Kwa nini ni muhimu Mjamzito kushiriki Tendo la Ndoa?

Kwa nini ni muhimu Mjamzito kushiriki Tendo la Ndoa?

Kwa nini ni muhimu Mjamzito kushiriki Tendo la Ndoa?

Tendo la Ndoa ni Mojawapo ya starehe ambayo Mwanadamu alipewa na mwenyezi Mungu.Japokuwa zaidi ya 50% ya Wajawazito kupunguza hamu ya kushiriki Tendo hilo katika kipindi Cha Ujauzito ukilinganisha na kipindi kabla ya wao kuwa Wajawazito. Hii ni kwa sababu ya mabadiliko mbalimbali ya:

Homoni (Ongezeko la Estrogeni, Progesteroni,Prolactin na Relaxin),

Kisaikolojia ambapo wakati mwingine huchangiwa na imani mbali tajwa hapo chini.

Mwili kiujumla katika kipindi cha Ujauzito mfano; Ukuaji wa Mfuko wa Uzazi ambao hupelekea maumivu mbalimbali na Kupungua kwa upana wa Uke kutokana na ukuaji wa Seli mbalimbali ambazo huchochewa na Homoni ya Relaxin.

Miezi ya Mwanzoni mwa Ujauzito Mjamzito anaweza kuwa na hali ya kutapika mara kwa mara na nk ambayo huweza kupelekea kupungua kwa hamu ya Tendo hili.
Japokuwa baadhi ya Wajawazito hamu huweza kuongeza kwenye kipindi cha Kati cha Ujauzito (Miezi Mitatu ya katikati) na badae hupungua zaidi kwenye Miezi Mitatu ya Mwishoni mwa Ujauzito.

Imani mbalimbali ambazo ni Potofu.

IMANI POTOFU KUHUSIANA NA TENDO LA NDOA KIPINDI CHA UJAUZITO.

Kumekuwa na Imani nyingi kuhusiana na Mwanamke Mjamzito kushiriki Tendo la Ndoa kipindi cha Ujauzito mfano wa Imani hizo ni kama.

1.Mjamzito akishiriki Tendo la Ndoa kipindi cha Ujauzito basi Mbegu za Mwanaume huweza kumharibu Mtoto aliyepo Tumboni.

Mjamzito akishiriki Tendo la Ndoa njia itafunguka na Mwisho wa siku Mimba itaharibika.

Mjamzito akishiriki Tendo la Ndoa basi inawezeka inapelekea Mtoto kuweza kupata athari mfano; kuumia.

Mjamzito akishiriki Tendo la Ndoa anaweza kusababisha Maambukizi ya vijidudu kwa Mtoto aliyeko Tumboni.

Mjamzito akishiriki Tendo la Ndoa kipindi cha Ujauzito Chupa inaweza kupasuka na kusababisha Maji kupungua kwenye Mji wa Uzazi kutokana na kuvuja kwa Maji hayo.

Uoga na Imani za Tamaduni mbalimbali.

MJAMZITO ANAWEZA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA KAMA KAWAIDA.

Ukweli ni kwamba Mjamzito anaweza kushiriki Tendo la ndoa kama kawaida kwa muda wote katika kipindi cha Ujauzito mpaka kabla Uchungu unapoanza.
Ijapokuwa endapo Mjamzito ana changamoto za Ujauzito anaweza asishiriki Tendo hilo kulingana na yeye anavyoona au Mara baada ya kuzuiwa na Daktari kutokana na sababu za kiafya.

TAFADHARI ZA KUCHUKUA.

Endapo Mjamzito atakuwa na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kuathiri Mimba au Afya yake hataruhusiwa kushiriki Tendo la Ndoa,Mfano wa Changamoto hizo ni kama;-

Kutokwa na Damu katika kipindi cha Ujauzito.

Mimba kutishia kutoka au kuharibika.

Mwanamke au Mjamzito mwenye historia ya kuharibikiwa na Mimba Mara kwa Mara kutokana na Udhaifu wa Mlango wa Uzazi.

Mwanamke mwenye historia ya kujifungua Mimba kabla au chini ya Wiki 28.

Endapo Kondo la nyuma limejishikiza karibia na Mlango wa Uzazi na Mjamzito anatokwa na Damu.

Wakati mwingine Mjamzito anaweza asishiriki Tendo hilo kutokana na mabadiliko ya Homoni ambayo yanaweza kupelekea kujisikia vibaya, kutapika Mara kwa Mara hususani kipindi cha Miezi Mitatu ya mwanzoni, kupungua kwa hamu ya Tendo la Ndoa, Hata kama hana shida ambazo zimetajwa hapo juu.

JE MTOTO ALIYEPO TUMBONI ANAWEZA KUATHIRIWA KUTOKANA NA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA.
Endapo huna changamoto yoyote kati ya Tano zilizo tajwa hapo juu.
Unaposhiriki Tendo la Ndoa hata kama Mbegu za Mwanaume zikimwagwa kwenye Uke, Mtoto hawezi kuathiriwa. Hii ni kwa sababu Mtoto hulindwa na Kuta ngumu au Chupa imara inayo mzunguka lakini pia Mlango wa Uzazi huwa umefungwa vizuri na hauwezi kupitisha kitu chochote labda kama kutakuwa na Maambukizi ya vijidudu ambayo yamepelekea kupasuka kwa Chupa au kuchanika kwa Kuta zinazo mzunguka Mtoto.

UMUHIMU WA TENDO LA NDOA KIPINDI CHA MIEZI MITATU YA MWISHO YA UJAUZITO.
Baadhi ya Maandiko yanaelezea kwamba Mjamzito ambaye hana changamoto tajwa hapo juu, anaposhiriki Tendo la Ndoa ipasavyo husaidia katika kuanzisha Uchungu na kuivisha Mlango wa Uzazi na hivyo huwezesha kuanzishwa kwa Uchungu kipindi ambacho Mjamzito anatakiwa kujifungua.
Hii ni kwa sababu:

•Kwenye Ute uliochanganyika na Mbegu anaotoa Mwanaume kuna kiasi kidogo cha kemikali ya prostaglandini E ambayo huanzisha Uchungu mwishoni mwa Ujauzito.

Tendo la Ndoa husababisha utolewaji wa Homoni ya Oksitosini ambayo huhusika katika kuhakikisha Mjamzito anapata Uchungu.

Husaidia kuongeza nguvu ya kubana na kuachia ya mfuko wa Uzazi ili kuweza kumtoa Mtoto nje na kujifungua kwa Mjamzito.

Mapenzi au Tando la Ndoa wakati wa Ujauzito


Response to "Kwa nini ni muhimu Mjamzito kushiriki Tendo la Ndoa?"

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *