Je Mjamzito aliyewahi kujifungua kwa Upasuaji anaweza kujifungua kwa njia ya kawaida!
JE MJAMZITO ALIYEWAHI KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI ANAWEZA KUJIFUNGUA MIMBA INAYOFUATA KWA NJIA YA KAWAIDA?.
Mjamzito ambaye aliwahi kujifungua Mara moja kwa Upasuaji kwenye Mimba iliyopita na endapo sababu iliyopelekea kujifungua kwa Upasuaji siyo ya kujirudia rudia basi Mwanamke huyo anaweza kujifungua kwa njia ya kawaida kama wanawake wengine, ijapokuwa anatakiwa kuwa na Vigezo au sifa maalumu zitakazo mfanya aweze kujifungua kwa kawaida.
Mfano: endapo umewahi kubeba Mimba Mara tatu katika maisha yako na Mimba ya kwanza ukajifungua kawaida, Mimba ya Pili Kuna sababu ilipelekea kujifungua kwa Upasuaji Kuna uwezekano mkubwa wa kujifungua kwa njia ya kawaida kwenye Mimba ya Tatu endapo utatimiza Vigezo tajwa hapo chini.
Tafiti zinaonesha kwamba asilimia 70 mpaka 76 ya Wajawazito ambao wana mshono mmoja yaani Mjamzito ambaye aliwahi kujifungua kwa Upasuaji kwenye Mimba Moja ya nyuma pasipo kuwa na sababu inayopelekea kujifungua kwa Upasuaji Mara kwa Mara.
Mjamzito aliyewahi kujifungua kwa Upasuaji kwenye Mimba iliyopita anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo ili kuweza kujifungua kwa kawaida kwenye Mimba ya karibuni.
Sifa hizo ni kama zifuatazo;
1. Mshono mmoja kwenye mfuko wa Uzazi, yaani Mjamzito ambaye aliwahi kujifungua kwa Upasuaji Mara moja tuu na endapo walikata kwenye sehemu ya chini ya mfuko wa Uzazi.
2. Mjamzito ambaye ana Mtoto mmoja Tumboni na si Mimba ya Mapacha.
3. Uzito wa mtoto unaokadiriwa kuwa kati ya kilo 2.5 hadi 3.4 au Uzito usiozidi kilo 3.5.
4. Mjamzito au Mwanamke mwenye Uzito wa kawaida yaani BMI 18.5 hadi 24.5Kg/M² kabla ya kuwa Mjamzito.
5. Mkao wima wa Mtoto Tumboni ambapo anakuwa ametanguliza Kichwa kisogo kwa mbele na sura kwa nyuma.
6. Umri wa Mshono usiokuwa chini ya miezi 18 au miaka miwili na si zaidi ya miaka minne.
7. Mjamzito asiyekuwa na shida yoyote Mfano,kutokwa na Damu kipindi cha Ujauzito kutokana na Kondo la Nyuma kujishikiza sehemu ya chini ya Mfuko wa Uzazi au presha katika Ujauzito.
8. Mjamzito mwenye Nyonga ya kujitosheleza kuweza kupitisha Mtoto na kujifungua salama.
9. Mjamzito mwenye uhitaji na kuridhia kujifungua kawaida.
10. Hospitali ambayo ina vifaa na watalamu wa kutosha kwa ajili ya kujifungua kwa Upasuaji wa dharula.
Endapo ukiwa na sifa zifuatazo hutakiwi kabisa kujaribu kujifungua kwa kawaida endapo uliwahi kujifungua kwa Upasuaji!
1. Endapo Mjamzito ana Mishono Miwili au Kama una mshono mmoja ambao ulihusisha kukatwa kwa Mji wa Uzazi sehemu ya juu.
2. Mjamzito mwenye Mtoto mwenye Uzito unaokadiriwa kuwa na kilo zaidi ya 3.5.
3. Mjamzito ambaye Mtoto wake amekuwa katika mkao wa ulalo na si wima.
4. Mjamzito ambaye alijifungua kwa njia ya Upasuaji kutokana na Sababu za kujirudia rudia Mfano: Mwanamke mwenye Nyonga ndogo.
5. Mjamzito mwenye Magonjwa mfano: Presha katika Ujauzito, Kondo la Nyuma kujishikiza sehemu ya chini ya mfuko wa Uzazi.
6. Mshono uliokuwa na Umri chini ya Miaka Miwili au zaidi ya Miaka Minne.
7. Mimba ya Mapacha au watoto zaidi ya mmoja.
8. Mwanamke mwenye Uzito mkubwa kupindukia, BMI zaidi 30Kg/M²
9. Mjamzito kutoridhia kujifungua kawaida.
10. Hospitali isiyo na watalamu na Vifaa vya kutosha kwa ajili ya kufanya Upasuaji endapo kuna Dharula imetokea.
Endapo una sifa za kuweza kujifungua kwa kawaida endao uliwahi kujifungua kwa Upasuaji basi unaweza kujifungua kwa kawaida bila shida yoyote ile.
Usisahau kudownload application ya Mama Afya Bora pale playstore itakusaidia kujua tarehe ya matarajio na umri wa Mimba yako.
Response to "Je Mjamzito aliyewahi kujifungua kwa Upasuaji anaweza kujifungua kwa njia ya kawaida!"
Je mwanamke mwenye mshono miezi 14 anaweza kujifungua kawaida
Hapana
Je mwanamke mwenye mshono wa miaka minne na miez 5 anaweza kujifungua kawaida
Soma hapo juu
Mimi nilibeba mimba operesheni ikiwa ina mwaka mmoja na sahivi innaelekea miaka miwili na nina ujauzito wa miezi tisa naweza kujifungua kawaida?
Naomba usome somo vizuri utapata jibu lako kwa 100%