Chanjo ya Ugonjwa wa Pepopunda (Tetanus) kwa Mjamzito!
PEPOPUNDA (TETANUS)
Ni ugonjwa ambao huathiri watu wa rika zote na umri wowote ule na Ugonjwa huu huweza kuathiri Mfumo wa fahamu unao husika na Misuli inayojiunganisha na Mifupa ambayo huratibu matendo ya hiari, Mara baada ya kupata Maambukizi ya vijidudu husika kwa kupitia kidonda au mpasuko fulani wa mwili katika sehemu fulani ya Mwili kutokana na sumu inayozalishwa na vijidudu waitwao Clostridium Tetani.
Vijidudu hawa aina ya Clostridium Tetani hupendelea mazingira ambayo huwa na hewa safi (Oksijeni) chache au pasipo na hewa safi yaani mazingira ambayo kuna hewa chafu ya Karbonidioksaidi, endapo Wadudu hawa wakiwa kwenye mazingira yenye hewa safi huweza kuathiriwa na ili kuweza kuepuka, Athari hizo hujigeuza na kuwa kama mbegu (Spores) ambapo huwa watulivu na hawana mjongeo wowote.
Inawezekana tokea umezaliwa mpaka umekuwa Mtu mzima hujawahi kukutana na Mgonjwa wa Ugonjwa huu wa Pepopunda au inawezekana hujawahi kupata kabisa, hii ni kwa sababu ya matumizi makubwa na mazuri ya Chanjo ya Ugonjwa huu (Tetanus Toxoid Vaccine),endapo kama mtu hakuweza kupata chanjo hii Mara baada ya Mambo yafuatayo;
- Kujikata na kitu chenye ncha kali kama Kisu chenye kutu ,Jembe lenye kutu,Shoka lenye kutu,Panga, wembe wenye kutu na nk ambavyo vimekuwa na wadudu hao.
- Kujichoma na kitu chenye ncha kali mfano msumari wenye kutu, mwiba au Vyupa vilivyo na wadudu hao.
- Endapo mtu ameungua baada ya kupata Ajari ya Moto.
- Mtoto Mchanga baada kupata maambukizi kupitia kitovu endapo kisu au mkasi uliotumika kukatia kitovu ulikuwa mchafu au Maambukizi ya vijidudu hao.
- Kupitia Michubuko kwenye Ajari
Endapo vijidudu hao walipata nafasi ya kuingia kwenye kidonda huweza kuzaliana na kutengeneza sumu za aina mbili ambazo Ni:
a. Tetanolysin Sumu hii haina athari kubwa Sana ukilinganisha na sumu aina ya pili.
b. Tetanospasmin ni Sumu ambayo hutolewa na Clostridium Tetani sumu hii huwa na athari kubwa hata kama imekuwa katika kiwango kidogo Sana,
Endapo sumu hii ikiweza kwenda kwenye mfumo wa fahamu(CNS) hususani kwenye mfumo wa fahamu ambao unahusika na Misuri inayoratibu matendo ya hiari basi huweza kupelekea kupungua kwa ile hali ya kujilegeza kwa Misuri hiyo baada ya kufanya kazi na Misuri hiyo huendelea kukakamaa muda wote hata Kama haifanyikazi inayohitaji Misuri hiyo kuweza kukaza.
DALILI ZA UGONJWA WA PEPOPUNDA (TETANUS)
Dalili za Ugonjwa huu huweza kuonekana kuanzia siku ya 4 Hadi ya 14 mara baada ya kupata Maambukizi ya vijidudu hao. Na dalili hizo huwa ni Kama:
1. Kuchemka.
2. Misuri ya mwili kukakamaa au kukaza (Risus Sardonicas, Trismus na Opsthotonus).
3. Mapigo ya Moyo kwenda Mbio.
4. Kushindwa kupumua.
5. Mwili kupinda kutokana na athari za Misuli kukakamaa.
MATIBABU
Matibabu ya ugonjwa huu hulingana na athari za Ugonjwa huu kwa mgonjwa husika lakini wagonjwa wengi hupewa Dawa iitwa Tetanus immunoglobulin ambayo huweza kupunguza sumu hiyo vile vile huweza kupewa Dawa nyingine, ingawa ili kuepukana na adha za Ugonjwa huu Ni vema kuweza kutumia Chanjo Mara baada ya kuumia au kupata kidonda katika mazingira yasiyo salama.
MAMA MJAMZITO NA MTOTO MCHANGA
Kuna umuhimu mkubwa wa Mjamzito na Mtoto Mchanga kuweza kulindwa na Ugonjwa huu kwa kupewa Chanjo stahiki ili kuepuka athari za Ugonjwa hususani kwa Mtoto Mchanga katika kipindi ambacho Mjamzito anajifungua na kukata kitovu.
