MIMBA ZABIBU
MIMBA ZABIBU
Hii ni aina ya Mimba ambayo hutokea endapo mbegu ya Kiume imerutubisha Yai la Kike ambalo halina kiini au hata kama yai hilo lina kiini basi kiini ambacho hakija kamilika vizuri,
Lakini pia huweza kutokea endapo Mbegu Mbili za Kiume kuweza kurutubisha Yai moja la Kike kwa wakati mmoja, Matokeo yake kuna kuwa na mgawanyiko usio sahihi wa Kondo la nyuma na Kijusi pia.
Vihatarishi;
Mambo yafuatayo yanaweza kuhatarisha kuweza kupata Mimba Zabibu,Mambo hayo ni Kama;
- Mwanamke kubeba Ujauzito akiwa na umri wa chini ya miaka 20 au zaidi ya 35.
- Kuwa na historia ya kupata Mimba Zabibu kwenye Mimba zilizopita.
- Mwanamke ambaye hajazaa au Kuto zaa mapema.
- Ukosefu wa Vyakula vyenye beta Carotene kwa wingi kama Karoti na Spinachi.
- Ulaji wa vyakula visivyo na Vitamini B-9 au Folic acid vile vile ukosefu wa mafuta ya wanyama.
- Japokuwa Mwanamke ana weza kupata hata Kama hakuwa na hivyo Vihatarishi.
Kuna aina kuu mbili za Mimba Zabibu hii ni kutokana na utofauti pale ambapo yai la kike linakutana na la Kiume, katika kipindi cha urutubishwaji wa Yai kwa mbegu ya Kiume.
Ambazo ni kama ifuatavyo;
1. Mimba Zabibu iliyo kamili;
Aina hii ya Mimba Zabibu hutokea pale ambapo Mbegu Moja ya kiume hurutubisha Yai moja la Kike ambalo halina kiini au kiini ambacho hakija kamilika na matokeo yake mbegu moja ya Kiume pekee hugawanyikwa mara mbili, wakati mwingine japokuwa ni Mara chache mbegu mbili za kiume huingia kwa wakati mmoja kwenye Yai moja la Kike ambalo halina kiini na kuwa Mimba, hii ni tofauti na utungaji Mimba wa kawaida ambapo Mbegu ya Kiume na Kike hugawanyikwa ipasavyo.
Kutokana na kutungwa Mimba hii hupelekea hitilafu ya ugawangikaji wa Kondo la nyuma katika sehemu ambayo hutengeneza Homoni ya HCG na kupelekea ongezeko kubwa la Homoni hii na kufanya dalili nyingi zinazotokana na hitilafu ya mgawanyiko huo.
Dalili hizo ni kama;
1.Dalili za ongezeko la Homoni zitokanazo na Tezi ya Madini joto kama; uoga,kukonda,kutetemeka mwili,mapigo ya Moyo kwenda mbigo, kupumua haraka haraka na kushindwa kuvumilia joto.
2. Shinikizo kubwa la Damu katika Ujauzito kabla ya wiki 20 au Miezi Mitano ya Ujauzito ambapo mgonjwa huwa na dalili kama kukasirika haraka,kuogopa mwanga na kizunguzungu na mwishowe mtu huishia kupata Kifafa cha Mimba.
3. Kutapika kupita kiasi katika kipindi Cha Ujauzito hususani mwanzoni mwa Ujauzito.
4. Tumbo kukua kwa haraka kuliko umri wa Ujauzito.
5. Endapo mtu akifanya Ultrasound kwenye Tumbo la Uzazi Mtoto kutokuwepo badala yake huwa kuna na vitufe vya mviringo vilivyo jazwa maji ndani yake kama Tunda la Zabibu ya mezani.
MATIBABU.
Endapo umegundulika kuwa una Mimba ya Zabibu unatakiwa kusafishwa Mara moja na huweza kutibika kwa asilimia 95 hadi 100 endapo umewahi kungulika.
Lakini kwa baadhi ya akina Mama kama asilimia 15 hadi 25 huweza kuendelea kuwepo hata kama umesafishwa.
Dalili zitokanazo na ongezeka la homoni ya HCG mfano; Shinikizo kubwa la Damu la Ujauzito au Dalili kutokana na ongezeka la Homoni kutokana na Tezi ya Madini joto huweza kutibiwa kulingana na Dawa zake kila moja.
Ni vema kuweza kutibiwa mapema kwa sababu endapo ukichelewa kusafishwa huwa ina tabia ya kuwa Saratani baada ya muda fulani ambapo huweza kusambaa sehemu mbalimbali za Mwili ikiwemo Mapafu na kuleta athari kubwa.
UFUATILIAJI.
Baada ya kusafishwa utahitaji kuweza kufuatilia mwenendo kiwango cha homoni ya HCG,kwa sababu homoni hii inapopungua huonesha kuwa ugonjwa wako unapona na hivyo hutopata athari endelevu za Ugonjwa huu au hitilafu hiyo vile vile endapo Homoni hii inaongezeka huonesha kuwa ugonjwa unaendelea kuwemo na huweza kuleta athari nyingi zaidi.
Hivyo utafuatiliwa mwenendo wa Homoni hii kama ifuatavyo kwa sababu kabla ya kusafishwa kiwango chake huwa kimepimwa kiasi hicho hutumika kulinganishwa na kipimo kitakachopimwa Mara ya pili baada ya kusafishwa:
1. Kipimo Cha pili hupimwa masaa 48 tokea umesafishwa na kitalinganishwa na kiwango cha Homoni kabla ya kusafishwa ili kuona kinapungu au lah.
2. Kipimo Cha Tatu hufanyika wiki Mara baada ya kipimo Cha pili na huweza kulinganishwa kama kinapungua au lah.
3. Kipimo Cha Nne hufanyika Mara baada ya wiki moja tokea kipimo Cha tatu na huweza kulinganishwa kama kinapungua au lah.
4. Kipimo Cha Tano hufanyika Mara baada ya wiki moja tokea kipimo Cha tatu na huweza kulinganishwa kama kinapungua au lah.
5. Na vingenevyo vinavyofuata hufanyika kila baada ya Mwezi kwa mfululizo mpaka Miezi sita kuisha.
Endapo kiwango cha Homoni hii kitapungua na kubaki katika kiwango cha kawaida itakuwa ni habari njema na utakuwa umepona kabisa.
Lakini endapo kiwango hicho kitaendelea kuwa juu au kuongezeka kadiri muda uvyokwenda basi ina maana bado shida ipo na Ugonjwa umeendelea kuwepo unahitaji huduma zaidi na matibabu zaidi ili kuepuka athari zake.
Aina ya Pili ni;
1. Mimba Zabibu isiyokamili;
Aina hii ya Mimba ya Zabibu hutokea pale ambapo Mbegu Mbili za Kiume hurutubisha Yai moja la Kike lililo na kiini salama,matokeo yake Mbegu Mbili za Kiume na Yai moja la Kike hutunga Mimba, hii ni tofauti na utungaji Mimba wa kawaida ambapo Mbegu ya Kiume na Kike hugawanyikwa ipasavyo.
Kutokana na kutungwa Mimba hii hupelekea hitilafu ya ugawangikaji wa Kondo la nyuma na utengenezwaji wa Kijusi ambacho hakitaweza kuishi kwa muda mrefu, sehemu ya Kondo la nyuma inayogawanyika huwa haitengenezi kiwango kikubwa cha homoni ya HCG hivyo huwa kunaongezeko kiasi tu la Homoni hiyo ukilinganisha na Mimba Zabibu iliyokamilika.
Mama huweza kuwa na dalili mfano;
1. Kujiona Mjamzito.
2. Dalili nyingine hufanana na Dalili za Mimba Zabibu iliyokamili japokuwa huwa haziwi zaidi kama aina ya kwanza ya Mimba Zabibu.
3. Kutokwa na Damu kwenye njia ya Uke inayoashiria kuwa Mimba imetoka lakini Tishu zilizomo kwenye Tumbo la Uzazi hazijatoka zote.
4. Ukifanya Ultrasound unaweza kuona Mapigo ya Moyo Mtoto, huonesha kuwa Mtoto yuko hai ingawa anaweza kuwa na ukilema au kushindwa kukua vizuri Tumboni mwisho wa siku Mtoto hufariki na Mimba kuharibika.
MATIBABU.
Matibabu ya aina hii ya Mimba huwa ni kusafishwa na hufanana na aina Ile ya kwanza na kwa sababu haina dalili nyingi za hatari ukilinganisha na Mimba zabibu iliyokamilika, hii huweza kutibika na huwa na 4% ya kuwa Saratani au Ugonjwa endelevu hivyo huwa na athari chache zaidi.
UFUATILIAJI.
Mara baada ya kusafishwa unahitaji kufuatiliwa kiwango cha homoni ya HCG katika Mwili wako ili kujua kinapungua au lah kama ilivyoelezewa kwenye Mimba Zabibu iliyokamili hapo juu hufanana hivyo hivyo na hapa.
KUMBUKA:
Kwa kawaida kiwango cha homoni ya HCG huweza kupungua na kuwa katika Hali ya kawaida kwa muda wa wiki 2 hadi 4 Mara baada ya kujifungua Mimba ya kawaida au Mimba kuharibika, Muda wa Miezi miwili baada ya kusafishwa Mimba Zabibu isiyokamili na wiki 14 baada ya kusafishwa Mimba Zabibu iliyokamili kila moja.
Usikose kunifuatilia YouTube kwa jina la Dr.mwanyika
Website ya mamaafya.com
Bonyeza link hii ilikuweza kupakua application ya Mama Afya pale playstore.
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.wapnum.mamaafya
Mwandishi: Dr.Mwanyika
Phone: 0629019936
No comments.