ONGEZEKO LA UZITO KWA MJAMZITO MWENYE MIMBA YA MAPACHA.
Uzito wa mama Mjamzito mwenye Mimba ya Mapacha hutofautiana na Mjamzito mwenye Mimba ya mtoto mmoja kwa kiasi kikubwa Sana, hivyo endepo Mjamzito akiwa na Mimba ya Mapacha anahitaji kuongezeka Uzito maradufu ya mwenye Mimba ya kawaida hii ni kwa sababu ya Watoto wawili waliomo ndani mwake, kuwepo wa kuta zinazo wazunguka watoto zaidi ya mbili na vitu vingine vingi.
Hivyo Mjamzito mwenye Mimba ya Mapacha anashauriwa kufuata utaratibu wa kiafya ili kuhakikisha kuwa mwishoni mwa Ujauzito ajifungue Watoto wenye Uzito stahiki ili kuwa na Afya Bora na ukuaji Bora wa watoto wake.
Ili kuweza kujua ni namna gani ya kujua mwenendo wa Uzito wako katika kipindi cha Ujauzito unatakiwa kufahamu upo katika kundi gani la watu kulingana na uwiano wa Uzito wako na Urefu wako (Body Mass Index).
Uzito wa Mimba ya Mjamzito mwenye Mtoto mmoja unaweza kubongeza link hii
https://youtu.be/i6VH7MFjQyE
Mjamzito mwenye Mapacha huweza kujifungua wiki ya ngapi?
https://youtu.be/HdTgtvFY6jk
Kwa kawaida kuna makundi manne ya watu kulingana na Uwiano wa Uzito na Urefu wa watu (BMI),Makundi hayo ni kama ifuatavyo;
1.Kundi la kwanza ni akina Mama wenye Uzito chini ya 18.5Kg/M².
Hawa ni akina Mama wenye Utapiamlo hawa wanatakiwa kuongezeka Uzito kuanzia kilo 22.7 mpaka kilo 28.2 kwa hiyo akina Mama katika kundi hili wanatakiwa kuongezeka Uzito ndani ya hiko kiwango kuanzia mwanzo wa Ujauzito mpaka mwishoni wanapojifungua .
2.Kundi la pili ni akina Mama wenye Uzito kati ya 18.5Kg/M² -24.9kg/M².
Hawa ni akina Mama wenye Uzito wa kawaida na stahiki hawa wanatakiwa kuongezeka Uzito kuanzia kilo 16.8 mpaka kilo 24.5 kwa hiyo akina Mama katika kundi hili wanatakiwa kuongezeka Uzito ndani ya hiko kiwango kuanzia mwanzo wa Ujauzito mpaka mwishoni wanapojifungua.
3.Kundi la tatu ni akina Mama wenye Uzito kati ya 25Kg/M² -29.9kg/M².
Hawa ni akina Mama wenye Uzito Mkubwa kupindukia hawa wanatakiwa kuongezeka Uzito kuanzia kilo 14.1 mpaka kilo 22.7 kwa hiyo akina Mama katika kundi hili wanatakiwa kuongezeka Uzito ndani ya hiko kiwango kuanzia mwanzo wa Ujauzito mpaka mwishoni wanapojifungua.
4.Kundi la tatu ni akina Mama wenye Uzito kati ya 30kg/M² na zaidi.
Hawa ni akina Mama wenye kiriba tumbo hawa wanatakiwa kuongezeka Uzito kuanzia kilo 11.9 mpaka kilo 19.1 kwa hiyo akina Mama katika kundi hili wanatakiwa kuongezeka Uzito ndani ya hiko kiwango kuanzia mwanzo wa Ujauzito mpaka mwishoni wanapojifungua.
Endapo Mjamzito ataongezeka Uzito chini ya kiwango huweza kupelekea kujifungua Mtoto mwenye chini ya kilo 2.5 na kupelekea Mtoto kupoteza joto kwa haraka zaidi,kushindwa kunyonya kwa wakati na kuwa kwenye hatari ya kupata Magonjwa mbali.
Dalili za Mimba ya Mapacha
https://youtu.be/v_uPcQa_lfU
Endapo Mjamzito ataongezeka Uzito zaidi ya kiasi stahiki huwezi kupelekea Mama kujifungua Mtoto mwenye zaidi ya kilo 4 ambapo huweza kusababisha mama kufanyiwa upasuaji, Mtoto kuishiwa sukari mwilini na huweza kupelekea kifo kwa Mtoto wake mara baada ya kujifungua.
Usikose kutembelea video youtube
No comments.