KUTOKWA NA UCHAFU WENYE HARUFU MBAYA UKENI | SHOMBO YA SAMAKI KWA MJAMZITO NA KIPINDI CHA UJAUZITO!

KUTOKWA NA UCHAFU WENYE HARUFU MBAYA UKENI | SHOMBO YA SAMAKI KWA MJAMZITO NA KIPINDI CHA UJAUZITO!

KUTOKWA NA UCHAFU WENYE HARUFU MBAYA UKENI | SHOMBO YA SAMAKI KWA MJAMZITO NA KIPINDI CHA UJAUZITO!

KUTOKWA NA UCHAFU WA NJANO UKENI KWA MJAMZITO NI UGONJWA AMBAO HUSABABISHWA NA BAKTERIA.

UGONJWA HUU HUITWA BACTERIAL VAGINOSIS.
Bacterial Vaginosis husababisha na Bakteria aina ya Garnerella Vaginalis ambaye huvamia Ukeni kwa Mjamzito endapo kutakuwa na mabadiliko ya kifiziolojia ambapo Tindikali iliyopo Ukeni hupungua na Kusababisha Bakteria huyu kuishi na kuzaliana katika uke wa Mwanamke au Mjamzito.

Dalili za Ugonjwa huu ni kama;

  1. Kutokwa na Uchafu wa Njano au Kijani Ukeni.
  2. Kutokwa na Uchafu wenye harufu ya Mbaya au Shombo ya Samaki.
  3. Kutokwa na Uchafu wenye harufu Mara baada ya Tendo la Ndoa au Ngono.
  4. Kupata Muwasho kwenye Mashavu ya Uke.
  5. Kupata Maumivu wakati wa kukojoa au kufanya Tendo la Ndoa.

VIHATARISHI VYA UGONJWA HUU NI KAMA;

  1. Kuingiza Vidole Ukeni (Douching).
  2. Kuvuta Sigara.
  3. Matumizi ya Dawa za kuua Bakteria wa aina nyingi (Broad Spectrum Antibiotics).
  4. Kuwa na wapenzi wengi.

MATIBABU.
Endapo ukiwa na Ugonjwa huu unahitaji Matibabu ya haraka ili kuepuka athari za Maambukizi kwenye Mji wa Uzazi na Kuta zinazo mzunguka Mtoto wako katika Mji wa Uzazi na kupelekea Udhaifu wa Kuta hizo na kupasuka kwa Chupa kabla ya wakati.

Endapo Chupa imepasuka Mimba yenye umri chini ya wiki 28 huweza kupelekea Kifo kwa Mtoto wako endapo atazaliwa kabla ya wakati kipindi ambacho Mapafu hayaja komaa vizuri.

Endapo utahitaji Matibabu ya Ugonjwa huu wasiliana nami WhatsApp kwa namba 0629019936 au unaweza kwenda hospital ukutane na Daktari na akuandikie Dawa stahiki.

NB: Epuka kununua Dawa kiholela kwenye Maduka ya Madawa baridi ya Binadamu bila idhini ya Daktari.

Bacterial Vaginosis husababisha na Bakteria aina ya Garnerella Vaginalis

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *