Je kwa nini Mjamzito hupimwa (Kimo) Urefu wa tumbo?? na Je Urefu wa tumbo humaanisha umri wa Ujauzito???
Kimo au Urefu wa tumbo kitaalamu huitwa Fundal Height ambao ni Urefu kutoka kwenye mfupa wa kinena (Pubic Bone) mpaka kwenye sehemu ya juu ya tumbo au mfuko wa uzazi(Fundus).
Kimo au Urefu huo hufanywa na wahudumu wa afya ili kuweza kuangalia Kama umri wa Mimba katika wiki unaendana na ukuaji wa Mtoto tumboni, kuangalia Kama Kuna Maji ya kutosha kwenye mfuko wa Mjamzito.
Kwa kawaida Urefu huo huweza kuwiana na Umri wa Mimba/Ujauzito endapo Mimba ina umri wa wiki 24 au miezi 6 mpaka umri wa wiki 36 sawa sawa na miezi 9 na pia ikumbukwe kwamba endapo Urefu au kimo hicho kinatofautiana kwa sentimenta 2 pungufu au 2 zaidi ukilinganisha na Umri wa Ujauzito basi huwa haina shida endapo tofauti umekuwa zaidi ya 2 Basi unatakiwa kufanyiwa ultrasound kwa sababu hiyo huweza kuashiria shida fulani inaendelea au kitu fulani kisicho Cha kawaida katika ukuwaji wa Mimba hiyo.
Mambo yanaweza kuathiri Kimo au Urefu huo na kutokuwa unawiana na umri wa Mimba katika wiki 24 Hadi 36 Ni Kama yafuatayo:
1. Akina Mama Wajawazito wenye Viriba tumbo/Obesity.
2. Akina Mama wenye Mimba ambayo watoto wao wanakuaji wa taratibu kuliko kawaida/IUGR.
3. Mimba ya Mtoto mkubwa kuliko Kawaida kuanzia kilo 4 na nk/Macrosomia.
4. Uwepo wa Maji mengi kwenye mfuko wa Uzazi /Polyhydramnios.
5. Kuwepo kwa Maji Machache kwenye mfuko wa Uzazi/Oligohydramnios.
6. Mimba ya Mapacha
Vile vile unaweza kujifunza zaidi kwa kutazama video hii
No comments.