Mlo Kamili kwa Wajawazito na Watoto
Ni muhimu sana akina mama wajawazito na watoto wadogo kula mlo kamili na ulio salama.
Katika utafiti uliofanyika katika nchi 6 kule Ulaya na ukachapishwa tarehe 16 oktoba 2019,umeonesha kwamba, matumizi ya samaki mara 4 au zaidi ya mara 4 kwa wiki yalihusishwa na 15% ya PCB na vile vile kwa watoto wadogo, kiwango cha mara 3 au zaidi ya mara 3 kwa wiki ilihusishwa na 23% ya mafuta ya juu (PFNA). Vile vile endapo wahanga hawa watatumia matunda au mboga za majani ambazo ziliwekwa dawa ya kuua wadudu basi wanaweza kupata matatizo kama Kansa,sumu kwenye mfumo wa fahamu,kupunguzwa kwa kinga ya miili yao, kupata fetma na magonjwa yasiyoambukizwa kama kisukari namba 2.
Hii ni kwa sababu ya kemikali kama Polychlorinated biphenyls (PCBs), perfluoroalkyl substances (PFAS)
na organophosphate pesticides (OP)
Ambazo zipo kwenye samaki na madawa ya kuulia wadudu yanayotumika kwenye kilimo cha matunda na mboga mboga.
No comments.