ufyonzwaji wa Madini Chuma yatokanayo na Mimea (Non Heme Iron) ambayo ufyonzwaji wake huwa duni endapo kama Mjamzito atakuwa na upungufu wa Vitamini C.

  1. VITAMINI B-9 (FOLATE)
    Folate huwa na umuhimu kwa Mjamzito kwa sababu hutumika kutengeneza Vinasaba vinavyotumia kutengeneza Seli hai Nyekundu za Damu na kuzuia kujifungua Mtoto mwenye Mgongo au Kichwa wazi, hivyo unapotumia Ubuyu huweza kukuongezea kiasi fulani cha Vitamini B-9 au Folate.
  2. MADINI YA CALCIUM.
    Mjamzito ni muhimu kupata Calcium ya kutosha ili kuhakikisha kuwa na Afya ya Mifupa yako Mjamzito na Mtoto pia , Unapotumia Ubuyu huongeza kiasi fulani cha Madini ya Calcium katika Ujauzito wako.
  3. NYUZI NYUZI (INSOLUBLE FIBRES)
    Unapokuwa Mjamzito ni rahisi kuwa na Choo kigumu (Constipation) hii ni kutokana na mabadiliko ya homoni katika kipindi cha Ujauzito hususani ongezeko la Homoni ya Progesteroni ambayo hupunguza mjongeo wa Utumbo na kupelekea kuwa na dalili za choo kigumu ambazo huweza kupelekea Mjamzito kupata Bawasiri katika kipindi cha Ujauzito, Unapotumia Ubuyu huweza kupunguza dalili za choo kigumu kwa sababu huwa na nyuzi nyuzi ambazo husaidia kulainisha choo kwenye Utumbo na kupunguza choo kigumu.
  4. KUTAPIKA AU KICHEFU CHEFU.
    Baadhi ya Wajawazito huwa na Dalili za kutapika au kuwa na kichefu chefu zaidi, hali hii huweza kupungua endapo Mjamzito anatumia Ubuyu kwa sababu Ubuyu huwa na kiwango kingi cha Vitamini C ambayo hupunguza hali ya kichefuchefu kwa Mjamzito.
  5. MADINI CHUMA.
    Kuna umuhimu mkubwa wa madini Chuma kwa Mjamzito hivyo unapotumia Ubuyu au Unga wa Ubuyu huweza kukuongezea kiasi fulani cha Madini Chuma katika Ujauzito wako.

KUMBUKA:
Pamoja na kwamba Ubuyu una faida nyingi kiafya lakini Mbegu za Ubuyu huwa na Kemikali (Tanins,Phytates na Oxalate) ambazo huzuia ufyonzwaji wa baadhi ya Madini kutokana kwenye Utumbo kwenda kwenye Damu mfano; Madini Chuma.
Hivyo Tumia Ubuyu kwa Kiasi tu.!

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *