Je Mjamzito anatakiwa kulalia Upande wa Kushoto Mimba inapofikisha wiki ngapi?
Endapo wewe ni Mjamzito kwa Mara ya kwanza tambua ya kwamba kuna Mambo unatakiwa kuacha kufanya endapo ulikuwa unafanya kipindi ambacho hukuwa Mjamzito lakini pia unatakiwa kuanza kufanya Mambo mapya katika kipindi cha Ujauzito.
Unapofikia Umri fulani wa Ujauzito unatakiwa uanze kujizoesha kulala Upande na hutakiwi kulala kwa kutumia Mgongo au Tumbo au vile ambavyo ulikuwa unafanya kipindi ambacho si Mjamzito.
Je Mjamzito anatakiwa kutumia upande gani wakati wa kulala!?
Mjamzito anashauriwa kutumia Upande wa Kushoto kuweza kulala kuliko Upande wa kulia au Mgongo au kulala kwa kutumia Tumbo.
Je ni lini Mjamzito anatakiwa kuanza kulala kwa kutumia Upande wa Kushoto?
Mjamzito unashauriwa kuweza kulala kwa kutumia Upande wa Kushoto Mimba inapofikisha umri wa Miezi 5 au wiki 20 kwenda juu lakini haswa unatakiwa kuhakikisha utatumia upande wa kushoto zaidi Mimba inapokuwa Miezi Mitatu ya Mwishoni kuanzia wiki 28 kwenda juu!.
Endapo Mimba yako ina umri wa Miezi Mitatu ya mwanzoni unaweza kuendelea na utaratibu wa kulalia Tumbo,Mgongo au Upande wowote ule ambao unajisikia vizuri kuweza kutumia.
Ukweli ni kwamba endapo Tumbo lako linapoanza kuwa kubwa hata kama Mimba Ina umri wa wiki 16 au 18 hususani kwa wale wenye Mimba za Mapacha wanatakiwa kuanza kujizoesha kulalia Upande wa Kushoto zaidi kuliko Upande wa Kulia au Mgongo.
Kwa Nini Mjamzito hashauriwi kulala kwa kutumia Upande wa Kulia?
Mjamzito anatakiwa kutumia Upande wa kushoto na siku kulia Mara kwa Mara kwa sababu;
Mishipa mikubwa Miwili ya Damu huwa sehemu ya nyuma ya Tumbo katika yake japokuwa huwa iko upande wa kulia zaidi hivyo Mjamzito anapotumia upande wa kulia kuna asilimia chache za uwezekano wa Kugandamizwa kwa Mishipa hiyo na kuleta athari kwa Mtoto kutokana na Kupungua kwa usafirishwaji wa Damu kutoka na kwenda kwenye mfuko wa Uzazi.
Je Mjamzito akilala kwa Mgongo apata Madhara yapi?
Endapo Mjamzito atalala kwa kutumia Mgongo atapata shida au Tatizo la kupungua kwa usafirishwaji wa Damu kutoka na kwenda sehemu ya chini ya Mwili, hii hutokana na Kugandamizwa kwa Mishipa mikuu Miwili ambayo ni Vena ya chini na Aota ambayo hutoa Damu chafu kutoka sehemu za chini za Mwili kwenda sehemu ya Kulia ya Moyo kwa ajili ya kusafishwa na kupeleka Damu Safi kutoka sehemu ya Kushoto ya Moyo kwenye sehemu ya chini ya Mwili ikijumuisha Mfuko wa Uzazi na Kondo la Nyuma kila mmoja.
Tafiti zinaonesha kwamba asilimia 80 ya Damu inayosafirishwa kwenye Mshipa wa Vena ya chini huathiriwa kutokana na Kugandamizwa kwa Mshipa huo endapo Mama amelala kwa kutumia Mgongo, vile vile hii huweza kutokea endapo Mama amelala kwa kutumia Tumbo japokuwa wanawake wengi huwa hawawezi kulalia Tumbo kwa sababu hujisikia vibaya.
Kutokana na Upungufu wa usafishwaji wa Damu katika Mwili kwa Mjamzito aliyelala kwa kutumia Mgongo;
- Huweza kupelekea kujifungua Mtoto ambaye ana Uzito mdogo ukilinganisha na umri wa Mimba au,
- Mtoto kufia Ndani katika kipindi cha Ujauzito,Mimba inapofikia wiki 28 kwenda juu au Miezi 3 ya Mwishoni mwa Ujauzito.
Tafiti zinaonesha kwamba Kati ya Mimba 10 ambazo Watoto walifia Tumboni kwenye Miezi Mitatu ya Mwishoni, Mimba 1 Ambapo Mtoto alifia Tumboni ilitokana na Mjamzito kulala kwa kutumia Mgongo hususani Mimba inapofikisha wiki 28 kwenda juu.
Je endapo Mjamzito alilala kwa kutumia Upande wa Kushoto alipoamka akajikuta amelala kwa kutumia Mgongo afanyaje?
Kwanza kabisa nikutoe hofu kwamba hiyo huwa inatokea unatakiwa usihofu kabisa,unachotakiwa kufanya unalala kwa kutumia Upande wa Kushoto tena endapo bado utaendelea kulala katika huo muda. Je ni Muda wote nao lala natakiwa kulala kwa kutumia Upande wa Kushoto?
Ndio, iwe mchana au unapoenda kulala usiku au kama ukiamka kwa ajili ya kwenda choo usiku unaporejea Kitandani unatakiwa kulala kwa kutumia Upande wa Kushoto.
Je Mjamzito ambaye anapata maumivu makali anapolala kwa kutumia upande wa kushoto afanye nini ili kuhakikisha kuwa ana Afya Bora?
Endapo Mjamzito anapata maumivu makali anapolala kwa kutumia upande wa kushoto anatakiwa kutumia upande wa kulia na anahitaji kutumia mto wa Ujauzito ambao huwa na umbile la C au U huu huweza kukusaidia kupunguza uwezekano wa Kugandamizwa kwa mishipa hiyo ya Damu na kuleta athari.
No comments.