ONGEZEKA LA UZITO KWA MJAMZITO KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO.
Uchunguzi wa hivi karibuni uligundua kuwa karibu theluthi moja (32%) ya wanawake walipata kiwango kilichopendekezwa cha uzito wakati wa ujauzito na wanawake wengi walipata uzito nje ya mapendekezo (21% kidogo sana, 48% zaidi).
Kwa kawaida Uzito wa Mama Mjamzito unatakiwa kuongezeka kuanzia wastani wa kilo 11 mpaka kilo 12.7 kuanzia mwanzoni mwa Ujauzito mpaka kujifungua.
Yani Miezi mitatu ya mwanzo Mjamzito anaweza kuongezeka kilo 1 hii ni kutokana na changamoto mbalimbali mwanzoni mwa Ujauzito, huweza kuongezeka kilo 5 na pia kuongezeka kilo 5 miezi mitatu ya mwisho ya Ujauzito hivyo basi kuanzia miezi minne mpaka miezi tisa Mjamzito huongezeka kwa wastani wa kilo 1 kwa kila mwezi.
Ili kuweza kujua ongezeko la Uzito wakati wa Ujauzito ni lazima kuweza kujua uwiano wa Uzito na urefu wako ambapo kitalamu huitwa Body Mass Index (BMI) na kizio chake huwa ni Kg/M²
Kulingana na Uwiano wa Uzito na Urefu wa Mama husika kuna aina nne(4) za makundi ya watu.
Ambazo ni:-
1. Akina Mama wenye utapia mlo ambao BMI yao huwa chini ya 18.5kg/M².
Endapo upo katika kundi hili unatakiwa kuongezeka Uzito kati ya kilo 12.7 mpaka kilo 18.2 tokea ulipo pata Ujauzito mpaka kujifungua.
2. Akina Mama wenye Uzito wa kawaida ambao BMI yao huwa kati ya 18.5kg/M² mpaka 24.9kg/M².
Endapo upo katika kundi hili unatakiwa kuongezeka Uzito kati ya kilo 11.4 mpaka kilo 15.9 tokea ulipo pata Ujauzito mpaka kujifungua.
3. Akina Mama wenye Uzito mkubwa kupindukia ambao BMI yao huwa kati ya 25kg/M² mpaka 29.9kg/M².
Endapo upo katika kundi hili unatakiwa kuongezeka Uzito kati ya kilo 6.8 mpaka kilo 11.4 tokea ulipo pata Ujauzito mpaka kujifungua.
4. Akina Mama wenye kiriba tumbo ambao BMI yao huwa kuanzia 30kg/M² au zaidi.
Endapo upo katika kundi hili unatakiwa kuongezeka Uzito kati ya kilo 5 mpaka kilo 9.1 tokea ulipo pata Ujauzito mpaka kujifungua.
Unaweza kusikiliza video hii hapa
Response to "ONGEZEKA LA UZITO KWA MJAMZITO KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO."
Habari ndugu
Ongezeko la uzito tumboni linatokana
Na nini doctor.
Kwa Mjamzito au Mtoto yoyote?
Me kabla ya mimba nilikuwa na kilo 70 nikapima kilo mimb ya wki 5 nikakuta na kilo 76 nikapima kilo mimba ya wiki 11 nikakuta na kilo 86 je izi kilo ni sahihi auzinapand san nijib pls
Hakuna shida ila uzito wako unaongezeka kwa kasi sana, jitahidi kupima presha pia mara kwa mara