Je Mtoto kucheza zaidi Tumboni mwa Mjamzito huwa ni hatari?

Je Mtoto kucheza zaidi Tumboni mwa Mjamzito huwa ni hatari?

Je Mtoto kucheza zaidi Tumboni mwa Mjamzito huwa ni hatari?

Kwa kawaida Mtoto anaweza kucheza kuanzia Mara 3 mpaka Mara 100 ndani ya saa 1!

Tafiti nyingi zilionesha ya kwamba kupunguza kucheza kwa Mtoto Tumboni mwa Mjamzito huwa ni hatari zaidi ukilinganisha na Mtoto kuongezeka kucheza Tumboni mwa Mjamzito.

Japokuwa tafiti za Miaka ya hivi karibu zimeonesha kwamba 10% – 30% ya Wajawazito walio jifungua Watoto waliofariki au Mimba ambazo Watoto waliofia Tumboni akina Mama hao wali ripoti historia ya kuongezeka kucheza kwa Mtoto ghafla tumboni.

Mjamzito tambua ya kwamba Mtoto huongezeka kucheza taratibu taratibu kadiri Mimba inavyokuwa yaani kuongezeka kwa umri wa Ujauzito tokea umeanza kuhisi Mtoto anacheza tumboni mwako Mara nyingi kuanzia wiki ya 16 mpaka 18 kwa Mjamzito aliyewahi kuwa Mjamzito na wiki ya 18 mpaka 20 kwa Mama aliyebeba Mimba kwa Mara ya kwanza na kufikia wiki ya 32 ndipo Mtoto hucheza zaidi kuliko kawaida baada ya hapo huweza kupunguza kucheza au kuendelea kucheza kawaida mabadiliko hayo ni ya kawaida kabisa.

KUMBUKA: Ewe Mama Mjamzito endapo Mtoto wako Tumboni ameongezeka kucheza ghafla, Ni vema kuweza kwenda hospitali mapema unapohisi Mtoto ameongeza kucheza au amepunguza kucheza Tumboni mwako ili kuepuka kumpoteza Mtoto wako kabla ya kujifungua, hii ni kwa sababu ni vigumu kujua ameongeza kucheza ni mabadiliko ya kawaida au kuna shida fulani Tumboni mwako.

MAMBO YANAYOPELEKEA MTOTO KUONGEZEKA KUCHEZA TUMBONI MWA MJAMZITO.

Mambo yanayopelekea Mtoto kuanza kucheza zaidi ya kawaida ghafla huwa inaweza ashiria hatari kwa mtoto.
Na mambo yanayopelekea hivyo ni Kama ;

1. Hofu ya Mjamzito.

2. Matumizi ya Caffeine kwa Mjamzito

3. Upungufu wa hewa safi kwa Mtoto akiwa tumboni(asphyxia) ambapo huweza pelekea Dege Dege kwa Mtoto akiwa tumboni.

4. Kujifunga au kubanwa kwa Kondo la nyuma (cord entanglement).

5. Magonjwa fulani ya kuambukizwa kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto akiwa tumboni.

MUHIMU: Ni vema Mjamzito kuwa hospitali ili kuepuka kumpoteza mwanao pale unapoona amepunguza kucheza au ameongezeka kucheza kwa ghafla Tumboni kuliko kufikiria kuwa ni kawaida, Mara baada ya kusikilizwa mapigo ya Moyo na Daktari au Mkunga hospitali au kufanyiwa Ultrasound ndipo unaweza kujiridhisha kuwa Mtoto yuko salama au lah.

Unaweza kujiunza kupitia video YouTube kwa bonyeza hapo chini:

Mtoto kuongezeka kucheza Tumboni mwa Mjamzito.

Response to "Je Mtoto kucheza zaidi Tumboni mwa Mjamzito huwa ni hatari?"

  • Mke wangu anamenimbia haoni pilika pilika za mtoto tumboni tangu juz. Hii ipoje naomba msaada kujua je Kuna shida ama?

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *