Je Macho mekundu kwa Kichanga husababishwa na nini? (Subconjunctival Hemorrhage)

Je Macho mekundu kwa Kichanga husababishwa na nini? (Subconjunctival Hemorrhage)

Je Macho mekundu kwa Kichanga husababishwa na nini? (Subconjunctival Hemorrhage)

Hali ya Kichanga kuwa na Macho mekundu muda mfupi tokea kuzaliwa ni kawaida haswa kwa Vichanga walio zaliwa kwa njia ya kawaida ila kwa njia za usaidizi kitalaam huitwa Subconjuctival hemorrhage, Hutokea ndani ya Siku 14 au Wiki 2 tokea kuzaliwa kwa Kichanga.

Hali hii huweza kuathiri Vichanga wawili (2) hadi kumi na nane (18) haswa kwa wale wanao zaliwa kwa nji ya kawaida,Macho mekundu kwa Kichanga hutokea pale ambapo vijishipa vidogo vidogo vya Damu vilivyopo kati ya sehemu nyeupe ya Jicho (Sclera) na ukuta angavu wa Jicho (Conjunctiva) ambapo hupasuka na Damu hiyo huvuja na kujaa eneo hilo na Kichanga huonekana akiwa na Macho mekundu kutokana na Damu iliyovilia katika sehemu hiyo.

Mishipa midogo midogo ya Damu au Vijishipa hivyo vya Damu vilivyopo chini ya ukuta angavu wa jicho hupasuka kutokana na ongezeko kubwa la presha kwenye Macho ya Kichanga wakati anapopita kwenye via vya uzazi haswa wakati wa kuzaliwa kwa njia ya kawaida na endapo Uchungu umekuwa wa muda mrefu sana au muda mfupi sana.

Dalili za Damu Kuvilia kwenye Macho ya Kichanga (Subconjuctival hemorrhage)

Mtoto mchanga mwenye hali hii ya kuwa na Macho mekundu kutokana na Damu kuvilia chini ya ukuta angavu wa jicho huwa na dalili kama;

  1. Jicho moja huwa na rangi nyekundu (Damu nyekundu), Hali hii mara nyingi hauthiri jicho moja pekee na mara chache sana huweza kuwa kwenye Macho yote mawili.
Jicho moja jekundu
  1. Rangi nyeundu huonekana zaidi upande wa pembeni mwa Macho au sehemu za chini za Macho ya Mtoto Mchanga.
  2. Macho huwa makendu pasipo kuwa na uchafu wowote unaotokao Machoni.
Macho yote mekundu
  1. Hakuna maumivu yoyote; Hali hii huwa haina maumivu kwa Mtoto mchanga.
  2. Hakuna homa au kuchemka kwa Mtoto mchanga.
  3. Huweza kuambatana na shida nyingine mfano; kuvilia kwa Damu kwenye fuvu au usoni kwa Mtoto mchanga.

Vihatarishi vya Macho mekundu kwa Mtoto Mchanga (Subconjuctival hemorrhage).

Hali huweza kutokea kwa Watoto wachanga baadhi ambao huhatarishwa na baadhi ya vitu,Vifuatavyo ni vihatarishi vinavyoweza kupelekea Kichanga zaliwa na damu kuvilia kwenye Macho yake ndani ya siku 14 tokea kuzaliwa kwao;

  1. Kichanga aliyezaliwa na Mama aliyejifungua kawaida ila kwa njia za usaidizi kama Vacuum au forceps delivery, hii hutokea endapo Mtoto amekwama kwenye via vya uzazi wakati wa kuzaliwa na hupelekea ongezeko kubwa la presha kifuani na machoni kwa Kichanga hivyo huweza kuchangia kupasuka kwa mishipa midogo midogo chini ya ukuta anguvu wa jicho na damu kujaa sehemu hiyo(Hutokea kwa Vichanga 75 kati ya Vichanga 100 walio zaliwa kwa akina Mama waliopata Uchungu wa muda mrefu)..
  2. Kichanga aliyezaliwa kutoka kwa Mjamzito aliyekuwa na Uchungu wa muda mrefu kuliko kawaida (Hutokea kwa Vichanga 33 kati ya Vichanga 100 walio zaliwa kwa akina mama waliopata uchungu wa muda mrefu).
  3. Kichanga aliyezaliwa kutoka kwa Mjamzito aliyekuwa na Uchungu wa haraka kuliko kawaida.
  4. Mtoto mkubwa tumboni huweza kuwa kwenye hatari ya kuwa na hali hii baada ya kuzaliwa.
  5. Vichanga wanaozaliwa kwa njia za upasuaji wa mama zao ni mara chache sana huwa na shida hii.

Matibabu ya Macho mekundu kwa Kichanga (Subconjuctival hemorrhage).

Hali hii hupona yenyewe kwa muda wa wiki 2 hadi 3 tokea kuanza kutokea kwa Kichanga wako haswa kama imetokea kwenye Jicho moja au hata macho yote mawili pasipo kuhitaji matibabu ya aina yoyote,

Damu iliyojaa chini ya ukuta angavu wa jicho hufyonzwa kwa ndani bila kuathiri afya ya Jicho au Macho ya Kichanga wako,hivyo usiwe na wasiwasi hali hii ni kawaida kutokea kwa Vichanga haswa wanaozaliwa kawaida kwa Mjamzito aliyekuwa na Uchungu wa muda mrefu au Kujifungua kwa njia za usaidizi.

KUMBUKA:Ikitokea kwenye Macho pande zote kwa Kichanga wako ni vema kuhakikisha kwamba unaenda hospitali uonane na Daktari bingwa wa Macho aweze kumkagua mwanao na kuhakikisha kama haitokuwa na athari zozote kwa Kichanga wako, Endapo imehusisha Macho yote mawili wakati mwingine huweza kuambatana na Damu kuvilia kwenye Retina ambayo huhusika katika suala la kuona hivyo huweza kuathiri afya Macho kwa Kichanga wako kwa muda mrefu au katika maisha yake ya badae.

Ukiona hivi wahi hospitali

Endapo kichanga wako ana Macho mekundu ambayo huwa na dalili zifuatazo ni vema kwenda hospitali haraka sana;

  1. Kichanga mwenye Macho mekundu pande zote mbili kwa wakati mmoja.
  2. Mtoto mchanga anayepata hali hii ya Macho mekundu baada ya wiki 2 tokea kuzaliwa, Inawezekana ni maambukizi ya Vijidudu au Virusi hivyo huhitaji matibabu ya haraka.
  3. Kutokwa uchafu wa njano au mweupe; Mtoto Mchanga mwenye Macho mekundu yanayo ambatana na kutokwa uchafu wa Njano au Mweupe.
  4. Kichanga mwenye hali hii ikiwa ina ambata na Homa kali au Joto la mwili wake kuwa juu.
Macho mekundu kwa Mtoto Mchanga.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *