MJAMZITO KUNYOA MAVUZI KABLA YA KUJIFUNGUA

MJAMZITO KUNYOA MAVUZI KABLA YA KUJIFUNGUA

MJAMZITO KUNYOA MAVUZI KABLA YA KUJIFUNGUA

Unyoaji wa mavuzi kwa mjamzito kabla ya kujifungua imekua ni utaratibu wa akina mama wajawazito walio wengi ambao hunyoa vuzi muda mfupi kabla ya kwenda kujifungua kawaida au kwa upasuaji.

Wajawazito hunyoa nywele za kwa bibi au mavuzi kutokana sababu mbalimbali kama:

  1. Njia mojawapo ya kujisafisha na kuhakikisha mwili unakuwa safi kabla ya kujifungua.
  2. Kujisikia vizuri na amani kabla ya kwenda hospitali au kituo cha afya kujifungua.
  3. Utamaduni wa baadhi ya koo na makabila kunyoa kabla ya kujifungua mtoto.
  4. Hofu ya kwamba nywele hizo zinaweza kuingia kwenye kidonda endapo mjamzito anajifungua kwa upasuaji.
  5. Hofu ya kusemwa vibaya na manesi au wakunga wakati wa kujifungua endapo mjamzito hakunyoa mavuzi kabla ya kujifungua.
  6. Hofu ya kwamba Damu inaweza kushikana na nywele baada ya kujifungua.
  7. Vuzi huweza kuongeza maambukizi ya vijidudu ukeni na kwenye kidonda baada ya kujifungua.
  8. Kutokuwa na uelewa haswa kwa mjamzito anayebeba mimba kwa mara ya kwanza.

JE NI KWELI MJAMZITO UNATAKIWA KUNYOA KABLA YA KUJIFUNGUA?

Ukweli ni kwamba mjamzito hutakiwi kunyoa vuzi au nywele za kwa bibi iwe unajifungua kwa upasuaji au unajifungua kawaida, muongozo wa WHO mwaka 2018 unaeleza ya kwamba Mjamzito au Mtu yeyote si vema kunyoa vuzi kabla ya upasuaji au kujifungua haswa kama unajifungua kwa upasuaji, japokuwa hata kama unajifungua kawaida unaweza kuchanika au kupata michubuko mbalimbali hivyo haina haja ya kunyoa vuzi au nywele kwa bibi kutokana na sababu zifuatazo;

  1. Huongeza maambukizi ya vijidudu wakati wa kujifungua kawaida au upasuaji, hii ni kwa sababu unapojinyoa kwa mashine au viwembe kuna uwezekano mkubwa wa kujichubua au kujikata na kuwa na vidonda ambavyo huongeza uwezekano magonjwa ya vijidudu.
  2. Unapojinyoa kwa mashine au viwembe unaweza kujikata au kumiza sehemu hizo na kuongeza hatari ya kuwa na maambukizi ya magonjwa ya ngono hata kama si mjamzito.
  3. Unaponyoa kwa viwembe au mashine unaweza kukata nywele vibaya na kuweza kusababisha nywele kujiviriga ndani ya ngozi huweza kusababisha vipele vyenye maumivu makali sana.
  4. Ongezeko la homoni kwa mjamzito na usafirishwaji wa damu sehemu za siri huweza kupelekea muwasho, maumivu na kutojisikia vizuri kwa mjamzito baada ya kunyoa.
Kunyoa vuzi kwa Mjamzito

MJAMZITO FANYA HIZI KABLA YA KWENDA KUJIFUNGUA.

Mjamzito haina haja ya kunyoa nywele kwa kuondoa nywele zote sehemu za siri au ukeni kwa tumia viwembe au mashine badala yake punguza nywele hizo kwa kutumia mkasi endapo unaona unakosa amani kwenda kujifungua na nywele au vuzi ndefu sana.

UNATAKA KUNYOA VUZI ZAKO KABLA YA KUJIFUNGUA.

Mjamzito kama unataka kupunguza au kunyoa kwa kupunguza nywele hizo kwa kutumia mkasi basi ni vema kunyoa au kupunguza nywele au vuzi zako, mwezi mmoja kabla ya kuelekea kujifungua kwa upasuaji au kawaida au ikiwezekana iwe zaidi ya siku 7 hadi 14 kabla ya kujifungua mimba yako.

Kunyoa vuzi kwa mjamzito kabla ya kujifungua

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *