DALILI 30 ZA MIMBA CHANGA (Wiki 2 mpaka Miezi 3 ya Ujauzito)

DALILI 30 ZA MIMBA CHANGA (Wiki 2 mpaka Miezi 3 ya Ujauzito)

DALILI 30 ZA MIMBA CHANGA (Wiki 2 mpaka Miezi 3 ya Ujauzito)

Mjamzito mwenye Ujauzito wa kuanzia wiki 2 mpaka mwezi mmoja anaweza kuwa na Dalili zifuatazo;

  1. Kutoona siku zako au Hedhi yako kwa Mjamzito.
  2. Kupata kichefu chefu na kutapika kwa Mjamzito.
  3. Kuchoka Sana Mara kwa Mara kwa Mjamzito.
  4. Kutokwa na Damu kama Matone kwa Mjamzito .
  5. Kulala Mara kwa Mara kwa Mjamzito
  6. Kutokwa na Ute mwingi Ukeni kwa Mjamzito.
  7. Matiti/Maziwa kuuma kwa Mjamzito.
  8. Kubadilika kwa Harufu kwa Mjamzito.
  9. Chuchu Kubadilika Rangi na kuwa nyeusi kwa Mjamzito.
  10. Matiti kuwa makubwa zaidi na kuongezeka Uzito kwa Mjamzito.
  11. Maumivu ya Tumbo ya kubana na kuachia kwa Mjamzito.
  12. Maumivu ya Kiunoni kwa Mjamzito.
  13. Maumuzi ya Mgongoni karibia na kiunoni kwa Mjamzito.
  14. Mapigo ya Moyo kwenda mbio ktk kipindi cha Ujauzito.
  15. Kujaa Mate Mdomoni mwa Mjamzito.
  16. Mdomo kuwa Mchungu kwa Mjamzito.
  17. Mjamzito kula Udongo.
  18. Tumbo la Mjamzito kujaa Gesi.
  19. Kupunguza hamu ya kufanya Tendo la Ndoa ktk kipindi cha Ujauzito.
  20. Kukojoa Mara kwa Mara katika kipindi cha Ujauzito.
  21. Kupata kiungulia ktk kipindi cha Ujauzito.
  22. Mjamzito kuwa na Chunusi Usoni.
  23. Mjamzito kuwa Mstari Tumboni ambao unatoka sehemu ya chini ya kifuani mpaka kwenye sehemu ya chini ya Kitovu karibia na mfupa wa Kinena.
  24. Tumbo la Mjamzito kuwa na Michirizi ktk kipindi cha Ujauzito.
  25. Mjamzito kutokwa na Damu Puani au kwenye Fizi/Meno katika kipindi fulani Cha Ujauzito.
  26. Baadhi ya Wajawazito hupata Bawasiri au vinyama vinavyokuwepo kwenye njia ya haja kubwa.
  27. Mjamzito Kupata maumivu ya Kichwa.
  28. Mjamzito kukosa Usingizi.
  29. Kubadilika kwa mhemuko au Mudi.
  30. Tumbo kuwa kubwa na kuongezeka katika kipindi cha Ujauzito Kutokana na ukuaji wa Mtoto Tumboni na nk.

KUMBUKA; Dalili pekee hazitoshi kuonesha kuwa Mjamzito kuna Baadhi ya Magonjwa huwa na Dalili zinazofanana na Baadhi ya Dalili za Ujauzito,
Hivyo ni vema kuweza kufanya kipimo Cha Mimba Cha Mkojo (UPT) endapo unahisi kuwa na Ujauzito.
Kipimo hiki kinapofanyika siku ya 10 au 14 tokea Mimba kutungwa huweza kuonesha Majibu sahihi kwa asilimia 99% na endapo hakikuonesha Mimba na bado unapata Dalili za Mimba unaweza kurudia kipimo hiki siku 3 – 5 tokea ufanye kile kipimo Cha kwanza.

Mkojo wa kutumia ili kupima Mimba ni Mkojo wa ahsubuhi huwa na kiwango kingi Cha Homoni ya HCG ambayo hugunduliwa na kipimo Cha Mkojo (UPT).

https://youtu.be/cFrUimnSMuo

Response to "DALILI 30 ZA MIMBA CHANGA (Wiki 2 mpaka Miezi 3 ya Ujauzito)"

  • Nina miaka hamsini na cjaona miezi 2,nimekua na kiungulia,tumbo kujaa upepo,kuchoka cna na kulala cna na maumivu ya kiuno kama kwamba nitapata damu ya mwezi lalini hamna.Je naeza kua mja mzito kweli hasa na umri wangu

  • nilifanya tendo la ndoa siku ya saba nikaanza kusikia kichefu chefu na kutapika na tumbo kuuma chini ya kitovu km nataka kuingia hedhi je ni dalili ya mimba?

  • Nikila kuna mda naisi kichefuchefu lkn sijawai tapika na naisi maumivu ya mgongo yaani uti wa mgongo kama unachoma na nakojoa mkojo wenye arufu kali matiti yananiuuma sana na ninalala sana lkn tabia ya kulala uvyo ninayo toka zaman na sioni sikuzangu na ninatokwa na uchavu mweipe kwa wingi na nimeongezeka uzito ni mwezi wa pili sasa lkn auna harufu inaweza kuwa ujauzito?

  • Nili bebe mimba ikatoka mwenz wa pili mwaka huu mbaka sas sijapata mimba ten na mimb yangu ime alibikika ikiwa ya mwezi mmoj na nusu sas sijui nitakuwa natatizo gan ??

  • Sku zangu huwa haziji kwa mpangilionaweza nkavusha hata mwez nkaingia mwezi mwingine na tarehe hazijawahi kuja kwa moangilio mzuri na nakumbuka hedhi yang ya kwanza nilienda siku 17 ila baada ya kufanya tendo najikuta muoga Sanaa maana nahis kuwa nina mamba japo mwenza wang aliniambia kuwa hakufanya mistake ndani ya uke wang ila shuka lililoa bado nahis kuogopa sana

  • Ninamiaka 26 mm nilipitiliza mwezi moja na siku 10lakin damu ilikuwa inanitoka matone matone alafuinakata siku ya kumina 15 ikaja ikatoka damu nyingi.sana nikaenda siku 10. Talehe24 NIKAWA nikosawa nikakutana kimwili . .sasa nashangaa ninadalili kizungu zungu na kutapia

  • Nina miaka 44 nimemaliza siku zangu tar 23/11 Sasa nashangaa tar6)12 zimejirudia na maumivu ya tumbo na kiuno

    • Mie nilienda period mwezi wa 3 trh 7 mwakahuu lakin mpka mwezi wa nne ukapita mwezi huu wa tano trh mbili nimeenda kukojoa vimetoka vidamu na tumbo la chini linauma ila hili lakuuma tumbo nikila siku linauma lkin Leo ndo vidamu vimetoka shida itakuwa nn

  • Dr tumbo linauma chini ya kitovu,ute umezidi kuwa mwingi ukeni,na maumivu ya kichwa napata lakio sio mara kwa mara joto linapanda
    Je itakuwa ni nn dr??

  • halaf pia napta maumivu ya tumbo,kiuno,kichwa n chuchu zinauma na pia tumbo langu Liko na gesi xn xx cjui itakuw nn naomb unixaidie

  • Hajaona siku zake siku12 ,anakojoa mala kwa mala na kipimo Cha UPT kimeonyesha mimba ila Cha ajabu damu imetoka alafu ikakata,je ni nini?

  • Habari Dr naomb kuuliza mm yaan ziwa moja linaniuma xana na linatoa majimaji sijui shida ni nn

  • Mimi NILIPATA bleed tareh 22
    Nikamaliza tareh 26
    Then tareh 27 ,28,1 mwez wa 5
    Nilisex
    Nikawa napata dam ndogo tu za cku 2 zinaisha
    Nikaendelea kujisikia vibaya tareh 8 mwez wa 5 nimepima u.p.t inaonesha positive ndo najiuliza inawezekana ikawa ni mimba????? Na nimepima kwa vipimo v3 vyote vinaonesha ivo

  • Nina umri wa miaka 25 na sioni siku zangu ila sina dalili yoyote ya mimba shida ni nn au inaweza kuwa ni sababu ya kubadilisha mazingira.

  • Ndugu yang anashida samahani dokta Mimba iliharibika mwezi wa 4 tarehe 15 hadi leo mimba Bado inasoma ipo je Ni mimba nyingine au mimba ya mwanzo inasoma?

      • Habari nina dada yangu anaujauzito wa wiki ya nne sasa ila ameanza kupata maumivu ya mgongo kiuno na tumbo leo ni siku ya tatu na akienda haja ndogo mkojo unakua msafi ila mwisho kabisa anaona matone ya damu je nini afanye mana ameenda duka la dawa wanasema viashiria vya mimba kutoka na wamempa phenobabiton na buscopai

  • Mimba yangu ilitoka nliona vinyamanyama tuh na damu kidogo ikawa inaendelea iliyopauka mimba ilikuwa wiki mbili ila sasa hiv nashika chini ya kitovu kwa mbali nahisi ugumu shida ni nini?? Haijatoka ama

  • mm nilikuwa natumia sindano za uzazi lakn ilipo isha muda sikuchoma na nikapata siku zangu 26 mwez wa 5 mpka ss sijaona tena lakin nimekuwa pono na mvivu sana chuchu zimeanza kuuma nina wiki ss nimepima lakin kipimo kimekuja negative hvi nitakuwa na dalili ya nn

      • Habari Mimi nilikua natumia dawa za kupanga uzazi ndani ya mwaka mmja na nikaziacha tokea mwezi wa nne nikapata period mwezi wa tano na sasa imefika miezi 3 sijapata periods naumwa chini ya kitovu na nimepima mimba zaidi ya Mara tano sina mimba na dalili zote za mimba nikonazo na nimepima kila ugongwa sina sasa itakua ni nn nisaidieni na mawazo maana mwili wangu naona unaongezeka kila Mara.

    • Habari mama mjamzito wa wiki 8 anaumwa sana tena mara kwa mara akienda kupima hana ugonjwa ila anasikia maumivu tumboni na kichwa kuuma pia kuhisi homa hii inasababishwa na nini na ikiwa huu ni ujauzito wake wa kwanza
      Na nini anapaswa kufanya ili awe sawaa

  • Mim nilikutan namr wangu baada ya hapo Huw nahisi homa hasa asubuhi na usku na tumbo linaniuma kama ntaka kuingia kweny period na vitone vya damu alfu vinakta unatoka Ute mwingi mweupe hii inawez kuw mimb?

  • Shida yangu huwa nahisi tumboni kuna vitu vinacheza shida nin?. Na jambo lingine nimeshangaa kuingia kwenye siku zangu mala mbili na haijawai nitokea

  • Dr. Mke wng toka atoe ujauzito mwez wa 2 mpaka leo hajawahi kukaa sawa kwenye siku, mwezi wa 4 alienda sku 13 ila maumivu yalizidi mpaka nikampelela hosptl wakampa dawa na sindano, akakaa sawa ila mwez wa tano na wa sita kaingia sku 6 mpaka 7. Mwez huu wa sita ikiwa naendelea kulala nae tena sku za ovulation ili apate mtoto kwa mda huu ameingia leo asubuhi kwa kuona mabonge bonge basi then ikakata alivoenda kukojoa. Je tatizo ni nini doc.?

    • Kama Mimba iliharibika mnatakiwa msubiri angalau miezi 6 pasipo kupata Mimba ili Mkeo Mji wa Uzazi uweze kupumzika, sasa mpeleke hospitali kafanyiwe vipimo zaidi ili kujua shida yake haswa ni ipi?!

  • Samahan doctor mm nilipata hedhi tareh 30 mwez5 ila ilikuwa siku yangu imebadirika nilishangaa sana kuona siku zimebadirika nikajua tapa tena siki zang tareh 7 mwez 7 ila chakushangaza sijapata siku zangu mpk hii tareh 14 ila napata maumiv yakiuno kama naingia kwenye siku zang nq chuchu zinauma
    Sanq kichwa na mgongo inaweza ikawa nn docter

  • Sijawahi fanya mapenzi ila Nina Mpenz I amabaye huwa tunafanya lakini hajawahi kabisa kuingiza ndani yaani hufanya juujuu tu.je hapo naweza kupata mimba?

  • Niliona Ute wa uzazi siku ya Saba ya hedhi nikafanya mapenzi siku hiohio ya Saba saiv mwili hauna nguvu nahisi kulala Kila muda naona Ute mwing unatoka ukeni mdomo mchungy.

  • Habar docta swal langu n kwamba cjapata hedh mwez huu na zmepitilza xk 5 kuna mda nahisi dalil za hedh lkn cn dalil yyt ya mimb n matit kujaa t sijajua nbtatzo gan

  • Dr mm nimemaliza piriad nikakutana na mume wangu siku zangu za hatari lkn saiv tumbo linaniuma sana chini ya kitovu mda mwengine mpaka chini kunavuta mpaka kiuno kinauma nikifanya kazi za kuinama sana mgongo unauma nimetoka chunusi maziwa yanauma mda mwengine kama nataka kuingia kwenye piriad lkn tarehe yangu bado sana inaweza ikawa ni mimba mda mwengin nikimaliza kusex tumbo linauma sana

  • Naomba kuuliza Kuna dalili naziona natema sana mate mdomo mchungu nachagua vyakula miguu Haina nguvu….Cha hajabu jana nilipo amka na kwenda chooni nikaona Ute Ute umachanganyika na damu Kwa mbali

  • Nina maumivu sana ya kiuno na mgongo na mda mwingine swezi fanya kazi nikiwa nmeinama mpaka nikiwa nimekaa.. mwili nao unachoka saanaa je na mim nitakuwa na ujauzito??

  • Sina dalili za mimba kama vile kichefuchefu wala kutapika na zingne pya lakin kipimo cha mkojo kinaonesha na mimba je hii inawezekan?

  • Habari mama afya pole na majukumu ya kazi..mimi siku nane baada ya kukutana na mwenza wangu nilianza kutokwa na damu natone haijai kwenye pad na nikifuta inakuwa na rangi ya pink nikajaribu kupima mimba ikatokea mstari moja umekoa na mwingine umefifia,baada ya siku tatu nikapima tena majibu yakaja negative sasa sielewi shida ni nini

  • Samahn sifaham jinsi ya kuhesabu mzunguko mfano nimeanza piriod tareh 18 mwez 12harafu nikaanza Tena piriod tarehe 15mwez wa1 je hapo na hesabu vip ili
    kujuwa siku ya kushika ujauzito

  • Samahani DR Mimi nilikutana na mpenzi wangu siku ya 18 na ya 25 januari baada ya period lakini mpaka sasa sijaingia period je naweza kupata mimba?

  • Nina zaid ya wiki mbili napata dalili zote za mimba ila wiki ya tatu kwenye tarehe zang za period nimeingia period lkn damu ni nyepesi na kichwa kinauma pamoja na maumivu ya tumbo chini ya kitovu na nilipima mimba wiki moja kabla ya hedhi kipimo kikaonyesha sina je hii inaweza kua ni nini?

  • Habari, naomba kuuliza niliweka kipandikizi (kijiti) Cha miaka 3 lakini nilikitoa baada ya miezi 4 tu kwasababu ya changamoto nilizokuwa napitia kama kuumwa mara kwa mara na matone ya damu Kila wakati. Tangu nimekitoa Nina week mbili sasa sijaingia period je naweza kuwa na shida mahala?

  • Habari naomba kujua kuwa nimepitiliza siku zangu Leo siku ya 2 Ila nahisi maumivu ya tumbo LA period kwa mbali Siku ya tatu hii hali lakini dam hazitoki hii inaweza kuwa shida gani?

  • Habari Dr
    Me nimekutana na mwenzangu katika siku zangu za hatari lakini sioni dalili zozote za mimba ila tarehe zangu za period zimepita na sijaona siku zangu je naweza kuwa mjamzito

  • Mm sijaona siku zangu nimepitiliza siku 4 lakin; naumwa tumbo kam nataka kuingia p, pia naumwa kiuno na uchovu na sipat haha kubwa je shida itakuwa nn

  • Mim nahc kichefuchefu,kichwa kinauma na tumbo langu limeanza kukua,mwili umechoka,uchovu mood ni hasira sana lakn cha ajabu nimeenda period ck 7, ambayo c Kawaida na nimechelewa kupata period…inawezekana ikawa ni mimba?

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *