Ugonjwa Unaoathiri Meno Katika Kipindi Cha Ujauzito (Pregnancy Gingivitis)!
Ni shida au Ugonjwa unaoathiri baadhi ya Wajawazito ambapo Dalili zake huweza kuanza kuonekana kuanzia mwezi mmoja wa ujauzito mpaka miezi Tisa na hupotea Mara baada ya kujifungua au baada ya muda fulani baada ya kujifungua,Ugonjwa huu hutokana na mabadiliko mbalimbali wakati wa ujauzito na hutokea hususani Mimba inapofikisha miezi 4 hadi 8!.
Ugonjwa huu huathiri zaidi Fizi au Sehemu ya Meno kwenye kinywa sehemu ya mbele zaidi sehemu au Meno ya juu!
Shida au ugonjwa huwa na Dalili zifuatazo;
1. Kutokwa na Damu kwenye Fizi Mara baada ya kuswaki au wakati mwingine bila kuswaki!
2. Kubadilika rangi ya Fizi na kuwa nyekundu zaidi!
3. Fizi kuvimba wakati mwingine Mjamzito anaweza kuvimba na akahisi ni uvimbe kama saratani kumbe siyo saratani!
4. Fizi kuwa nyembamba na laini hivyo huweza kutoa Damu endapo utasugua kwa kutumia Mswaki wenye vibashio vigumu sana!
na nk
FANYA MAMBO HAYA ILI KUPUNGUZA DALILI HIZO ZA SHIDA YA MENO WAKATI WA UJAUZITO!
1. Swaki meno yako Mara mbili kwa siku kwa kutumia Mswaki wenye vibrashio vilaini na pia tumia dawa ya Meno yenye fluoride!
2. Badili Mswaki unaotumia kila baada ya miezi 3/4 au unapoona Mswaki wako umeisha.
3. Tumia Mswaki unaotosha kinywa chako hakikisha Mswaki wako usiwe mdogo wala mkubwa sana kwa sababu unaweza kuumiza Fizi au Kinywa chako!
4. Ukisha Swaki Meno hakikisha unasafisha sehemu zilizopo kati ya Jino na Jino!
5. Kula vyakula vya asili na visivyo na sukari!
6. Kula vyakula vyenye Vitamin C na B-12 kwa wingi
7. Mwone Daktari wa Meno endapo njia hizo hapo juu hazija kusaidia!
Response to "Ugonjwa Unaoathiri Meno Katika Kipindi Cha Ujauzito (Pregnancy Gingivitis)!"
Nafurahia masomo yako