Dalili za Mwanzoni za Kujifungua au Uchungu kwa Mjamzito.

Dalili za Mwanzoni za Kujifungua au Uchungu kwa Mjamzito.

Dalili za Mwanzoni za Kujifungua au Uchungu kwa Mjamzito.

Endapo umefikisha Miezi Mitatu ya Mwishoni mwa Ujauzito yaani Wiki 28 Hadi Wiki 36, kipindi ambacho bado Mtoto hajakomaa vizuri na Uchungu Halisia kuanza Baadhi ya Wajawazito hupata Dalili mbalimbali za Mwanzoni za Kujifungua au Uchungu, Wengi wao hudhani kuwa ni Uchungu wa kweli kumbe ni viashiria vya Uchungu ambao utakuja kutokea mbeleni Baada ya Muda fulani.

Dalili za Mwanzoni za Kujifungua huweza kujitokeza Miezi Mitatu ya Mwishoni mwa Ujauzito na hutofautiana kati ya Mama mmoja na mwingine vile vile na Endapo ni Mimba ya kwanza au Mimba zinazofuatia.

Bonyeza hapa jifunze kuhusu dalili za Uchungu usiohalisi

Mwanamke ambaye Ujauzito wake wa Kwanza Mara nyingi wao huanza kuhisi Dalili za Kujifungua mapema zaidi inawezekana Wiki 2 hadi 4 kabla ya Dalili za Uchungu Halisia kutokea hii huwa tofauti na Mwanamke ambaye anabeba Mimba ya Pili, Ya Tatu na Nk ambapo Hawa huweza kupata Dalili hizi siku kadhaa kabla ya Uchungu halisia au Dalili za Uchungu Halisia kutokea na Kujifungua rasmi Watoto wao.

Kwa Kawaida Uchungu Halisia au Uchungu wa Kweli hutokea Kati ya Wiki 37 hadi 42 kipindi ambacho Mtoto anakuwa amekomaa vizuri na anaweza Kuishi Duniani.

Zifuatazo ni Dalili za Mwanzoni za Kujifungua au Dalili za Mwanzoni za Uchungu.

1. Maumivu ya Mgongo na Kiuno Wakati fulani.
Wajawazito wengi hupata Maumivu haya kutokana na Ongezeko la Homoni ya Relaxin ambayo hulegeza Nyonga kwa ajili ya kuhakikisha kuwa Mtoto anaweza kupita kwenye Nyonga, wakati Mwingine hii Homoni huweza kuathiri Jointi na Ligamenti za Mwili mzima na Mjamzito hupata Maumivu Jointi nyingine za Mwili wake.

2. Mtoto Kushuka (Lightening).
Kuanzia Wiki ya 32 Mara nyingi Mtoto hushuka kwenda kwenye Nyonga tayari kwa ajili ya Kuzaliwa na Kutoka Duniani.

3. Kukojoa Mara kwa Mara.
Baada ya Mtoto Kushuka Mjamzito huanza kupata Dalili za Kukojoa Mara kwa Mara, Ni kwa sababu Kibofu Cha Mkojo hugandamizwa na sehemu ya Mtoto ambayo iko Chini kwenye Nyonga ya Mjamzito na kubanwa kwa Kibofu Kati ya sehemu hiyo ya Mtoto na Mfupa wa Kinena.

4. Kuchoka Mara kwa Mara na Kukosa Usingizi.
Maumivu katika kipindi cha Mwishoni mwa Ujauzito na Kukojoa Mara kwa Mara hii hupelekea Mjamzito kukosa Usingizi wa kutosha hivyo Muda mwingi huwa na Uchovu wa Mara kwa Mara.

5. Uzito kutoongezeka.
Kwa kawaida Mjamzito huongezeka Uzito wa Wastani wa 1kg katika kila Mwezi mmoja katika Kipindi cha Ujauzito lakini inapofika Mwishoni mwa Ujauzito Uzito huwa hauongezeki na wakati mwingine inawezekana kabisa Uzito hupungua ndio maana ni vema inapofikisha Wiki 42 ujifungue na hutakiwi kuzidisha Wiki 43 za Ujauzito.

6. Kuharisha.
Baadhi ya Wajawazito hupata Dalili ya Kuharisha hii ni Kutokana na Ongezeko la Homoni za Prostaglandins ambazo hupelekea Mfuko wa Uzazi kujikunja na kuweza kutoa Mtoto Wakati wa Kujifungua lakini pia huweza kupelekea Ongezeko kubwa la mjongeo wa Utumbo Mdogo hivyo huweza kupelekea Dalili za Kuharisha kwa Mjamzito.
Hutofautiana kati ya Mjamzito moja na mwingine.

7. Maumivu ya Kubana na Kuachia.
Maumivu ya kubana na kuachia hutokea katika kipindi chote Cha Ujauzito, Lakini endapo Maumivu hayo hayana Mpangilio maalumu basi huwa ni Dalili za Mwanzoni za Kujifungua tofauti na Uchungu Kamili ambapo Maumivu huongezeka kadiri Muda unavyoenda na huwa na Mpangilio maalumu.

8. Mtoto kupunguza kucheza.
Kwa kawaida Wajawazito huanza kuhisi Mtoto kucheza kuanzia Wiki ya 20 kwenda juu na Mtoto huongezeka kucheza kadiri umri wa Mimba unavyoongezeka na kufikia Wiki ya 32 Mtoto hucheza zaidi baada ya hapo Mtoto hupunguza Kucheza kwa sababu anakuwa ameshuka kwenye Nyonga tayari kwa ajili ya Kutoka na Kuzaliwa.

Bonyeza hapa Dalili za Uchungu usiohalisi

MUHIMU:
Endapo Mtoto amepunguza kucheza unatakiwa kwenda hospitali kwa ajili ya kujihakikishia kuwa hana shida nyingine.

Dalili za Uchungu wa Mwanzoni

Response to "Dalili za Mwanzoni za Kujifungua au Uchungu kwa Mjamzito."

  • Wiki ya 34 kutumia mishipa kwenye kine na kwa upande wa kushoto yaaa I maumivu makalu hii ni nini Hasa nakosa raha

  • Habari,mke wangu Leo hii ameanza kuhisi dalili za kushika na kuachia wiki ya 36, pia kutokwa na Ute mweupe, je ni dalili gani? Na Nini tufanye,

  • Tarehe 25 mwez wa tisa ultrasound nilipiga ikasema mimba ina week 39 na pia ikasema tarehe ya kujifungua ni leo tarehe 8 ila me nina kama week mbili naumwa nyonga na uku chini kuna vuta kama kuna kitu kinaachia inaweza kuwa uchungu ila sion makamas wala maji maji

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *