ULAJI WA UDONGO KWA MJAMZITO

ULAJI WA UDONGO KWA MJAMZITO

ULAJI WA UDONGO KWA MJAMZITO

Ulaji wa Udongo kwa Mjamzito ni hali ya kawaida na hujumuisha asilimia 20 ya Wajawazito wote Duniani, Mjamzito anaweza kupata tatizo hili katika Miezi Mitatu ya mwanzo ya Ujauzito, Japokuwa huweza kuwaathiri Wajawazito katika vipindi tofauti tofauti vya Ujauzito, Pamoja na hali hii ya kula Udongo kuna baadhi ya Wajawazito hupendelea kula vitu vingine visivyo na manufaa/mengenywa katika Mwili, hii inaweza kupelekea Mjamzito kupata matatizo mbalimbali ikiwemo kupata Minyoo kutoka kwenye Udongo au uchafu, Sumu, kuziba kwa Utumbo na nk.

Hali hii ya kula Udongo au Vyakula visivyo na manufaa katika Mwili,endapo ikizidi kiasi kwamba inaweza kudhuru afya ya Mama kwa namna yoyote ile huitwa Pica. Hali hii pia huweza kuhusishwa na Magonjwa ya kisaikolojia au Magonjwa ya akili,vile vile huweza kuathiri Watoto wenye umri wa zaidi ya miaka miwili kwa asilimia 25 hadi 30.

Pica ni Tatizo au Ugonjwa wa kisaikolojia au hali ya kula vitu ambavyo havina umuhimu au manufaa katika Mwili kuliko kawaida Mfano; Mjamzito kula vitu kama Mchanga, Udongo,Mawe,Barafu,Mkaa, Majivu na nk kupita kiasi. Neno “Pica” lilitokana na neno “Magpie”, la Kilantini ambalo ni jina la Ndege mmoja mwenye tabia ya kula karibia kila kitu anachokutana mbele yake ndipo walifananisha na ugonjwa huu unapo muathiri Mwanadamu.

Ili Mtu aweze kuwa na Ugonjwa au tatizo hili anatakiwa kukidhi vigezo vinne ambavyo ni Kama ifuatavyo;

1.Kula vitu visivyo na manufaa katika Mwili kama ilivyotajwa hapo juu kwa Muda wa kuanzia mwezi mmoja na zaidi.
2.Kula vitu hivyo ambapo ni tofauti na taratibu au utamaduni katika jamii husika.

  1. Ulaji wa vitu visivyo meng’enywa au kuwa na manufaa mwilini bila kuhusisha ukuaji wa huyo Mtu.
  2. Endapo Mtu huyo ana Magonjwa ya akili, Mjamzito au Usonji anatumia vitu hivyo zaidi ambapo huhatarisha hali yake kiafya kutokana na kula vitu hivyo na Mtu huyo huhitaji Vipimo au matibabu zaidi ijapokuwa alipata matibabu mwanzo kuhusiana na hali hiyo.

MAMBO YANAYOPELEKEA ULAJI WA UDONGO KWA MJAMZITO.

Mambo yanayopelekea Ulaji wa Udongo kwa Mjamzito haya fahamiki,
Lakini vitu vifuatavyo vinaweza kuhatarisha hali hiyo;
1.Ukosefu au Upungufu wa Damu kutoka na Upungufu wa Madini Chuma.

  1. Upungufu wa Vitamini mbalimbali katika Mwili wa Mjamzito.
  2. Utapia mlo au Upungufu wa Madini muhimu katika Mwili mfano; Upungufu wa Madini ya Zinki.
    4.Msongo wa Mawazo na Uoga au kuogopa huweza kupelekea hali hii.
    5.Magonjwa ya akili

MATIBABU NA JINSI YA KUDHIBITI
Unatakiwa kwenda hospitali na kufanyiwa Vipimo kwa ajili ya kuangalia uwingi wa Damu katika Mwili vile vile unatakiwa kupewa Vitamini na Madini mbalimbali kama Madini Chuma na Zinki ili kuweza kudhibiti hali hiyo katika kipindi Cha Ujauzito bila kusahau tiba ya kisaikolojia.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *