Vyakula anavyopaswa kula mtoto kulingana na Umri Wake.
Kama unapenda mtoto wako awe na Afya bora tunapendekeza fanya haya katika chakula chake ili kuepusha kupata magonjwa yanayoepukika;
Kuzaliwa hadi miezi 6 : watoto wachanga wanapaswa kunywa maziwa ya mama tuu au formula ya watoto wachanga tuu, hutakiwi kuwapa maji.
Miezi 6 hadi 12: Watoto bado wanapaswa kutegemea maziwa ya mama au formula ya watoto wachanga. Mara tu wameanza kula chakula kigumu, wanaweza kuanza kunywa maji kidogo kidogo.
Miezi 12 hadi 24: Watoto wanapaswa kunywa kikombe kimoja hadi vinne vya maji kila siku. Wanaweza kuanza kunywa maziwa mengineyo kama ya Ng’ombe na vyakula vingine.
Miaka 2-3 : Watoto hawa wanapaswa kunywa kikombe moja hadi vinne vya maji kila siku. Wanapaswa kuhamia maziwa mengine na vyakula vingine.
Umri wa miaka 4 hadi 5: Watoto hawa wanapaswa kunywa vikombe 1.5 hadi vitano vya maji kwa siku. Wanapaswa kunywa maziwa yenye mafuta kidogo
No comments.