RATIBA YA CHANJO YA PEPOPUNDA (TETANUS TOXOID VACCINE)
Kwa kawaida Mwanamke ambaye anaweza kubeba Ujauzito au Mimba (Umri wa miaka 18 mpaka 45) na Mjamzito wanatakiwa kupata Chanjo hii Mara tano ambapo huwa ulinzi wa zaidi ya miaka 20.
Mjamzito anatakiwa kupata Chanjo hii kama ifuatavyo:
- Chanjo ya Kwanza hufanyika kwa mara kwanza endapo Mjamzito anaenda kliniki akutanapo na mhudumu wa afya.
- Chanjo ya Pili hufanyika Mara baada ya mwezi Mmoja au wiki 4 baada ya kupata chanjo ya Kwanza.
- Chanjo ya Tatu hufanyika Mara baada ya Miezi 6 baada ya kupata chanjo ya Pili.
- Chanjo ya Nne hufanyika Mara baada ya Miezi 12 au mwaka mmoja baada ya kupata chanjo ya Tatu.
- Chanjo ya Tano hufanyika Mara baada ya Miezi 12 au mwaka mmoja baada ya kupata chanjo ya Tano.
Ni vema kuweza kupata walau Chanjo tatu za mwanzo ambapo huweza kukusaidia kukulinda na Ugonjwa huu endapo umepata michubuko au vidonda baada ya kupata Ajari na huweza kukulinda kwa asilimia 80.
Usikose kunifuatilia YouTube kwenye channel ya Dr.Mwanyika
Response to "Chanjo ya Ugonjwa wa Pepopunda (Tetanus) kwa Mjamzito!"
Nilikua nauliz mimi ni mjamzito wa miez mi5 n nusu nishapat chanjo mbili za pepopunda jana nilijichoma na kiway chenye ncha je nilazima nikapige sindano y tetnus
Hapana ndugu yangu
Mih nilikuw nauliz “chanjo ya kwanz ukishachom ina mashart yyt lbd maan mih nimechoma ila bega linanium vby cn. Nifanyj
Pole sana ndugu yangu inategemeana na mtu aliyekuchoma sindano nunua Dawa za maumivu tumia ndugu yangu.
Nimechoma chanjo hii mimba ikiwa na miez mitatu kwa sasa imamiezi mitano natakiwa nikachome ya pili?
Naomba usome somo hilo vizuri
Ni kwa muda gani maumivu ya sindano ya chanjo yanadumu,maana kwangu ni siku ya tatu yanaendelea,ni hali ya kawaida au kuna shida?
Ndani ya wiki 2 yatakuwa yameisha
Naomba kufahamu je kama itatokea mjamzito amechomwa sindano ya 3 ya pepopunda kbla ya hyo miezi 6 anapaswa kufanya nn na je kuna madhara?
Haina shida ya mkuu ndugu yangu
Je ukiwahi kuchoma sindano ya pili Kabla ya muda wa Ile ya kwanza kuisha kuna madhara?
Kwa nini uwahi?
Nauliza swali, Mimi nilichoma kinga zile tatu za Kwanza na ya nne Ni baada ya mwaka mmoja sikuchoma ikapita miaka miwili ndio nikaenda hospital wakaendeleza ile kinga ya nne. je hapo ntakua sijaharibu kinga?
Hapana wako sahihi ndugu yangu
Naomba kuuliza kuhusu mtoto iyo chanjo ya tetenasi inakaa kwa mda Gani? maana nmemsikia nurse akisema baada ya miaka kumi na tano arafu mimi ufahamu wangu ni baada ya miaka mitano na mtoto amepita iyo mitano….je, kama amepata jeraha awez kuchoma Tena au anachoma
Ndio anaweza kuchoma
Ukichoma sindano ya kwanza the ya pili ukapitiliza mwezi kuna ttzo lolote au unaweza choma ya pili
Unakuwa umeharibu utaratibu wa hiyo chanjo japokuwa utachoma hivyo hivyo haina namna
Habar Mimi nimejichoma na sindano kwenye goti mapata maumivu makali Sana na pia nimechoma sindano za chanjo 3 je natakiwa nikachome sindano za tetenasi?
Chanjo ipi?
Nampenda kuuliza Mimi nimechoma sindano mbili nilipokuwa mjamnzito2021 juzi nimejikata najembe je napaswa kwenda kuchoma sindano nyingine Tena ?
Ndio
Samahani naomba kuuliza mimi nilichoma sindano mbili za mwanzo ya tatu nilitaka kuchoma tarehe 27 mwezi wa tano nikasahau nikaenda kuchoma tarehe 20mwezi wa sita je ni sawa au natakiwa kuanza upya
Uanze upya ndugu yangu