Sababu za Kuumwa kichwa kwa Mama Mjamzito

Sababu za Kuumwa kichwa kwa Mama Mjamzito

Sababu za Kuumwa kichwa kwa Mama Mjamzito

Kuumwa kichwa kwa Mama Mjamzito huweza kutokea kwa sababu ya mabadiliko ya kibaolojia katika mwili wa Mama huyo.

Lakini kumbuka kwamba wanawake ambao wana umri ambao wanaweza kubeba Mimba ndio huongoza kuwa na maumivu ya kichwa kuliko Wanaume,Wanawake baadhi hupata maumivu ya kichwa kutoka(Kipanda uso) kwa sababu ya kubadilika badilika kwa homoni katika mizunguko yao ya siku au Hedhi!

Mama Mjamzito kama unapata maumivu ya kichwa jiulize maswali haya hapa chini!

Swali la 1. Je umekuwa na maumivu katika vipindi fulani fulani tokea angali huna Mimba na maumivu bado yanatokea vile vile bila mabadiliko?

Swali la 2. Je umekuwa na maumivu kwa Mara ya kwanza wakati wa Ujauzito?

Swali la 3. Je ulikuwa na maumivu tokea huna ujauzito na kwa sasa maumivu yamekuwa makali zaidi au yamebadilika na kuwa zaidi?

Swali la 2 na swali la 3 ni maswali muhimu sana kwa sababu kama unapata maumivu hayo, inawezekana una shida fulani naomba soma hapa chini, yawezekana maumivu hayo ni kutoka na sababu hizi👇👇👇👇!

  1. Maumivu kutoka na shida ya kichwa chenyewe:
    Maumivu haya hutokana na shida zifuatazo;

A.KIPANDA USO( MIGRAINE HEADACHE).
Dalili zake;
Maumivu ya kichwa upande mmoja wa kichwa,
Maumivu ya kupwita pwita,
Kupata shida kuona huweza kuambatana na kutapika na kichefu chefu.

MUHIMU;Ukiona dalili hizo kama ni mjamzito wahi hospitali usinunue dawa kiholela.

B. CLUSTER HEADACHE
Dalili zake;
Maumivu kwenye eneo la jicho moja au sehemu ya juu ya jicho Mara nyingi huwa ni upande mmoja wa kichwa na huwa ya kupwita pwita.

MUHIMU; Ili kupinguza maumivu hayo pata hewa safi ya Oksjeni na wahi Hospitali.

C. TENSION TYPE HEADACHE
Dalili zake;
Maumivu huwa pande mbili za kichwa au kichwa chote huwa kama yanabana ukiona dalili hizo wahi hospitali.

  1. Maumivu ya kichwa kutokana na magonjwa mengine yanaweza kuwa ya kuambukizwa au yasiyoambukizwa.
    Kwa mama mjamzito yanaweza kutokana na Magonjwa kama;
    Kiharusi,kupasuka au kuziba kwa mishipa ya damu kichwani au kwenye ubongo,presha wakati wa ujauzito au dalili za kifafa cha Mimba!

MUHIMU; Presha wakati wa Mimba!,
Endapo umepata maumivu ya kichwa kuanzia wiki 20 au miezi 5 ya Mimba kwenda juu mpaka Wiki 4 Mara baada ya kujifungua,

Response to "Sababu za Kuumwa kichwa kwa Mama Mjamzito"

  • Habari naomba uniandikie dawa ya kipanda uso nina ujauzito wa wiki 20 siku ya pili kichwa kinaniuma sana

  • Kiukwel nashukuru San kwamaan ufafanuzi wako umetusaidia Sana ktk familia yetu. MUNGU AKUBARIKI!

  • Napata maumivu makali kwny kichwa had naona kizito mim ni mjamzito na hii mimba yang ya pili lakini ujauzito wa kwanza hali hii sikuwahi kuwa nayo

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *