Dalili za hatari kwa Afya ya Mama Mjamzito au Kwa mtoto aliyepo tumboni mwake!
Kuna wakati fulani Mama Mjamzito anaweza kupata Dalili ambazo ni hatari kwa Afya yake au Kwa mtoto aliyepo tumboni mwake!
Kulingana na shirika la Afya Duniani (WHO)
limeanisha Dalili Tisa hatari kwa Mjamzito, hivyo Mjamzito anapokuwa na Dalili hizo anatakiwa kujua kuwa ni Dalili hatarishi kwenye Ujauzito wake.
Dalili hizo hatarishi kwa Mjamzito ni kama;
- Kutokwa na Damu katika kipindi cha Ujauzito!
- Kuumwa kichwa wakati wa Ujauzito!
- Kupata homa kali wakati wa Ujauzito!
- Kuvimba Miguu, Vidole vya Mikono na Uso ambapo huambatana na kupata shida ya kuona!
- Kuwa na Dege dege katika kipindi cha Ujauzito!
- Kupata Maumivu Makali ya Tumbo!
- Kupata shida Kupumua!
- Mtoto kupunguza kucheza tumboni.
- Kuchoka kupita kiasi / kuliko kawaida.
Lakini kuna dalili nyingine ambazo zinaweza kuwa za hatari mfano;
- Kupasuka kwa chupa kabla ya uchungu kuanza au kabla ya wakati wa kujifungua!
- Kutokwa na uchafu au magonjwa katika njia ya uzazi na nk.
KUMBUKA; Uonapo Dalili hizo wakati wa Ujauzito basi unatakiwa kupata ushauri kutokwa kwa Mkunga au Daktari ili kuhakikisha unakuwa na Afya!
Response to "Dalili za hatari kwa Afya ya Mama Mjamzito au Kwa mtoto aliyepo tumboni mwake!"
Make wangu mda mwingi tumbo linamuuma alipoi tatizo ni ni?
Mpeleke hospitali akafanyiwe Uchunguzi