Ugonjwa wa Fangasi Ukeni kwa Mjamzito na Matibabu yake! (VAGINA CANDIDIASIS / VULVOVAGINAL CANDIDIASIS (MONILIASIS).

Ugonjwa wa Fangasi Ukeni kwa Mjamzito na Matibabu yake! (VAGINA CANDIDIASIS / VULVOVAGINAL CANDIDIASIS (MONILIASIS).

Ugonjwa wa Fangasi Ukeni kwa Mjamzito na Matibabu yake! (VAGINA CANDIDIASIS / VULVOVAGINAL CANDIDIASIS (MONILIASIS).

Fangasi za Ukeni kwa Wanawake huwa ni Ugonjwa ambao unawapata kwa kiasi kikubwa (40%) haswa baada ya kubarehe hadi kipindi cha ukomo wa wanawake kushika ujauzito(Miaka 12 – 45).

Fangasi za Ukeni huweza kuathiri haswa akina Mama Wajawazito kwa (10% – 75%), Akina Mama/Dada wanatumia Dawa za kuua vijidudu kiholela, Watumiaji wa Dawa za kupunguza kinga mfano; Corticosteroid na Dawa za kutibu Saratani mbalimbali na wenye Upungufu wa Kinga kutokana na Magonjwa kama Kisukari au HIV/AIDS na nk.

JE NI KWA NINI AKINA MAMA WAJAWAZITO HUPATA ZAIDI (10% – 75%) FANGASI UKENI?
Sababu zinazopelekea Mama mjamzito kuwa kwenye hatari ya kupata fangusi ukeni ni kama zifuatazo!

1. Ongezeko kubwa la homoni za Progesterone na Estrogen wakati wa ujauzito,hususani homoni ya estrogen ambayo husababisha ongezeko la glycogen na hii hufanya ongezeko la ukuaji wa Fangasi hawa kwa kasi kubwa japokuwa pia estrogen hupelekea ongezeko la wadudu walinzi akina Candida Albicans!

2. Unapokuwa mjamzito kinga yako ya mwili huwa chini na hivyo hupelekea kuharibiwa kwa msawazo kati ya ulinzi wa maeneo ya ukeni na Fangasi aina ya Candida Albican ambapo endapo wadudu walinzi aina ya Lactobacilli wakipungua hupelekea ukuaji mkubwa wa Fangasi na kupelekea dalili za ugonjwa wa Fangasi!

3. Endapo Mama mjamzito anatabia ya kutumia dawa za kuua vidudu mfano wadudu wanaosababisha ugonjwa wa UTI au Magonjwa ya zinaa kiholela au kwa muda mrefu hupelekea kuharibiwa kwa msawazo kati ya ulinzi wa maeneo ya ukeni na Fangasi aina ya Candida Albicans ambapo endapo wadudu walinzi aina ya Lactobacilli wakipungua hupelekea ukuaji mkubwa wa Fangasi na kupelekea dalili za ugonjwa wa Fangasi!

DALILI ZA FANGASI ZA UKENI.

1. Kutokwa na uchafu ukeni au kuwepo kwa uchafu huo kwenye kuta za uke na kwenye mashavu ya uke, ambao hufanana na maziwa yaliyoganda au wakati mwingine huwa kama maziwa yaliyo chacha na pia hautoi halufu yoyote kali!

2. Kupata miwasho ukeni.
Kutokana na ongezeko la fangasi kwa Mama Mjamzito atakuwa anapata dalili za kuwashwa mara kwa mara ukeni.

3. Uke kubadilika rangi na kuwa rangi nyekundu zaidi.

4. Maumivu ya kuchoma choma, Mama mjamzito kuhisi kama vitu vinachoma choma!

5. Kujisikia vibaya wakati wa tendo la ndoa na kupata maumivu wakati wa kukojoa!

Jizuie au Punguza Dalili za Ugonjwa wa Fangasi Ukeni kwa kufanya mambo haya!

1. Hakikisha unakuwa msafi fua nguo za ndani Mara kwa Mara na anika nguo hizo juani!

2. Usiingize vidole kwenye uke kwa ajili ya kupunguza miwasho kwa kufanya hivyo utaongeza uwezekano wa kupata vijidudu ambao wanasababisha magonjwa mengine!

3. Epuka kutumia dawa za kuua vijidudu mfano wa UTI au Magonjwa ya zinaa kiholela bila ithini ya Daktari!

4. Matumizi ya Dawa za kupaka au kuweka Ukeni mfano: Clotrimazole pessaries, Miconazole cream na nk, Kumbuka usitumie Dawa za kunywa za fangasi katika kipindi cha Ujauzito kwa sababu huweza kuathiri Mimba yako mfano; Fluconazole

Unaweza kujifunza kwa kupitia video hapa

Response to "Ugonjwa wa Fangasi Ukeni kwa Mjamzito na Matibabu yake! (VAGINA CANDIDIASIS / VULVOVAGINAL CANDIDIASIS (MONILIASIS)."

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *